Oct 7, 2010

APARTMENT INSTALLATIONS

Wengi wanapenda kufunga DSTV huku local na channel nyengine zikiachwa kwa wapangaji wenyewe kama wanahitaji kutokana na ukweli kwamba wapangaji wengi wa Apartment si wenyeji wa Tanzania hivyo hawaoni umuhimu wa kuangalia channel za nyumbani wakiamini TBC inawatosha ambayo inapatikana kwenye DSTV.Ambacho kinafanyika tunainstall Dish 1 ama 2 mbili kwa apartment nzima,nikimaanisha nyumba zote za wapangaji wa humo kutakuwa na connection ya DSTV ambacho yeye anafanya ni kukunua DSTV decoder tu ambayo hata akihama anaweza kuhama nayo.Hii pia inafanya mazingira ya apartment husika kuwa nadhifu na muonekano mzuri kwa kupunguza wingi wa madish,njia hii inawezekana kwa channel za local ama nyengine pia inategemea na wapangaji husika ama mmiliki wa apartment.
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: