Oct 7, 2010

TOFAUTI YA RECEIVER NA DECODER

Decoder ni kifaa kinachopokea Channel ambazo zipo fixed kwa mfano DSTV,ni lazima ziwe zinalipiwa na kampuni husika,hii inamaana huwezi kupata bure labda wenyewe waamue hivyo ama upite wizi.
 Receiver ni kifaa kinachopokea channel zote zilizopo kwenye satellite,haijarishi kama ni fixed ama zipo zipo tu,ila hii inategemea na muelekeo na setting husika ikizingatiwa freequence.Haina maana kwamba hata zile za kulipia utazipata bure,zipo ambazo utazipata kutokana na ukubwa wa dish na muelekeo na huwa sio zote.
Pia kuna Receiver zinazotumia smart card hivyo unaweza ukapata channel zote za kulipia mf: channel za DSTV unaweza ukapata bila kutumia decoder zao,kitakachokulazimu ni kununua smart card yao.
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: