Dec 13, 2010

Buriani DR REMMY..........!!!

Kiukweli kila kukicha tunapoteza wakongwe katika fani,inasikitisha ila mwisho wa yote inakuwa hatuna jinsi kwa7bu tumezaliwa ni lazima tutakufa isipokuwa tunachogopa ni kutangulia tu....!!
Kifo cha DR REMMY kamwe hakitasahaulika na hakuna wa kuziba pengo lake,kila mtu atakumbuka kwa style yake ila kwangu mimi ni zaidi ya ambavyo wengi wanadhani...!!
Mimi ni kati ya wale watanzania wachache waliopata bahati ya kuzaliwa mjini tena ni maeneo ya sinza pale nyuma ya shule ya Mashujaa kiasi kwamba ukitoka tu nje unakutana na kanisa....!!
Hivyo nikisema hivyo wale ambao wanakumbukumbu nzuri watakumbuka enzi hizo yaani nyumba za hapo kulikuwa na muingilianowa watoto sana yaani hakukuwa na mipaka kwa jinsi tulivyoishi enzi hizo so watoto wa DR REMMY walikuwa home hawapungui nasi kwao kama kawa...!!
Ila tulikuja kuhama sinza mwaka 1993 ambapo ndo ukawepo umbali,kiukweli nimesikitishwa sana poleni sana wana wa familia ya DR REMMY na wapenzi wote wa mkongwe huyu ambaye alikuwa JEMBE.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,Ameen.
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Mungu ailaze roho ya marehemu dr remmy mahali pema peponi.
Amin
Mdau

Anonymous said...

Mh si nasikia wewe umezaliwa mbagala wewe.....!!!
la msingi ni kwamba mungu alaze roho ya marehemu pema peponi.

Mustapha maDish said...

Natamani kucheka uliyesema mi nimezaliwa mbagara lau ningelikuwa nimezaliwa huko pia ningesema kwa wakati wake ila tupo kwenye huzuni jamani...!!
Kwa kumpoteza mtu ambaye alikuwa zaidi ya mwanamuziki..!!
La msingi na tuliloliacha ni kwamba tumuombee m'mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.

Anonymous said...

Welcome To Tommys Bookmarks. [url=http://detailarticles.info/celebrity-stolen-videos.html]detailarticles.info[/url]