Dec 3, 2010

Katika mwaka huu banaa nimepata wasaa ya kupita pita katika matawi kadhaa ya CRDB bank,nilianzia pale Mliman city branch,nikaja pale Azikiwe branch na leo nipo hapa Mikocheni branch.
Hili bana ni tawi jipya,hapa ilifungwa DSTV ila ikawa kesi kubwa ni kupoteza signal,katika kutafuta 7bu nikagundua ya kuwa ilipofungwa ilikuwa si sehemu sahihi kutokana na kuwa na movement nyingi eneo hilo la mafundi wa AC.Hivyo nikaona solution ni kulihamisha kutoka chini na kuliweka juu na ilikuwa kama ifuatavyo:-

Hii inaonekana imekaa vema ila tatizo likawa inaguswa guswa,mfano tulikuta ngazi ya mafundi wa AC na ndo ambao walifanya tuitwe baada ya kuigonga na ngazi yao hiyo ya mabomba bomba. Ili tatizo liishe nikaona ni vema kuihamisha na kuiweka juu ambapo ni ukutani.
Hapa wafanyakazi pamoja na wateja wanasafisha macho kwenye hii flat.
nami kipindi hicho nakusanya kilicho changu na kuchapa mwendo.....!!

4:20 AM   Posted by Mustapha Hanya with 4 comments

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hivi kuhamisha Dish si ni kufungua tu ama kuna effect yeyote,maana karibuni nitahama ninapokaa sinza na kuhamia kibamba,hivyo nilitaka kuwasiliana nawe baada ili uje kunifungia,
nina DSTV na lile la za bure Tanzania na machannel za nje.

Anonymous said...

Habari,huku kwetu mkuu kuna jamaa anatufungia DSTV na kwa mwezi tunalipia 5000 tu lakini ambacho anafanya ukihitaji anakuvutia waya mpaka nyumbani kwako na mpira tunaangalia hii inakuwaje maana hatupati channel nyingi...!!
John s.
Serengeti,Tanzania.

Mustapha maDish said...

Bwana John hiyo issue ina maana kwamba haukufungiwa Dish wala hupewi Decoder...??
Kama ndivyo huyo jamaa kafanya installation kama ya nyumba moja na kila nyumba anayopeleka inakuwa ndo kama chumba katika nyumba hiyo,so controler inakuwa kwake akibadili nayo kwako inabadilika otherwise awe na decoder zaidi ya 1....!!
Zaidi ya yote jua ya kuwa siku yeyote mfumo huo utakufa maana yeye amechukua kwa matumizi binafsi lakini anafanya biashara maana yake kama wahusika wataamua kumfuatilia anayo kesi ya kujibu.

Mustapha maDish said...

Kama unaidea unaweza kufungua ila kinachotakiwa ni umakini wa ubebaji wa Dish na uangalizi wa LNBF...!!
Maana kama dish utaibeba vibaya na kuigonga gonga ukafanya ikapinda itamuwia vigumu fundi kupata signal na akilijua hilo itakuwa imekula kwako,yupo ambae anaweza kulinyoosha na kupata vipimo vile vile na yupo ambaye hawezi hivyo atakununulisha dish mpya na upande wa LNBF vivyohivyo...!!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search