Dec 19, 2010

Dish hii haina uwezo....!!

Dish ndogo ( ku satellite dish ) haina uwezo wa kukamata channel zilizopo cband kama kwa mfano channel za Tanzania,pia haina uwezo wa kuondoa chenga zilizopo kwenye Antenna uliyofunga kwa ajili ya local kwani haina muingiliano wowote na channel zilizopo kwenye transmetter zaidi ya yote inatumia lnb ndogo tu.
Kwa kuongezea ukifunga Dish huwezi kumuona jirani yako akiwa anafanya mambo yake,maana wapo wanaoamini na kutoa soga za kwamba ukifunga dish ndo kila kitu hata mwizi wako unamuona jamani jamani si hivyo hayo mambo ni ya CCTV camera,nadhani nimesomeka......!!

Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Umesomeka mkuu,nimesikia kuna DSTV za magumashi vipi etii hii ipo??
Ukifunga inakuwa ndio umefunga hakuna malipo ya mwezi unasemaje hapo??

Anonymous said...

mimi nimeona ila kwa sasa jamaa haoni vipi hao dstv wamegundua nn?
Kama vp hiyo ndo issue hata mm nataka nitapaje hiyo ambayo haina malipo ya mwezi?

Mustapha maDish said...

kuhusu dstv za magumashi siwezi nikasema zipo ama hazipo ambacho naweza kusema naanda post ambayo itafafanua kwa kina kuhusu dstv bila malipo ya mwezi,maana napata email na simu nyingi nikiulizwa swali hilo...!!
La msingi tembea na mimi katika ukanda huu utang'amua meengi...!!

Anonymous said...

ahsante kwa kutuletea hii kitu nimekupigia kwa number zote hupatikani,nipo mlandizi hapa tuna ofisi yetu mpya tunafungua january kwa hivyo tulitaka huduma.
Nimekutumia contact zetu kwenye email yako,kama utapiga simu iwe saa 2:30-11:30 jioni daily kasoro jumapili na itakuwa vizuri tukiwasiliana siku mbili hizi....!
Kscw