Dec 19, 2010

EURO MIND Antenna

Si wanainchi wote ambao wana uwezo wa kufunga Dish ama king'amuzi kutokana na hali ya maisha jinsi ilivyo na kwa upande wa pili pia si channel zote za nyumbani zinazopatikana kwenye Satellite Dish ama hata penye king'amuzi pia,hivyo swala la Antenna linabaki pale pale kwamba ni la muhimu si uwezo ijapokuwa linahusika pia.
Kwa wapatao tabu kuhusu Antenna ipi inaweza ikawasaidia kuona picha clear kutokana na eneo waishilo,jibu ni moja tu EURO MIND Antenna na ikitokea haishiki basi ujue eneo lako halistahili Antenna.
Kwa wale wenzangu na mimi wa uswazi kuna zile tube ambazo unazifanyia mambo na kuwa bonge la Antenna.
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

6 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Mkubwa umejuaje kama tupo watu wa Tube...!!!
Eeehee na hiyo euromind c ndio milaki..??
Eti mkuu nikuulize zamaani nilikuwa nasikia eti mtu ukifunga dish unaweza ukaona hata mtu akiwa chooni hapo jirani yako,je ni dish aina gani hizooo....!!
Au ilikuwa ni fix...!!

Mustapha maDish said...

Ahahahaa...!!
sio kwamba nakucheka bali umenichekesha hiyo issue ya ukifunga dish hata wa chooni unamuona si kweli maana kila ukifunga dish unaweka frequency maalumu kwa satellite husika,huduma hiyo ni mitambo mengine kama CCTV..!!
EUROMIND wala sio kama udhaniavyo mkuu.

Anonymous said...

mi nipo na ile wanaita soneti na inaonyesha baadhi vizuri tu lakini kama tbc1,channel10,na c2c sizipati vizuri,inakuwa mpaka tuzungushe,je hiyo euromind itaonyesha clear zote hizo.....??

Mustapha maDish said...

kiukweli ambacho naweza kusema euromind imeiacha soneti hatua 3 nyuma,nikiwa na maana euromind ipo juu ya soneti kwa ubora...!!
Lakini siwezi kusema kama ukifunga euromind hizo channel usemazo zitaonyesha clear kama utakavyo..!!
Sijui upo maeneo gani?
Ila mpaka hapo nadhani umenisoma...!!

Anonymous said...

Kaka mimi nimeuziwa hii EURO MIND isipokuwa hakuna nafuu yeyote nipo maneo ya mbezi.

Anonymous said...

Nitajuaje kama Original or Fake??