Dec 28, 2010

Kwa kuanza tu naweza nikasema kwa mwaka huu 2010 ni mwaka mgumu sana hasa kwa vijana,yananitoka haya kutokana na mazungumzo yao pale unapokaa nao,maana wenyewe wanakwambia hakuna njia kama milango inazidi kufungwa ili watu wasitoke,hivyo kipindi wao wanasema hivyo sijui wewe unasema aje kuhusu mwaka huu unaoishia.....!!
Upande wa kazi banaa jua halikuwa kali saana maana ushindani ulikuwepo ila si mkali sana ni wa kawaida tu,ilizaliwa kampuni inayojulikana kama star times ambayo kuna mkono wa TBC na wachina,ambao wamekuja tofauti kidogo,badala ya kutumia dish wao walitumia Antenna na decoder,ni kitu kizuri na watanzania wamekipokea ila si kama ambavyo walidhani hasa baada kufa GTV na kusemekana inakuja kampuni ambayo itakuwa inafanana na GTV ili kuleta ushindani na DSTV katika swala la mpira kuhusu malipo ya mwezi,sitaki kuelezea sana ila tukaitambua star time na utofauti wa kutumia antenna ila yenyewe si ya kwanza ilitangulia EASY TV ambayo mpaka sasa bado ipo na inafanya vizuri pia.
Pia ATN nao wametoa ving'amuzi vyao ikiwa hawana tofauti na star time ila wao wapo kidini zaidi na channel zao,hii ina maana kwamba kwa mwaka ujao 2011 kutakuwa na mapokezi ya vingamuzi vyengine toka kwa wamiliki wa makampuni ya habari Tanzania,ugomvi wa kibiashara ndio sababu ya kuwaumiza watanzania kwa kuwalazimisha kujaza decoder majumbani kwao.......!!
Star times ilitosha kabisa kukidhi mahitaji ya watanzania ijapokuwa Easy tv nao walikidhi ila sijui sababu ni nini mpaka wakatolewa maana na TBC kuamua kuanzisha ya kwao ambayo channel zote za Mengi hazipo,ikisemekana hawataungana maana wana ugomvi wa kibiashara,huku easy tv ikiwa na channel zote za local mpaka TVZ.....!!
Ni meengi sana kipindi tunaendelea kukumbuka lichukue hili...!!
10:24 AM   Posted by Mustapha Hanya with No comments

0 Unasemaje..??:

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search