Dec 18, 2010

Segerea ilikuwa pangu pa kavu....!!

Offer bado inaendelea nami nazidi kusababisha watu wafurahie maisha,nilikuwa maeneo maeneo wanapaita segerea ambapo nyuma ya nyumba hizi ndipo ilipo gereza la segerea.....!!
Hapa tatizo kubwa lilikuwa ni pa kufunga dish maana nyumba ilikuwa imejengwa kiaina yake,kwa kawaida ili dish likae kwa uzuri na usimwite fundi kila baada ya muda ni lazima tudrill ukutani lakini sometimes inakuwa haina jinsi kama ilivyo hapa na ndio tukaamua tufunge kwenye mbao ili tu mwenye yake aweze kuona kama yalivyo matakwa yake......!!
 Tumeangalia ubora wa mbao kama kweli unaweza kubeba dish na ndipo tukafunga maana unaweza ukafunga ile unaondoka tu unapigiwa simu ya kwamba dish lipo chini....!!

Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: