Dec 19, 2010

Ili mkono uende kinywani na hata ukikosa kicheko basi likutoke tabasamu ni lazima pesa zikutembelee,hata zikiwa za msimu na kwa kulijua hilo ndo maana watu wanaamka asubuhi wanajituma sana ilihali ankala ipatikane na maisha yaweze kwenda as usually banaa....!!
Kipindi wewe unaumia kutafuta pesa mwengine anaumia jinsi gani atakavyokuchukulia kiulaini na kuondoka nazo,akikuacha kwenye majuto ya ningejua ningenunua hata nanii... ila inakuwa ushachelewa wenye kazi zao washachukua mahela yao...!!
Kiukweli nilichogundua tunapenda sana shortcut ya maisha ila tunasahau misemo ya wazungu yenye maana kubwa sana,NO PAIN NO HONEY au NO GANE WITHOUT PAIN sasa iweje tupende vizuri bila kutaabika...??
Maisha ni magumu sana tena na bila kujituma kamwe hauwezi kutoka na kupenda shorcut madhara yake ni makubwa sana,pesa bila kufanya kazi ni sawa na kulipwa kabla ya kazi maana kazi utakuja ifanya tu siku za usoni,tena inaweza ikawa ni ngumu kuliko malipo ambayo ulikwishapokea,kuwa makini especially vijana wenzangu..!!
 Hii ni picha tu ambayo najua itakuwa imewatamanisha wengi na kudhani nina zaidi ya hizo kwenye akiba yangu kumbe ni picha tu wanaharakati wenzangu....!!
Nimeandika hii kutokana na jamaa fulani ambao waliwahi kunipigia simu kitambo kidogo,wakidai kunifahamu sana na kudai kuna wazungu wamefikia hotel hapa dar na walitaka kufanya biashara hivyo hawana mwenyeji,jamaa mmojawapo katika mtandao huo ambaye alijifanya yupo mkoa na ndiye ananijua mimi kwa maelezo yake,akaomba mimi niwe mwenyeji na kuna madawa ya mazao ama kitu kama mifugo ambayo yanapatikana s.group hivyo niwe kama mtu wa kati then nitapata % fulani....!!
Kusema kweli alivyokuwa ameanza huyo jamaa ndipo alipokosea na nikagudua hanijui bali alipata contact zangu kutoka mtandaoni ama kwa mtu hivyo hata dili yenyewe ilikuwa ya uongo kama jinsi alivyoanza nami nikawapotezea.....!!
Baada ya muda jamaa yangu mmoja nae akanihadithia kama ambavyo mimi nilikumbana nayo ila yeye ikawa wamefika kwenye suala la kutakiwa kutoa pesa kidogo ili apate kingi....!!
Kama ni watanzania ama wageni tunaenda wapi....???
Umakini katika pesa iwe wa hali ya juu otherwise mtalia jamani.....!!
7:51 AM   Posted by Mustapha Hanya with 7 comments

7 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kwanza hongera kwa blog yako kijana tena bil kuficha ndo kwanza nimeona hiki kitu kwenye list ya afrigator umefanya vizuri ingawa mimi sipo Tanzania ila siku nikiwa huko nitanufaika na huduma zako.
unaambiwa ukimchunguza bata huwezi mlaa kwani patikanaji wa hela robo tatu ni kudhurumu tu hivyo usishangae mdogo wangu kama wewe umegutuka kaa pembeni na mwengine alie...!!

mustapha Hanya said...

Ahsante mzee kwa kupenda ambacho nimefanya...!!
Ila si mbaya kukumbusha wengine ili wajue isije ikawa huwezi kuwa wa mjini mpaka uingizwe mjini...!!

Anonymous said...

Hao jamaa ndo wamefanya deal hiyo kumbe hata wewe walikuingia,mimi waliwahi kumdhulumu ndugu yangu laki 5 na wakayeyuka ila kwa sasa wamesahau wamerejea tena ila safari hii lazima kieleweke.
John wa Dar es salaam.
Tanzania.

Anonymous said...

bwana mdogo inaonyesha unazo unazo,okey tutazifuata maana hujui matumizi yake,ww unadhani watu wanaishije maisha mazuri?
Tunamiliki vipi watoto wazuri bila ya kuwa na pesa na ukizitafuta kihalali unachelewa.
Ongelea tu madish na ukanda wa kazi zako huku si kazi yako chunga kijana.

Mustapha maDish said...

hivi inawezekana pesa atafute mwengine matumizi ujue wewe,hivi utazitumia kwa uchungu kweli..??
Daima dumu nitasimamia na kutetea ambacho najua kitakuwa na manufaa kwangu na kwa taifa langu kwa ujumla...!!

Anonymous said...

wajinga ndio waliwao.....!!
Kila mtu ananjia zake za kupata pesa 1 niwamegee wadau hii ya moto moto,juzi nilipata sms toka kwenye number fulani za tigo zina t'ziro,mtumaji alinitaja kwa jina othuman,nimepata no.toka kwa selemani abdallah,kwamba tunaweza kufanya kazi....
Akanielekeza nifike sinza mori saa 5 na nusu,siku inayofuata....kwa maelezo zaidi nikaelekezwa nipge no.hiyo,nami nikapiga kutaka kujua kazi gani na mengineyo wakanikatisha kwa kuniambia nifike hapo mori..
M2 mzima nikaenda kwamba kulikuwa na wa2 kibaoo na wt waliwapata kwa njia kama yngu..
Hapo tukapewa maelezo tu ambayo ni ndimu mwanzo mwisho na ili uweze kupata kazi ktk kampuni hiyo kujaza form tsh 50000 na huulizwi habari ya elimu,ahdi ni kupata vyeo ndani ya muda mfupi...
Walianza na kuja wakaka na wadada kuja kujinadi jinsi hiyo kampuni ilivyowasaidia mpaka kufikia mshahara wa mil.1 na laki 2 lakini huyo anayesema hvyo akisimama nami naonekana mimi namzidi ingawa sina kazi...
Hao ndio mataperi wapya na bado wanaendelea,muda wa kuondoka wanaomba no.za vijana wengine mnaowafahamu na mchezo unakuwa huo huo.

Anonymous said...

Achana na hayo mamambo Mustapha tuongelee issue zetu,hivi ni kweli ATN nao wanaking'amuzi chao...??

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search