Apr 30, 2011

ATN wahama Satellite...!!


Kadri siku zinavyozidi kwenda na mambo yanazidi kubadilik
a,ATN yaweza kuwa kama channel 10 kwa wanaokumbuka jinsi walivyohama na kurejea tena baada ya kupoteza watazamaji,ijapokuwa kuna utofauti wa malengo ya kuhama,ATN wametoka kwenye masafa ya c band ( dish kubwa ) na kuhamia kwenye KU ( dish ndogo ),hapa inaonyesha lengo kuu ni kuuza ving'amuzi kwa mtazamo wangu ila pengine wanaweza wakawa na maana zaidi ya hii ambayo nafikiria mimi.
ATN wametangaza,je TBC nao wapo njiani...?? maana kwanza TBC1 inasumbua sana kwenye futi 6 kwa sasa lakini kwenye ving'amuzi mambo yanaenda vizuri sana,hili linapaswa liangaliwe kwa umakini kabla ya kuchukua uamuzi huu maana mnaweza mkapoteza watazamaji wengi ambao hawana uwezo wa kununua ving'amuzi.
Ni hayo tu kwa leo nawatakia kila la kheri wana TING....!!
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

3 Unasemaje..??:

Anonymous said...

kaka mkuu mbona bado mimi naipata home kwenye dish kubwa?

Mustapha maDish said...

Itakuja kukata ndugu.....!!!
Nikwambialo lizingatie..!!

Anonymous said...

Ulichokisema ndicho kilichotokea sasa vipi kuhusu Local channels zitaendelea kuwepo ama nazo ndo zinapotea zote namaanisha kwenye Dish langu la local!