May 1, 2011

Nawatakia sikukuu njema wajenga nchi wenzangu !

Leo ni tarehere 1 mwezi wa 5,kila tarehe hii imekuwa tunasherehekea sikukuu ya wafanyakazi,lengo na madhumuni ni kuthamini uwepo wa wafanyakazi na kukutana pamoja kuonyesha na kuzunguza ambayo yanaweza yakatupa changamoto wafanyakazi wa kila idara,huu ni mtazamo wangu kwa upeo wangu mdogo nilionao juu ya siku hii ya leo,pengine wewe unajua zaidi ya hii...!!
Hivyo popote mlipo nawatakia sikukuu njema watanzania wenzangu na msio watanzania pia maana lengo ni kujenga nchi huku mkono ukienda kinywani na maisha yakiendelea.
Kwa mwaka huu imefanyika kitaifa Morogoro mgeni rasmi akiwa mkuu wa nchi,binafsi napenda kuchukua nafasi hii kuwahusia vijana wenzangu kufanya kazi kwa bidii huku tukikumbuka ya kuwa "CHEZA NA MSHAHARA NA SI KUCHEZA NA KAZI" maisha mazuri hayaji kiurahisi yatupasa kufanyakazi kwa bidii sana na mliopo shule msome kweli maana kadri siku zinavyozidi kwenda maisha yanazidi kuwa magumu.
Ni hayo tu kwa leo wajameni....!!!
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: