May 7, 2011

WENYE KUMBI ZA KUONYESHA MPIRA KUPITIA DSTV IMEKULA KWAO...!!!


 Ni kilio cha watanzania wengi pande mbili kwa wakati mmoja,namaanisha kwa wale wapenzi wa mpira ligi za nje na wale wamiliki kumbi hizo...!!
MULTICHOICE TANZANIA ( DSTV ) kwa sasa ipo katika operations ya kuwafungia wale wote ambao walinunua DSTV kwa matumizi binafsi matokeo yake wakaenda kufanyia biashara kwa kutoza watu kiingilio na kufanya idadi ya wamiliki kumbi za kuonyesha mpira kuongezeka kila kukicha,huku idadi ya wateja wa kawaida kupungua kutokana na wengi kuangalia kupitia kumbi za mpira hizo....!!
Wapo ambao lishawakumba hili na kama wewe bado yakupasa ujiandae kwani wapo njiani,labda itangua ngumu kwa wale wenzangu namie walio ndani ndani,huku mafundi wao wakiwalinda maana ndo watoa taarifa wa kwanza...!!
Je hii ni kweli itaongeza wateja maana hakutakuwa na kumbi za mpira na kuwalazimu wapenzi wa mpira kufunga DSTV majumbani mwao...!!
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Mh mbona wanatuumbua hawa

Mustapha maDish said...

Na kwa wale wateja wapya wote ambao wanataka kujiunga na DSTV itakulazimu ulipie vifaa 89000+access package kwa miezi mitatu ambayo ni 60000=149000,kisha unachagua na kulipia package uitakayo....!!