Call / WhatsApp +255673378129

Jun 20, 2011

TUSIUCHUKULIE POA UKIMWI..!!


 Kwa mtazamo wangu kutokana na research ndogo niliyoifanya inaonyesha kwa sasa swala la gonjwa la ukimwi si kama ilivyokuwa kama miaka ya nyuma na kadri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kuchukulia poa na kuona kama  mtu kuugua mafua na maisha kuendelea kama kawa..!!
Nimetumia neno kuchukulia poa kwasababu katika watu ambao nawakusudia zaidi ni vijana ijapokuwa wote nataka twende sawa ila kwa vijana ni too much..!!
Leo hii NGONO imekuwa ndio inawatumikisha sana watu,utakuta watu wapo bize sana kwa ajili ya kufanya NGONO.wanatafuta pesa,wanaongopa,wanatumia muda mwingi sana na kufanya kila linalowezekana ili tu mwisho wa siku wafanikishe kufanya NGONO.
Siku hizi idadi ya walio wengi wanapenda sana ngono na upendo wa dhati unakuja baada ya kufanya ngono na hii inasababisha idadi ya wanaooa/kuolewa hupungua kila kukicha maana inakuwa ngumu kudumu kwa kutokupata kile ambacho either alikitegemea kabla ama alitaka tu kuona kiundani inakuwa aje..?
Mapenzi yanadumu miezi kadhaa tu then wanaachana ama mtu mmoja anakuwa na zaidi ya mpenzi mmoja na ndo pabaya sana hapa..
Unayemuamini ana wapenzi wawili nawe ukiwa wa tatu,hapo hapo nawe unakiacha unayemuamini unao wengine wa kuzugia pengine watatu,inaweza ikawa mpenzi wako unayemuamini hayuko poa kifedha hivyo kuna wa kukununulia vocha na matumizi mengine huku ukiwalipa kwa penzi lako lakini huna future nao,uliye na future nae ndiye huyo mwenye wapenzi wawili wewe ukiwa wa tatu na yaweza kuwa mmoja tu kati ya hao ndo unatumia kinga tena pia pengine siku za mwanzo mwanzo tu na mkishazoeana inakuwa mpango....!!
Hapa UKIMWI utatukosa ??
Kama ulikuwa hujui automatically kama utamsaliti mpenzi wako jua ya kuwa nawe atakusaliti ama anakusaliti...!!
Jamani,jamani UKIMWI upo tusijisahaulishe kama vipi tuwe na mmoja na yakishindikana hayo TUVAE..!!
Ni hayo tu kwa leo toka kwangu kuja kwenu.
Mustapha E. Hanya
Share:

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Ayaaaah Mustapha leo umeongea neno la maana sana ukiachilia hayo madish yako,safi sana uwe unakumbuka mambo ya kijamii kama hayo,hii inaonekana unatujali sana wateja zako.
Ukweli mtupu uliongea hapo SIDHANI KAMA TUTAPONA NI KUOMBA MUNGU TU ATUEPUSHE.

Anonymous said...

Tena siku hizi ukiwa huna kitu kila siku utalia na hata ukitulia mpenzi wako atakuletea hilo gonjwa.

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita