Call / WhatsApp +255673378129

Aug 31, 2011

Savvanah Bar & Restaurant

In Quality centre Dar es salaam....!!!
Mpaka sasa najivunia kuwa na watu ambao wanaheshimu uwepo wangu,wanathamini mchango wangu na mengineyo mazuri kama hayo,hii imepelekea leo kupewa shavu palee kwenye jengo jipya kabisa la Quality centre lililop pugu road,hapa ndani pana kitu kipya pia kinaitwa Nivvanah bar & restaurant...!!
Hapa tenda ilikuwa ya wenzangu ambao walikuwa wanafunzi wangu na wao ndo waliosababisha mimi kuhitajika hapo kwenda kutoa ambacho nilistahili kukitoa na mwisho wa yoote ikawa kama ambavyo utapata fursa kutembelea na kujionea..!!
Kuna channels za Local na DSTV zaidi ya yote kumepambwa na flat screen ni hayo tu kwa leooo...!!!
Share:

Aug 8, 2011

DSTV offer imeisha..!!

Ilikuwa kama utani na kuacha watu wakajiuliza hee DSTV kunani tena ama ndo wameishiwa,ama wameteteleka kwa sababu ya STAR TIMES...!!!??
Baada ya kutoa bonge la offer kwa 89000/= uliweza kupata full installations..!!
Watu wakajisahau na wengine wakiamini wataendelea kushuka ndipo wao watakapofunga ila mambo yakawa ndivyo sivyo,offer imeisha na wengine wakiitamani hata ile bei ya 89000/= ambayo muda wake umeshaisha..!!
Jamani labda kama itakuwa mmepoteza umakini ni kwamba Multichoice ni kampuni kubwa na ipo serious na kazi zaidi ya yote wanajua wakifanyacho na hata burudani zao za ukweli na ndio maana hata wateja zao ni watu makini na ambao wapo up to date..!!

Share:

Aug 4, 2011

CHANNELS ZA TANZANIA KWENYE DISH..!!




 Swali ambalo nakumbana nalo kila kukicha ya kuwa channel gani na ngapi za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish na kwanini nyengine hazipatikani? huku wengine wakidhani channels zote za Tanzania zinapatikana kwenye S.Dish..!!
Zaidi ya yote kuna ambao mpaka leo hii wanaamini ya kuwa ukifunga S.Dish Antenna hata zile channel ambazo zinatumia Antenna zitakuwa hazina chenga kwa sababu karibu na Antenna hiyo kuna Dish...!!
Channels za Tanzania ambazo zinapatikana kwenye Dish ni zile tu zinazotumia Satellite kurusha matangazo yao mfano:-ITV,CAPITAL,EATV,AGAPE,CHANNEL 10,STAR TV na TBC1.
Pia hakuna ufundi wa kufanya nyengine zionekane kwenye Dish mpaka wahusika watakapoamua kujiunga na Satellite.
Uzuri wa kutumia Dish ni kwamba hata nje ya nchi channel husika inaonekana kwa kutumia dish lakini kama utatumia Transmetter kurusha matangazo itakuwa ni Tanzania tu tena wala si nchi nzima sehemu chache tu za nchi..!!
Hivyo kuna ulazima wa channel zote za Tanzania kujiunga na Satellite kurusha matangazo yao,hii ni kwa faida yao katika kujitangaza zaidi maana itakuwa inaonwa na watu wengi zaidi..!!
C2C,DTV,CTN,TV TUMAINI,CLOUDS.
Hizi hazipo kwenye Satellite hivyo hazipatikani kwenye Dish.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita