May 5, 2012

Nipo hapa kuwataarifu habari ya msiba wa baba yetu mpendwa MR ESMAILY OMARY HANYA wa magomeni mapipa mtaa Idrisa no.27.
Napenda kunukuu maneno ya mwenyewe MUSTAPHA ESMAILY O.HANYA kwa wadau wake wa blog hii "Muda mwingi sikuwa hewani kwasababu nilikuwa namuuguza baba yangu ambaye kwa bahati mbaya jana ametutoka na mazishi yanakuwa leo saa kumi jioni magomeni mapipa mtaa uweje no.47."
Kwa niaba ya Mustapha Esmaily Hanya.
Naitwa N.Salmin
12:26 AM   Posted by Mustapha Hanya with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Michael said...

Pole sana mkuu,nilipiga simu nikapewa taarifa ya dada aliyepokea simu ya ofisi kuwa ulikuwa unamuuguza mzee wako. Umefanya sehemu yako kama binadamu na tena kwa mapenzi mema ya kutaka baba yako apone,LAKINI MUNGU ALIPENDA AMCHUKUE KWA WAKATI HUU. Tunaamini kuwa kila kifo kinapomfika mwanadamu ni wakati wake ambao Mwenyezi Mungu alimpangia toka siku alipoina dunia.,hivyo na kwa kuwa ni Mapenzi yake,hakuna mwanadamu awezaye kuyazuia. Iliyobaki ni kumshukuru Mungu kwa kumpa nafasi ya kuwepo duniani kwa muda alompangia,na tumshukuru kwa kila jambo. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. A'min. Michael-YOMBO ABIOLA.

Mustapha Hanya said...

Kaka ahsante sana na nilipata taarifa zako ila ndo hivyo nikawa bize na mzee!!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search