May 19, 2012

NITANUNUA VING'AMUZI VINGAPI!!??

Tarehe 31.12.2012 saa 23:59 itakuwa mwisho wa Local channel kupitia c band na Antenna pia na ili upate Local itakulazimu ununue king'amuzi ama ving'amuzi kutokana na channel za Tanzania utakazo!!
Mawazo yangu binafsi kulikuwa na mapungufu mengi sana kwenye mchakato huu na mwisho wa siku inaonyesha dhahili wakuu walikurupuka hawakufikiri kwa kina kabla ya kuweka mwisho mwaka huu!!
Tuangalie hali za watanzania wengi wao ni duni then tuangalie bei za ving'amuzi na channels zinazopatikana kwa kila king'amuzi,kuna kampuni moja tu ambayo binafsi naipa pongezi za kutosha EASY TV unapata Local channels karibu zote na bei yao ni 9000 tu kwa mwezi lakini zooote tupa kule!!
Nawaangalia wale wa vijijini ina maana hawastahili tunachokipata!!?? maana ilikuwa mtu anajipinda anafunga Dish ya Local anasahau,haina malipo ya mwezi wala nini zaidi ni kurekebisha tu litakaposumbua!!
Au ndo wazo la mtu mmoja tu alienda nje ya nchi akaona watu wapo UP TO DATE then akaja Tanzania kuwashawishi viongozi wakalipitisha,je mnajua hao ambao wanakwenda na wakati walianzia wapi!!??
Wananchi wengi watakosa haki yao ya msingi ya kupata habari kwa kukosa pesa ya kulipia ili aone/asikie hiyo taarifa ya habari.
IJAPOKUWA HATA NKISEMA WALIOLIPITISHA LIMEPITA,HAKUNA JINSI ILA UJUMBE SI MBAYA UKAWAFIKIA NA MKAONA MLIVYOVURUNDA HAPA!!
Ina meengi sana ila wacha niishie hapa nisije nikanyimwa hata hizo tenda maofisini mwao maana ndo hao hao wateja zangu!
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

1 Unasemaje..??:

Anonymous said...

easy wapi napata kiongozi!!