Call / WhatsApp +255673378129

Sep 26, 2012

DSTV IMENIFANYA NIIJUE IKWIRIRI!!

DSTV bado inafanya vizuri na ukizingatia haina mipaka ndani ya Tanzania na ndo sababu ya kukufanya popote ulipo unaweza kufunga na ukaona kila ambacho unapaswa kuona kutokana na Package uliyoilipia!!
Kwa mantiki hiyo ikafanya watu watoke sehemu moja inaitwa IKWIRIRI na kutaka nikawafungie DSTV ili wacheck mipira na mengine ya kupendeza ila kubwa likiwa mipira,nami si nipo kwa ajili ya kufurahisha wengine huku mkono ukienda kinywani nikasababisha kama ambavyo unaona mwanaume hasifiwi sura!!





Hapa kazi tu!!
 Safari ilikuwa ni ya siku moja tu,nimetoka Dar mchana nikafika kule jioni nikapumzika kisha siku inayofuata asubuhi nikafanya kilichonipeleka nilipomaliza nikatembea tembea kidogo kuona IKWIRIRI ilivyo maana ndo mara ya kwanza kufika ila ambacho naweza kusema pazuri banaa nimepapenda kiasi kwamba hata kuweka kambi naweza kwasababu ni mjini na mji ndo unakua!!
Nnachofurahi kwangu safari moja huanzisha nyengine na ndo kilichotokea Mungu akipenda ntakuwepo tena next week,umuhimu wangu umeonekana hivyo nnahitajika kurudi!!
Share:

Sep 19, 2012

MBIO ZA ABUDHAB!!


ABUDHAB INSTALLATIONS!!
Napata maswali yenu mengi sana  kwamba mnataka kujua mnawezaje kupata Decoder za Abudhab!?,kiukweli kwa Tanzania sijui sehemu maalum ya wakala wa hawa jamaa na kama wapo tunaweza kufanya mawasiliano ili kwa wanaotaka niwaelekeze kwao kwasababu mimi ambacho nafanya ni Installations pamoja na vifaa vyengine kasoro Decoder tu.
Ugumu wa kupata Decoder ni jinsi ya kuagiza kutokana na ukweli kwamba hawa jamaa wapo Arabuni,hivyo hakuna jinsi zaidi ya kuagiza kwa kumtumia mtu ama kuagiza mwenyewe!
Unaweza ukanunua then ambacho mimi nitakusaidia ni kuhusu vifaa vyengine kama dish,cable na Installations ila kwa kuongezea tu unaponunua ni vizuri ukanunua card mbili,namaanisha na ya Aljazeera!!














Hapa nikiwa katika kufanikisha watu waone channels zilizomo baada ya kununua Decoder waliponunua then wakanitafuta nikawapelekea Dish na vifaa vyote vilivyohitajika na kuwafungia kisha nikachapa mwendo maana wengine pia walikuwa wananihitaji!!!
Share:

Sep 1, 2012

UZURI WA FLAT SCREEN KWA UKUTA!!

Kwanza inapendeza asikwambie mtu,ipo salama pia na haichukui nafasi kubwa,zaidi ya yote unakuwa wa kisasa zaidi na ambaye unakwenda na wakati,kama bado upo nyuma huyu ameshakuacha!!
Si kama nauza TV flat laa ila ambacho nafanya ni kufunga tu kama hivi,hii ni office ila nilianzia nyumbani kwa moja ya wafanyakazi wa hii Office baada ya kufanya vizuri ndipo nikatakiwa nifanye Installations ya Office nami ndo nikafanya haya ya kupendeza!!

Hapa ni kudrill mwanzo mwisho!

Ili niweze kufunga kishika TV!!

..........

 Nikiweka TV baada ya kfunga tv bracket!!!

 Inapendezaje!!

 Hapa nje nikiset Dish ya DSTV!

 Lazima umalize hivi kuweka muonekano mzuri na kazi saafi!!!!
Hapa nimefanya Installations ya DSTV na Local Channels.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita