Jul 14, 2013

CHANNEL ZA TANZANIA ZINAKAZIA SWAUMU!

 Hapa nawatafuta Watanzania
Yap ni siku nyengine tena tunaamshwa vema na muumba nikiwa na afya njema na nafanya yangu kama kawa!
Nimeamkia sehemu moja wanapaita sinza,hapa nilitakiwa kufanya channel za Local zionekane vema na ndo nilichofanya ingawaje kwa channel za Tanzania TBC1 na STAR TV zinasumbua kwenye futi sita,angalau STAR TV wakati mwengine inatulia,ila hii kwenye futi nane haipo,kama utatumia dish futi nane channel zote za Tanzania zitaonyesha vema

 Hapa naingiza frequency
Nikafanya ya kufanya kama ilivyo ada yangu na mwisho wa siku nikaacha watanzania wanatawala kama kawa ingawaje TBC iligoma kabisa ila STARTV ilikuwepo imejaa tele!
Pia kwenye futi 6 kuna CITIZEN pia.

Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kazi nzuri kijana!

Anonymous said...

Swaumu ipande kweli kaka!
ila hapo swala zinakupita ama unazikumbuka!
Nancy Salmin

Anonymous said...

Kaka kuna kifaa wameniibia kwenye dish kwa juu. Walichomoa waya wakafungua wakaondoka nacho. Sijui kitaalamu kinaitwaje kiko kama tochi kinelekea dish. Nitakipataje?

Mustapha MaDish said...

Unamaanisha LNB!!??
Vinapatikana!!