Sep 3, 2013

+255789476655/659161111/714973797
Ukija kwenye swala la kuhama toka nyumba moja mpaka nyengineni ni jambo la kawaida sana kuhama na Dish yako iwe ya DSTV ama ya kawaida yeyote ile unahama nayo na channel zako zile zile ama zinaweza kuzidi kama ulikuwa hujui!!!!
Ambacho wengi hawajui na kuona ni kitu cha kawaida tu kuifungua Dish iliyokwishafungwa then unatafuta fundi wakati wa kutaka kufunga ulihamia je unajua madhara ya kuifungua mwenyewe ikiwa haupo makini!!??
Kwanza unaweza ukaiharibu LNB!
Unaweza ukalipinda Dish na kumpa shida fundi wakati wa kufunga!
Hii inatokea kwenye ufunguaji na ubebaji pia toka ulipohama mpaka ulipohamia!
Lakini kama utaifungua kwa umakini inawezaekana kila kitu kikafika salama.
Hii ni DSTV ilikuwa naitoa Mbezi Africana na kwenda kuifunga Mbezi salasala kama ambavyo mwenyeji wangu alivyonituma!

 Hapa nafanya setting zangu

Hapa tayari signal za kumwaga  ila haijalipiwa
2:52 AM   Posted by Mustapha Hanya with 9 comments

9 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kaka mkuu eti ni kweli kwenye Dish ndogo unaweza pata Local channels na zinakuwa ngapi?

Mustapha MaDish said...

Ndio inawezekana,unapata Local 5 na nyengne za nje!

Anonymous said...

Channel gn za Tanzania unazopata??

Anonymous said...

Ntajuaje kama receiver n MPEG 4 ama 2?
Medio com 930 ni 4 ama 2?
Na je kwa Receiver yng hiyo napata hzo Local kwa Dish ndogo?

Mustapha MaDish said...

Unapata ITV.EATV,CHANNEL 10,STAR TV na ATN!

Kwa medio com 930 huwezi kupata Local kupitia Dish ndogo,Ili uweze kujua kama ni ya 4/2 kwenye Receiver kuna kitabu kinachoelezea sifa za Receiver husika n pia nje ya box huandikwa pia kama ni 2/4!

Anonymous said...

Naweza nikafungua mwenyewe nikahama nalo then nikakuitwa uje unisetie!

Mustapha MaDish said...

Unaweza ukafungua ikiwa unauzoefu na hivi vitu maana katika Dish 10 zinazofunguliwa na wateja 3 mpka 4 ndio huwa salama lakini zilizobaki lazima kuna kitu kinamcost mteja wakati wa fundi kuja kufunga!

Lucas Michael said...

nimependa local kwenye dish dogo, inatumia satelite gani mkubwa?
vip STAR na TBC , mbona zinasumbua C BAND? njia gani inatumika kuzipata?
pia, kipi kinaongeza chanel nyingi, receiver mpge4 au dish futi 8?

Lucas Michael said...

Local chanel kwenye dish dogo ziko satelite gani?
vp TBC na STAR TV , zinapatikana vip kwenye C BAND?
NAOMBA USHAURI, kutumia receiver mpge4 au dish futi nane, kip kinaongeza chanel zaidi?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search