Sep 13, 2013

KAZI NZURI KWA MACHO YAONEKANA!

Awali hapa fundi alipita na kutumia uwezo wake kufanya alichofanya na kuondoka,lakini haikupita muda kwa mujibu wa mwenyewe Dish ikazingua na fundi akipigiwa kimyaaaa!!
Wapi alipo MustaphaMadish baada ya kunipata solution ikapatikana!!
Kwanza labda nitoe angalizo kwa wateja na mafundi wote kama mimi Dish iliikae muda mwingi bila kusumbua ni lazima ikae sehemu ambayo unaweza kudril,vinginevyo itakuwa kila siku fundi hachezi mbali nawe!!
Hapa nilikuta Dish imewekewa mawe hivyo ikawa kila muda inacheza na kwa kuongezea mawe huchangia Dish kupata kutu maana mvua inaponyesha mawe hunyonya majina mpaka kukauka inachukua muda!

 Toboa toboa inaanza!

 Baada ya toboa!

 Somo linaeleweka!

Toboa inaendelea!

Wakujiita Kenya akikaza kaza!


+255789476655

Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

9 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kwangu pia fundi kaniwekea Mawe najipanga ili nikuite mkubwa

Anonymous said...

Nahitaji huduma zako ntakutafuta mwisho wa mwaka ndo namalizia ujenzi wa lodge yangu ipo Kibaha.

Anonymous said...

Upo vizuri kaka!
Ila simu ilikuwa inaita tu,nilikuwa nahitaji huduma zako!

Anonymous said...

Huku shinyanga unaweza kuja nna kahotel changu nipo katika hatua za mwisho fundi!

Anonymous said...

Eti zile Dish za nyavu huwa haziuzwi na stend zake,naomba nisaidie ufafanuzi kaka isije ikawa nimeliwa!

Mustapha MaDish said...

Inapotokea umenipigia na simu inaita tu unaweza kunitext then nnapomaliza kazi nakutafuta maana huwa napigiwa na watu wengi!

Mustapha MaDish said...

Popote ndani ya Tanzania nafanya kazi hivyo wewe tu!

Mustapha MaDish said...

Kazi nzuri kwa macho yaonekana hivyo ntafute nikufanyie kizuri!

Anonymous said...

vp fundi! je abdhabi sport yaweze lipatikana kwa mpeg2,na dish la fut ngapi?