Nov 1, 2013

Mustapha MaDish
Si kwamba najua kila kitu ila najua vitu vingi ukanda huu na nashukuru Mungu kupitia hii blog yangu nimeweza kupata kazi nyingi na kujuana na mafundi wenzangu wengi tu Tanzania na nje ya Tanzania na ushirikiano mzuri uliopo ndo uliopelekea mi kuwepo hapa hii leo.
Ni ukweli ulio wazi hii ndo blog ya kwanza Tanzania kama sio East Africa kwa ujumla kuanzishwa inayohusiana na mambo haya hususani kwa lugha yetu ya kiswahili!
Sina muda mrefu sana toka nianze kazi hii ila nina experience ya kutosha sana maana mwezi wa 12/2013 nafikisha mwaka wa saba (7) nikiwa fundi Madish na vyote vinavyohusiana!
Katika kazi za zamani nakumbuka enzi ya GTV na mteja mmoja kati ya wengi ninayemkumbuka kumfungia ni Mh.John Cheyo nyumbani kwake Masaki jijini Dar!
Kazi hii nimesababisha vijana wenzangu wapatao 9 nao waishi kupitia kazi hii yaani nimewafundisha na sasa mafundi wa kutegemewa na wengine wamepata ajira DSTV!

 Matiko

 Kenya
Baadhi ya ninaojivunia na watakuja kuwa moto zaidi ya Mustapha MaDish!
Ijapokuwa wapo ambao mpaka leo nikiwaambia kuwa mimi sijui kila kitu hawaamini ingawaje toka nianze kazi sijawahi kushindwa na kazi isipokuwa napata changamoto tu!
Blog imenifanya niwafikie watu wengi duniani kwa muda mchache na ntaendelea kushukuru kwa ushirikiano wenu wadau!
Ambacho kinanisikitisha kuna watu hawapo serious kabisa na juhudi za mtu,hivyo kwa kutumia no.zangu nilizotoa hapo mtu anakazana kukubeep,wakati mwengine unampigia cha maana hana anachoongea ama anakuuliza kuhusu mambo ya madish,ni sawa sababu ni kazi yangu ila ntawapigia wangapi wasioeleweka!!? pia wakati mwengine mtu unamsaidia pengine frequency hakuamini anaomba no.ya fundi mwengine matokeo yake yule fundi mwengine anarejea tena kwangu na kutaka msaada!
Mimi sifanyi kazi ya kubahatisha kwamaana najua ambacho nafanya na kama ntakwambia kitu fulani hakiwezekani jua hakiwezekani sababu simjibu mtu ambacho sikijui na mpakanakujibu nimeshafanya utafiti!
Ushirikiano ninaoutoa kwa mafundi wenzangu na wadau kiushauri ama frequency sihitaji malipo na sijawahi kumtoza mtu pesa ingawaje mara nyingi watu wanataka kufanya hivyo ukisema tu Ahsante kwangu ni malipo tosha!
Malipo unayopaswa kunilipa ni kunitoa nilipo na kuja kukufanyia kazi na si vinginevyo,mwisho wa yote kutoa frequency ama ushauri wowote kwa mafundi ama wadau wengine si lazima maana kuna watu wengine huwa wananikwaza sana kanakwamba nipo kwa ajili yake yeye tu yaani hata kama nna kazi niache ili nimtajie yeye frequency fulani inakuwa haupo sahihi ndugu zangu tuwe wastaarabu!
Nawashukuru sana!
Toka kwangu .
 Mustapha Hanya.
11:37 PM   Posted by Mustapha Hanya with 16 comments

16 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hongera Sana Kaka Mustapha,kwanza kwakweli sikuwa najua hayo machache uliyosema kumbe huu mwaka wa 6 katka fani toka enzi ya Gtv kaka wewe mkongwe.Mimi ni uthibitisho katika swala la ushirikiano,vingi umenisaidia na lau ningekuwa Dar nami ningekuwa miongoni mwa wanafunzi wako.Hongera sana na usichoke tupo pamoja mtaalam.
Ibraham,Sumbawanga.

Anonymous said...

Anayehitaji msaada wako utamuona tu kamwe hawezi kubeep,lakini majitu mengne mapunguani hata namba ya polisi wanabeep unashangaa wewe kaka.

Anonymous said...

Hongera sana kaka Mustapha,narudia tena Hongera sana.
Kabla nilikuwa sijui una uzoefu kiasi gani kumbe toka enzi ya Gtv,huu mwaka wa 7 kaka upo vizuri sana naweza kusema mimi mmojawapo kati ya wale wasioamini kama kuna usichokijua kuhusu hii fani.
Umenisaidia sana na nimenufaika kwa kusema ule ukweli,pia kama ningekuwa huko Dar nami ningekuwa miongoni mwa wanafunzi wako!
Endelea kutufumbua tupo nyuma yako mtaalamu wetu.
Ibraham,Sumbawanga.

Anonymous said...

upo vizuri sana kaka big up!

Anonymous said...

Hongera sana bwana Mustapha Hanya kitaaluma Mustapha Madish,leo umenifumbua vitu kuhusu wewe ambavyo nilikuwa sivijui kumbe unastahili heshima wewe ni mkongwe kwenye fani.
Nashukuru kwa kutuletea hii blog ambapo inatufaisha sana kuliko ambavyo kaka wewe unadhani,nimepata kujua vitu vingi kupitia hii blog na mara nyingi huwa nakupigia nawe huna choyo kwa moyo huo Mungu akuzidishie kaka usibadilike.
Matumaini yangu kama na mimi ningekuwa huko Dar ningekuwa miongoni mwa wanafunzi wako na naamini ningekuwa hatari huku Sumbawanga.
Siku nikija Dar ntakutafuta nawe ukipata tour ya huku naomba niwe mwenyeji wako kaka.
Ibraham,Sumbawanga.

Anonymous said...

Hongera sana bwana Mustapha Hanya kitaaluma Mustapha Madish,leo umenifumbua vitu kuhusu wewe ambavyo nilikuwa sivijui kumbe unastahili heshima wewe ni mkongwe kwenye fani.Nashukuru kwa kutuletea hii blog ambapo inatufaisha sana kuliko ambavyo kaka wewe unadhani,nimepata kujua vitu vingi kupitia hii blog na mara nyingi huwa nakupigia nawe huna choyo kwa moyo huo Mungu akuzidishie kaka usibadilike.Matumaini yangu kama na mimi ningekuwa huko Dar ningekuwa miongoni mwa wanafunzi wako na naamini ningekuwa hatari huku Sumbawanga.Siku nikija Dar ntakutafuta nawe ukipata tour ya huku naomba niwe mwenyeji wako kaka.Ibraham,Sumbawanga.

Anonymous said...

kazi nzuri sana kaka big up!

Anonymous said...

Thatz Gud!
Hii iwafikie wale wasiojua nini maana ya mtandao,nini maana ya blog..
Blog inakuingizia nini?? Ina faida gani kwako na kwa jamii kwa ujumla!
Kaka wewe ni kati ya vijana wachache wa kitanzania ambao wanajitambua na jua ya kuwa kuna kijiji kinakuunga mkono hvyo usijione kama upo peke yako!
Umeona fulsa na unaitumia ipasavyo,amini ambacho nakwambia utafika mbali sana kwa mwendo huu.Hongera sana!
Changamoto ndo chachu ya mafanikio yako kaka!

Anonymous said...

Mi nakupongeza na nashukuru kwa elimu na msaada wako unaoutoa kwetu!
ila swali langu nawezaje kupata Local kupia dish ndogo!?

Anonymous said...

Pongezi sana!
Unajua umuhimu wa mtandao na jinsi ya kuutumia ni vijana wachache sana wanaojua kuingiza kupitia mtandao,changamoto hazikosi kwa kila jambo lenye mafanikio na binadamu tunatofautiana ni kupambana kama unavyopambana na Mungu atakufikisha utakapo Inshallah.

Anonymous said...

Nahitaji kujua mengi toka kwako mkuu,msaada ntakucheck kwa cm ila tu ucnichoke.

Anonymous said...

Nami nahitaji hii elimu nafuata utaratibu gani maana nimekutumia email nimekupgia simu bila matumaini upo bize sana kaka naomba msaada wako nami nahitaji mautundu hayo!

Anonymous said...

HAKIKA NIMEPENDA SERVICE YAKO NA NTAKUPA JAMAA ZANGU WENGI TU KWAMAANA SIJATEGEMEA INGAWAJE NILIPATA SIFA ZAKO@mAMA BAHARI!

Anonymous said...

Nami nataka kujifunza kaka huo utaalamu wako nahitaji sana nimekuinbox ila bila mafanikio kaka naomba msaada wako mkuu!

Anonymous said...

hONGRA KAKA MKUU!
Tupo nyuma yako

Beston Mbaga said...

naomba ushauri channell za digitek na easy tv na zuku ziko ngapi na digtek hulipiwa?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search