Call / WhatsApp +255673378129

Sep 29, 2013

HATIMAE CLOUDS TV KWENYE DISH!!


Swali la wengi leo limepata jibu maana walikuwa wanauliza Clouds tv mbona haipo kwenye Dish,ukweli ni kwamba hili lilikuwa ni swala lililo ndani ya uwezo wa Clouds Media Group na sio mimi Mustapha Madish!!
wamefanya walichopaswa kufanya,ambapo kwangu imekuwa fulsa ndo hivi naitumia kuwaunganisha watu kuangalia clouds tv kupitia Dish,uzuri wake ni kwenye Dish ndogo pale pale zinapopatika zile za Local!!!
Hii inafanya idadi ya channel za Tanzania zinazopatikana kwenye Dish ndogo kuongezeka!!
Zaidi ya yote unapaswa utumie Receiver ya MPEG4 na si MPEG2!
Share:

Sep 13, 2013

KAZI NZURI KWA MACHO YAONEKANA!

Awali hapa fundi alipita na kutumia uwezo wake kufanya alichofanya na kuondoka,lakini haikupita muda kwa mujibu wa mwenyewe Dish ikazingua na fundi akipigiwa kimyaaaa!!
Wapi alipo MustaphaMadish baada ya kunipata solution ikapatikana!!
Kwanza labda nitoe angalizo kwa wateja na mafundi wote kama mimi Dish iliikae muda mwingi bila kusumbua ni lazima ikae sehemu ambayo unaweza kudril,vinginevyo itakuwa kila siku fundi hachezi mbali nawe!!
Hapa nilikuta Dish imewekewa mawe hivyo ikawa kila muda inacheza na kwa kuongezea mawe huchangia Dish kupata kutu maana mvua inaponyesha mawe hunyonya majina mpaka kukauka inachukua muda!

 Toboa toboa inaanza!

 Baada ya toboa!

 Somo linaeleweka!

Toboa inaendelea!

Wakujiita Kenya akikaza kaza!


+255789476655

Share:

Sep 3, 2013

TOKA AFRICANA KWENDA SALASALA

+255789476655/659161111/714973797
Ukija kwenye swala la kuhama toka nyumba moja mpaka nyengineni ni jambo la kawaida sana kuhama na Dish yako iwe ya DSTV ama ya kawaida yeyote ile unahama nayo na channel zako zile zile ama zinaweza kuzidi kama ulikuwa hujui!!!!
Ambacho wengi hawajui na kuona ni kitu cha kawaida tu kuifungua Dish iliyokwishafungwa then unatafuta fundi wakati wa kutaka kufunga ulihamia je unajua madhara ya kuifungua mwenyewe ikiwa haupo makini!!??
Kwanza unaweza ukaiharibu LNB!
Unaweza ukalipinda Dish na kumpa shida fundi wakati wa kufunga!
Hii inatokea kwenye ufunguaji na ubebaji pia toka ulipohama mpaka ulipohamia!
Lakini kama utaifungua kwa umakini inawezaekana kila kitu kikafika salama.
Hii ni DSTV ilikuwa naitoa Mbezi Africana na kwenda kuifunga Mbezi salasala kama ambavyo mwenyeji wangu alivyonituma!

 Hapa nafanya setting zangu

Hapa tayari signal za kumwaga  ila haijalipiwa
Share:

Sep 1, 2013

CHANNEL ZA TANZANIA KWENYE DISH NDOGO


Awali ilikuwa huwezi kupata Local channel mpaka ufunge dish ya c band yaani dish kubwa,lakini sasa mambo ni tofauti kwani unaweza kupata Local channel kwa kutumia kadish kadogo (KU) na lnb ya ku,isipokuwa Receiver ni lazima utumie ya MPEG4 tofauti na upatikanaji wa kwenye c band ambapo hata kwa MPEG2 unapata Local channel!
Channel za Tanzania zainazopatikana kwenye Dish ndogo:-
  1. TBC
  2. CAPITAL
  3. EATV
  4. ITV
  5. CHANNEL 10
  6. ATN
  7. STAR TV 
na nyenginezo za nje ikiwemo Emanuel tv kwa wale wapenzi wa Gospel!
+255789476655/714973797
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita