Call / WhatsApp +255673378129

Nov 30, 2013

AZAMTV | BURUANI KWA WOTE | AZAM TV


 BURUDANI KWA WOTE!!!
Azam Tv ni mtoa huduma ya kidigital kupitia Satellite,ina burudani yenye ubora wa hali ya juu kwa familia na kwa bei nafuu,makao makuu ya Azam tv yapo Dar es salaam Tanzania.Azam tv ilianzishwa mwaka 2013,ina nia ya kujipanua zaidi katika nchi nyengine za Africa siku za usoni.
Azam tv inamiliki vipindi channel zipatazo tatu,nazo ni:-
  1. Azam One
  2. Azam Two
  3. Sinema Zetu


HUDUMA ZA AZAM TV
Share:

Nov 29, 2013

TATIZO LAKO NI NINI ILI UPATE CHANNEL UTAKAZO!!??

Kwa Office nikikungoja wewe!
Kuhusu visimbuzi vyote kama:-
DStv, Azam tv, Startimes na Zuku.
Pengine toka ilipotulazimu tuingia kwenye Digital,ndugu yangu wewe bado hukuwa tayari,ama hujui ni King'amuzi gani bora cha kununua na ukapata kile ulichokuwa unakihitaji!
Una Dish linasumbua hujui mafundi wa uhakika utapata wapi!?
Unahitaji kununua Dish na hujui lipi ambalo utapata kile upendacho!
Umejenga ama unajenga Hotel,Lodge,Guest House na hujui wapi uatapata mtaalamu wa kuwezesha kufanya tv zako zote zilizomo kuonyesha channel uzitakazo na zinazopendwa na wengi bila chenga!?
Office yako nadhifu,unataka kufunga flat screen ili uone channel pendwa huji mtaalamu pa kumpata!?
Hujui wapi utapata vifaa vyote vinavyohusiana na Madish!?
Majibu ya Maswali yote hayo ni moja tu!
Mimi Mustapha MaDish Technician!
Si kwa maneno bali kwa taaluma yangu nauzoefu nilionao!
Nimeshafunga Ikulu ofisi ya waziri mkuu
Paradise ambayo sasa JB Belmont
CRDB Bank Azikiwe,Mikocheni,Mlimani city.
Geraffe View Hotel
Bahari Lodge
Dotto-Diwani wa kigamboni
Masaburi-Meya ya D'salaam
Mengi-M'Mtendaji IPP Media
Richmond tower
Flat za BOT
na sehemu nyengine nyingi zisizo na idadi!
Tunauza na kufunga Dish Antenna Aina zote.
Kwa Office,Hotel,Apartment n Majumbani.
Call +255784378129
WhatsApp +255658046655
mustaphamadish@gmail.com
Karibu!
Share:

KUHUSU AZAM TV

Azam tv ni kampuni mpya katika ukanda huu wa Digital,tunaanza rasmi kuuza tarehe 6/12/2013.
Inajumuisha Dish ndogo,lnb,Cable mt20,Decoder na air time mwezi mmoja!
Kumefanyika mabadiliko kidogo ya bei awali ilikuwa 85000/= full installations,kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo imelazimika kubadilisha bei ambapo sasa inauzwa 135000/= ikiwa vifaa na ufundi.
Na unalipia malipo ya mwezi hakuna mabadiliko ni ile ile 12500/= kwa mwezi.

Decoder ya Azamtv

Dish ya Azam tv.
Kwa Mawasiliano zaidi tupo:
 Morogoro rd,Magomeni Mapipa
Office:+255789476655
Personal:+255659161111/714973797
Email:mustaphamadish@gmail.com.
TUNAUZA | TUNAFUNGA | DISH AINA ZOTE.
Share:

Nov 19, 2013

UPO TAYARI KUIPOKEA AZAM TV!!??

Maswali yakiwa ni meeengi kuhusu lini king'amuzi cha Azam tv kitaanza kuuzwa ili wadau waweze kufurahia huduma hii alau jibu limeweza kupatikana ambapo itapelekea wewe kujiapanga kukipokea na kupata kile ulichokuwa unakitarajia!!

Setting zikiendelea!
Taarifa za awali ilikuwa mapema mwezi  huu ilikuwa kwenye majaribio na mwishoni mwa mwezi huu vitaanza kuuzwa na ndivyo itakavyokuwa,mwisho wa mwezi huu mzigo unaanza kuuzwa so kama upo Magomeni ama karibu na Magomeni unaweza kunicheck tu na ukapata Azam tv kama kawa!!
Bei ni 95000/= unapata Dish,Decoder,Cable,LNB na Kufungiwa!
Malipo ya mwezi ni Tsh.12500/=
Share:

Nov 2, 2013

HOTEL INSTALLATIONS

Kwanza ujue unachohitaji!
Channel gani na ngapi,je za kulipia ama za bure,vinginevyo iwe mchanganyiko za bure na kulipia!
Vyote ukishindwa utapata nafasi ya kupatiwa ushauri kwa zile channel pendwa na maelewano yatakapopita kazi ndipo inaanza kama furaha itawale kwako!
Ili uimara upatikane!
 Macho hayana pazia!
Matunda yangu akiwajibika!


 Hotel inapendeza na Flat Screen!
 ...........!!
Receivers

 Vimehusika!

 Vihusishi!

 Hotel tayari kwa kupokea wateja!
Installations hii inaweza kufanyika katika Lodge,Hotel na Guest House!
Kila tv inajitegemea katika kubadili channel bila kumbugudhi mwengine!
+255789476655/659161111

Share:

Nov 1, 2013

KUTOKA KWA MUSTAPHA MADISH

Mustapha MaDish
Si kwamba najua kila kitu ila najua vitu vingi ukanda huu na nashukuru Mungu kupitia hii blog yangu nimeweza kupata kazi nyingi na kujuana na mafundi wenzangu wengi tu Tanzania na nje ya Tanzania na ushirikiano mzuri uliopo ndo uliopelekea mi kuwepo hapa hii leo.
Ni ukweli ulio wazi hii ndo blog ya kwanza Tanzania kama sio East Africa kwa ujumla kuanzishwa inayohusiana na mambo haya hususani kwa lugha yetu ya kiswahili!
Sina muda mrefu sana toka nianze kazi hii ila nina experience ya kutosha sana maana mwezi wa 12/2013 nafikisha mwaka wa saba (7) nikiwa fundi Madish na vyote vinavyohusiana!
Katika kazi za zamani nakumbuka enzi ya GTV na mteja mmoja kati ya wengi ninayemkumbuka kumfungia ni Mh.John Cheyo nyumbani kwake Masaki jijini Dar!
Kazi hii nimesababisha vijana wenzangu wapatao 9 nao waishi kupitia kazi hii yaani nimewafundisha na sasa mafundi wa kutegemewa na wengine wamepata ajira DSTV!

 Matiko

 Kenya
Baadhi ya ninaojivunia na watakuja kuwa moto zaidi ya Mustapha MaDish!
Ijapokuwa wapo ambao mpaka leo nikiwaambia kuwa mimi sijui kila kitu hawaamini ingawaje toka nianze kazi sijawahi kushindwa na kazi isipokuwa napata changamoto tu!
Blog imenifanya niwafikie watu wengi duniani kwa muda mchache na ntaendelea kushukuru kwa ushirikiano wenu wadau!
Ambacho kinanisikitisha kuna watu hawapo serious kabisa na juhudi za mtu,hivyo kwa kutumia no.zangu nilizotoa hapo mtu anakazana kukubeep,wakati mwengine unampigia cha maana hana anachoongea ama anakuuliza kuhusu mambo ya madish,ni sawa sababu ni kazi yangu ila ntawapigia wangapi wasioeleweka!!? pia wakati mwengine mtu unamsaidia pengine frequency hakuamini anaomba no.ya fundi mwengine matokeo yake yule fundi mwengine anarejea tena kwangu na kutaka msaada!
Mimi sifanyi kazi ya kubahatisha kwamaana najua ambacho nafanya na kama ntakwambia kitu fulani hakiwezekani jua hakiwezekani sababu simjibu mtu ambacho sikijui na mpakanakujibu nimeshafanya utafiti!
Ushirikiano ninaoutoa kwa mafundi wenzangu na wadau kiushauri ama frequency sihitaji malipo na sijawahi kumtoza mtu pesa ingawaje mara nyingi watu wanataka kufanya hivyo ukisema tu Ahsante kwangu ni malipo tosha!
Malipo unayopaswa kunilipa ni kunitoa nilipo na kuja kukufanyia kazi na si vinginevyo,mwisho wa yote kutoa frequency ama ushauri wowote kwa mafundi ama wadau wengine si lazima maana kuna watu wengine huwa wananikwaza sana kanakwamba nipo kwa ajili yake yeye tu yaani hata kama nna kazi niache ili nimtajie yeye frequency fulani inakuwa haupo sahihi ndugu zangu tuwe wastaarabu!
Nawashukuru sana!
Toka kwangu .
 Mustapha Hanya.
Share:

TING WAMEHAMA SATELLITE


Niliwahi kuwaambia baadhi ya watu ila ikawa kama hawanielewi hivi baada ya kukataa kuwafungia local channels kupitia Dish dogo baada kugundua kama hizo local uhai wake mdogo,kwa maana satellite waliyokuwa wamewekwa na Ting kwa lugha nyepesi ilikuwa ni mali ya Ting!!
Awali Ting walikuwa Eutelsat 36A degree 36.0E,ambapo walikuwa sawa na Dstv wale wadau watakuwa wanakumbuka kwakuwa ilikuwa unaweza ukatumia Dish moja kwa kupata Ting na Dstv!!
Sasa wamehamia Amos 5 degree 17.0E wala sio mbali saaana na ilipokuwa awali!
Kama wewe ni fundi haya!
Satellite: Amos 5 - 17 degrees East
Frequency: 12417Mhz
Symbol Rate: 30000Msps
Modulation: 8 PSK
FEC : 2/3
Pilots On
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita