Jan 8, 2014


Hivi karibuni nilipokea simu ilinisikitisha sana kuhusu bei wanazouziwa watu hasa mikoani king'amuzi cha Azam tv na cha kushangaza zaidi hata hapa Dar kuna baadhi ya wakala wanauza bei juu tofauti na utaratibu uliowekwa,nilichogundua ni kwamba wengi wameingia kwenye hii biashara pasi kuijua vizuri wanachofanya wao ni kuuza tu lakini ufundi ni juu ya mteja mwenyewe matokeo yake mteja ananunua king'amuzi lakini anafungiwa baada ya wiki 1/2 mpaka 3 kwa kukosa fundi!
Simu toka Ruvuma niliambiwa wanauziwa 180000/= bila malipo ya mwezi bila ya kufungiwa!
Mwanza wanauziwa 160000/= bila malipo ya mwezi na bila ya kufungiwa!

Dar kuna kuna mtu aliuziwa 160000 full installation na malipo ya mwezi mmoja!

Na kwengineko nadhani haya yanatokea sana tu na kilichonifanya leo niweke post hii ni hii bei ya Ruvuma!!!
Sababu ya kila mtu kujiamulia bei anayotaka yeye ni kutokana na wauzaji kutokuwa wakala,hivyo ili nae apate faidi ananunua kwa wakala then anauza nae kwakuwa ndo msimu wa kupata pesa hasa kupitia Azam tv kuikweli mnatuharibia wenye kazi zetu,binafsi napenda sana tuwe wengi ili mnipe changamoto niweze kuwa mbunifu zaidi katika kazi yangu lakini hamuwezi mkanipa changamoto kiubabaishaji na kuibia watu namna hiyo!!
BEI YA AZAM TV NI 135000/=

Unapata Vifaa vyote!! Hii bila ya ufundi wala kifurushi.
UKITAKA KUJUA BEI ZA VIFURUSHI VYA AZAM TV BOFYA HAPA
PIGA +255789476655


11:26 AM   Posted by Mustapha Hanya with No comments

0 Unasemaje..??:

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search