Jan 24, 2014

Lazima kucheka ili siku ziongezeke!!
Ila mengine kiukweli yanamaudhi kupitiliza,tukiacha kibinafsi pia kikazi maana kazi yangu inahusisha watu wa aina tofauti kwa kipato,jinsia na hata uwezo wa uelewa kama si kufikiri!
Nianze na issue ya wale wateja wangu wanaopiga simu usiku ama asubuhi sana,nimewahi kupokea simu usiku wa saa 5,6,8 na kukuta miss call ya saa 10 alfajiri na baada ya kupiga mtu anakuuliza kuhusu Madish!
Kweli jamani! hata kama ni biashara tunawezaje kufanya kwa muda huo!
Na hao wote ambao wanapiga muda huo hakuna aliyenipigia mchana baada ya kumuelekeza afanye hivyo labda awe ametumia no.yengine tofauti na ile ya usiku!
Ingawaje sikuwa nimeweka muda wa kazi itanilazimu kufanya hivyo ili alau kwa ndugu zangu wale usiku kwao mchana wapate elewa!

Mustapha Hanya a.k.a Baba Fetty
11:02 PM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment

1 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kaka watu tunatofautiana kama unavyosema hivyo tuvumilie!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search