Sep 9, 2014

Mwaka 2014 ndio huu unaelekea ukingoni ambapo mwakani mwaka 2015 inatupasa nchi nzima tuwe tumeshahamia Digital huku tukiwa tumeondokana kabisa na Analogue!
Ijapokuwa kuigia Digital kulikuwa na misemo mingi,wapo waliunga mkono ambapo idadi kubwa walilalama huku kila mtu akiwa na sababu yake ila wengi wao wakilalamikia uchumi!
Ingawaje malalamiko yalikuwa meengi ila udigital tumeingia na faida zake zinaanza kuonekana.
Kuna kampuni nyingi za ving'amuzi na kwa ujumla zote zinafanya vizuri haina ubishi kuwa kila kampuni ina wapenzi wake kutokana na huduma na channel husika|
Hii Blog ipo toka hapa Tanzania kuna kampuni tatu tu za ving'amuzi DSTV,GTV na EASY TV ijapokuwa mmiliki mwenyewe ambaye ni Mustapha E.Hanya a.k.a Mustapha MaDish yupo toka enzi ya DSTV tu.
Ukomavu wangu kwenye ukanda huu umenifanya niwe msaada mkubwa kwa watanzania na wasio watanzania kwa kuwahudumia kwa mkono wangu ama kwa ushauri tu.
Nipo sahihi sana nikisema kuwa hii ndio nyumba ya ving'amuzi kwakuwa leta kesi ya king'amuzi chochote ikishindikana kwenye mikono yangu ni hakika umefail jumla.
Binafsi najisikia faraja sana kuona mimi nakuwa msaada kwa wengine,kuona wengine wanaendesha maisha yao kupitia mimi,kuona watu wanatamani kuwa kama mimi..
Sina ambacho naweza sema zaidi ya Ahsante Allah kwa kila hatua nipigayo..
Nafikiria kufanya bora zaidi..zaidi ya hili ambalo naliendeleza kwa lengo lile lile kuendesha maisha huku kuwafunua upeo wengine hasa vijana wenzangu..
kama nilikuwa mwanga kuwa mtanzania wa kwanza kufungua Blogsite inayohusu hii taaluma na ikawa ya kwanza kwa Africa mashariki na kati ni hakika nimechonga barabara wacha wengine wapite kiulaini lakini watakuwa wananishukuru si tu kwa kunifuata hata wakiwa peke yao ndani ya nafsi zao watanishukuru kama si kunizungumzia..
Ili ufikie mafanikio lazima ukumbane na changamoto na ndicho kinachotokea..
Nipo kwa ajili ya kuwahudumia watanzania na wasio watanzania,waishio Tanzania na nje ya Tanzania pia..
Niulize leo chochote kuhusu king'amuzi chochote Tanzania..
DSTV
AZAM TV
ZUKU TV
DIGITEK
TING
STARTIMES
CONTINENTAL
EASY TV
Kwa swali lolote liwe la kiufundi ama huduma kwa ujumla!
Kutaka kuunganishwa pia!
Unaweza wasiliana nami:
Kama upo facebook utafanya busara kama utalike page ya mustaphamadish
+255789476655/714973797
mustaphamadish@gmail.com

 
12:51 PM   Posted by Mustapha Hanya with 3 comments

3 Unasemaje..??:

Anonymous said...

hakika hii ni nyumba ya ving'amuzi..
nimeweza kujifunza mengi na umekuwa msaada sana kwangu na kwa wengne naamini hivyo..
ubarikiwe sana kaka

Anonymous said...

Jua kwamba tulionyuma yako ni wengi sana kaka hapa ni kabisa nyumba ya ving'amuzi maana kama shule hii.

Anonymous said...

Hivi inakuwaje unaweza kufanya na kampuni zote hizo?
Unajibu sawia kabisa tofauti na baadhi ya makampuni husika kaka hongera

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search