Oct 13, 2014

...nilipoona Dish hii ya DStv wala sikushangaa sana na badala yake ndipo nikaamua kupiga picha ili alau kile ambacho nilichokuwa sijawahi hata kukumbusha tukumbushane kwa pande zote mbili..
Mafundi wenzangu na wateja wetu pia wote wa ving'amuzi kwa ujumla hasa vile vya kutumia Satellite Dish.
Nianze na mafundi wenzangu wataalam wa madish... 
Inawezekana ukawa na kazi nyingi na inakulazimu ukifika site -kwa mteja,huwa huitaji kutumia muda mwingi bila kuangalia kama kazi unayoifanya itakuwa nzuri ama laa,matokeo yake unalipua tu ili mteja aone tu kwa wakati huo nawe uchukue chako na kesho akuite tena...
Kitaaluma hii si sawa hata kidogo..
Yaani kama umemuibia mteja wako..
Madhara ya hii licha ya kuonekana fundi mbabaishaji pia hautaweza kupata wateja wengine kupitia wateja uliowafanyia uhuni huu!!

Hakuna tangazo zuri kama kupitia kwa mteja uliyemuhudumia vema,labda nikwambie kitu ijapokuwa hii blog inanipa wateja lakini si kama ufikiriavyo wateja wangu wengi wanatokana na wale niliowahudumia vizuri na hii ndio siri ya mafanikio yangu katika taaluma hii..

Ila nilichogundua wateja wengi hasa wanawake si wasichana si wamama wao shida yao kubwa ni kuona tv inaonyesha,ila swala umefunga wapi hilo utajua fundi.
Wateja wetu wapendwa..

8:58 AM   Posted by Mustapha Hanya with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

mafundi wanaojua umuhimu wa kazu zao mpo wachache sana lau ingekuwa nami nipo dar ningenufaika na service yako.

Anonymous said...

Naomba kuuliza hivi zuku,azam na startime zipo sehemu moja!?
maana yake naweza nikatumia dish 1 kupata zote hizo!?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search