Oct 11, 2014

STARTIMES YA DISH

King'amuzi ambacho kilipoanza kilipokelewa vizuri sana,watanzania wengi walinunua ila baadae kidogo kulitokea tatizo,tatizo ambalo liliwaweka wakati mgumu sana hasa katika kupata wateja wapya na wale wa zamani kutafuta namna ya kuondokana na tatizo hilo..
Tatizo la signal ambalo lilipelekea picha kukata kata ama kupotea kabisa ila ambalo lililokuwa linatokea hata kama mteja hajafunga vizuri Antena yake ama mafundi ambao wateja wanawatafuta ili wafungiwe Antanna zao kufunga ndivyo sivyo lakini atakachomalizia kusema tatizo ni la star times wenyewe..
Tatizo ambalo walikabiliana nalo na kulimaliza kabisa na kama inatokea kwa sasa zungumza na fundi wako ila kama ni fundi wewe mwenyewe maana watanzania tunaongoza kwa kuingilia kazi za watu..unapaswa Antanna yako kuielekeza Makongo juu,tatizo likiendelea hebu angalia cable yako ipo sawa? hakuna sehemu iliyochubuka kama sio kukatika? 
Likizidi hapo kuna namna unaweza nicheck nikakusaidia!
Binafsi huwa nasema Digital ni Dish ila inapotumika Antenna naona bado Analogue!
Pongezi kwenu Star times Tanzania kwa kuboresha huduma zenu kwa kuleta startimes ya dish,hili ni jambo zuri sana kwenu na kwa wateja wenu kwa ujumla!
Kwa tsh 105000/= umepata star times ya dish
Ambayo inakuwa na kifurushi cha mwezi mmoja ndani
Kwa maelezo zaidi na kuunganishwa +255789476655
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

4 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hii malipo yake ya mwezi kama ya Antenna!?

Anonymous said...

Upatkanaji wake upoje ni tanzania nzima!?
king'amuzi HD kama azam ama ndo sukuma twende!?

Anonymous said...

Star times huwa napenda tv 1 tu.

Anonymous said...

Hii ya dish hata usipolipia local nazo zinabaki?