Dec 30, 2014



Namshukuru sana Allah,ni yeye ndiye aliyefanya mpaka sasa nipo hapa,wengi walitamani waifikie siku hii lakini kwa mapenzi yake hatupo nao,mpaka kufika hapa nasema Alhamdulllah!
Nakushukuru wewe mdau wangu ambaye haipiti siku bila kutembelea haka kablog chetu na kila ambaye unatembelea maana bila ya wewe wala nisingeweza kupata ambacho nakipata,ushirikiano wetu umeleta na unaendelea kuleta meengi mafanikio kwangu katika kazi yangu hii!


Sikukuu ambayo naweza kusema yenye nyimbo nyingi na mapambo imepita,wengi tukiijua kama x mass lakini sababu kuu ya kuwepo sikukuu hii ni kukumbukia siku ya kuzaliwa kwa yesu kristo!
Mwaka 2014 ndo umeishia,mwaka ambao kila mtu ana yake ya kuzungumzia mwaka huu,yanaweza kuwa mazuri ama mabaya lakini mwisho wa siku mwaka ndo umeshakatika hivyo,kama hatujatimiza yale ya msingi tuliojipangia ni jukumu letu kuangalia tulifail wapi na kisha kujipanga ili alau mwaka 2015 uwe mwaka wa mafanikio..
Mwaka huu katika ukanda wetu ndo mwaka wa mwisho kutumia Analogue,nchi nzima mwendo utakuwa ni Digital tu,ijapokuwa kuna changamoto kubwa ktk swala la network sehemu kubwa ya nchi yetu bado ni tatizo,nikizungumzia swala la mitandao ya simu,maana udigital bila ya network ni mtihani mkubwa sana,tukiacha swala la network wapo watanzania ambao mpaka sasa hawana king'amuzi na kila mtu anasababu yake,wapo ambao hawana uwezo wa kununua kabisa,wapo ambao bado wanajichanga,wapo ambao hawajui wanunue king'amuzi gani!
Mwaka 2015 mwaka ambao nitatoa ving'amuzi visivyo na idadi kwa watanzania karibu nchi nzima,kwa wale wasiokuwa na uwezo na wakafanikiwa kunishawishi mimi kufanya hivyo!
La msingi ni wewe na umwambie umpendae kwa pamoja mfatane na mimi kila hatua ntakayokuwa napiga ili niweze kukufikia na kuweza kumaliza tatizo lako!
MUSTAPHA MADISH TV SHOW

Nakutembelea ulipo,nakuuliza maswali machache tu,unauliza unachojisikia,ukinishawishi nakupa king'amuzi bureee hii ikiwa pamoja na kufungiwa papo hapo,pia kama tayari una king'amuzi na una shida za king'amuzi chako nakumalizia tatizo papohapo.
KUTOKA KWANGU KUJA KWAKO MPENDWA...
Kushindwa kufanya kila ulichopanga kufanya katika mwaka huu,maana yake si kushindwa kufanya milele,chukulia kama safari uliyochelewa kufika lakini jitahidi uwezavyo mpaka ufike hivyo mwaka 2015 jitahidi ufanye kila ambacho ulipanga kufanya mwaka huu na ukashindwa,kaa leo jiulize wapi ulikosea na kisha sahihisha makosa yako ili mwaka 2015 usiishe bure!
Zaidi ya yote nawatakia heri ya mwaka mpya!
12:11 AM   Posted by Mustapha Hanya with No comments

0 Unasemaje..??:

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search