Call / WhatsApp +255673378129

Jul 9, 2014

BVN CHANNEL - OYSTERBAY DAR ES SALAAM


Nakumbuka mwaka 2008 niliwahi kupata mteja wa channel hii,tena ilikuwa baada ya mafundi kadhaa kuambulia patupu ikiwa wameshapoteza siku kama si masaa!!
Kipindi hicho niliweza kufanikiwa kuipata kwenye Dish ya ft8,nikimaanisha c band!
Oysterbay jijini dar,wenzangu na mie wanapaita pa kishua ila sina sababu ya kubisha!
Hakuna tofauti na mteja wangu yulee wa miaka ile,kwa maana wote wametokea taifa hilo na walihitaji channel ya nchini mwao!

Kwenye KU ft4 na Receiver ya kawaida tu,Mustapha MaDish nikaileta Netherland Tanzania kwa dk zisizozidi 45,baada ya hapo kuchapa mwendo kukahusika!


Kwa mahitaji ya Mafundi/Ving'amuzi vinatumia Dish aina zote hapa ndipo jibu lako!
Piga:-0789476655/0732575718/0859161111
Email:mustaphamadish@gmail.com
Mahali:Magomeni Mapipa/Morogoro rd 

Share:

Jul 8, 2014

NILIYONAYO KWAKO...

 Baba na Mwana
Nawasikitikia sana wale wanaopiga mechi za kikubwa kisha wanakimbiana,sababu zikiwa nyingi zisizo hesabika huku mwanamke akibaki mjamzito,ujauzito ambao mwisho wake unakuwa sio mzuri sana kwa maana wapo ambao wanaamua kutoa..hapa kwenye kutoa wapo waliofanikiwa kuchota dhambi kwa wingi na wapo waliopoteza maisha wakiwa katika kutimiza hilo!
Pia wapo waliamua kwa dhati kujifungua huku akijua yeye ndiye atakayekuwa baba na yeye ndiye atakayekuwa mama..
Kwa hili wapo waliofanikiwa wachache sana ila wengi wamefail kwa kukimbilia kutoa ama kuzaa na kushindwa kumuangalia mtoto kwakuwa yupo pekee yake..
Matokeo yake idadi ya watoto wa mitaani inaongezeka...
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa angalizo wanawake na waschana wote kwa ujumla Mwanaume,
mimi ikiwa mmojawapo niliyeandika post hii,tuna salio la uongo la kutosha lisilopungua kukudanganya wewe ili tu niingie panapofanya wewe ukaitwa mwanamke..
Bahati mbaya hata muambiwe vipi uelewa wenu wengi wenu ni tatizo,tena tatizo kuwa..
Ila alau hata kwa mwezi mara tatu ama mbili si vibaya tukazungumza alau kukumbushana tu kwa yale machache niliyonayo kwenu wapendwa!
Share:

Jul 7, 2014

C BAND FT12 - ADA ESTATE

Sababu iliyonileta hapa

  Baba yake na Fetty

Moja kati ya wanafunzi wangu wa kwanza kwanza kuwapa ujuzi huu ni huyu ambaye anaitwa Dullah kwa sasa amekula ajira pale Multichoice Tanzania ( DSTV ).
Kutoka ku moyo najisikia faraja sana kuona nasababisha mtu au watu fulani hasa vijana wenzangu kupiga hatua moja juu ikiwa kwenye kutengeneza maisha yake na familia yake kwa ujumla!
Nashukuru hakuna aliyenisahau ijapokuwa si wote kati ya wanafunzi wang ambao tunawasiliana mara kwa mara,najua ubize unaweza ukawa umechukua nafasi yake ama mambo ya hapa na pale.
Kwanini nimemzungumzia Dullah kwasababu hii kazi ya leo ilikuwa yake,mteja alimpigia mara kadhaa kwa siku tatu lakini muda wa Dullah ulikuwa mdogo hivyo kutokana na ushirika mzuri ndipo akaileta mezani kwangu ili tumalize tatizo la huyu mteja!
C band hii si ile iliyozoeleka na mafundi wengi ft6 ama ft8 hii ni ft12.
Nami nilienda nikijua ni ft6 kama ambavyo Dullah alidhani,hata spana ilinilazimu kurudi tena ofisini kuchukua kwa maana zile nilizobeba hazikuwa na uwezo wowote wa c kufungua hata kufunga tu.
Hapa angeenda ndugu yangu lazima angehitaji twende sote kwa maana Dish hizi zinahitaji uwezo wa ziada!
Kwanini naitwa MUSTAPHA MADISH ndipo nikadumisha umwamba wangu kisha tukachapa mwendo!
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita