Mar 20, 2015

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu bei za ving'amuzi katika mikoa yote ukiacha dar es salaam ijapokuwa baadhi ya wauzaji wa dar es salaam hili linawahusu!
Hapa nazungumzia ving'amuzi vyote vilivyopo tanzania,kampuni husika wanatoa bei elekezi ambapo bei hiyo inapaswa kuuzwa kwa mikoa yote tanzania bila kuongeza hata senti 5.
Unaweza ukaona ni jambo ambalo haliwezekani ila mimi najua ya kuwa inawezekana kama muuzaji ni wakala aliyeidhinishwa na kampuni hhusika.
Mfano wakala anaponunua azam tv kwa jumla anapata punguzo maalum na kuna utaratibu wa kurudishiwa pesa ya usafiri kwa kuzingatia mkoa gani anatoka,pia ving'amuzi vyengine wanautaratibu wao unaofafana na huo ili tu kufanikisha mawakala wote katika mikoa yote waweze kuuza bei elekezi na si vinginevyo!
Kinachotokea kutokujulikana kwa mawakala walioidhinishwa kwa baadhi ya mikoa kumesababisha wafanyabiashara kujiamulia kununua tu ving'amuzi na kuweka kwenye maduka yao na kujiuzia bei wanazotaka wao huku wakiwa hawajui vema kuhusu hivyo ving'amuzi,hii imepelekea malalamiko kuwa mengi kwa mteja kuchelewa kufunguliwa ili aweze kuona ama chochote kikitokea cha kiufundi aliyemuuzia anashindwa kumpa msaada unaostahiki kwa wakati.
Kwa maoni ushauri:+255789476655
10:01 PM   Posted by Mustapha Hanya with 3 comments

3 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Mfano hapa mafinga bei ya azam tv ni tsh laki mbili bila ufundi sasa hii maana yake nini na mnatusaidiaje

Anonymous said...

huku dodoma pia wanauza 177500 bila kifurushi wala kufungiwa hivi ikiwwa hili jambo mnalifahamu kwanini hamlifanyii kazi???

Nancy Salmin said...

Tunachofanya ni kuwasaidia wateja wa ving'amuzi vyote kuwapa maelekezo ya wapi waende kununua kwa mawakala ambao wanauza bei elekezi kwa mkoa wowote ulipo..

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search