Call / WhatsApp +255673378129

May 18, 2015

KWANINI TUMELAZIMIKA KUIGIA DIGITAL NA KUACHANA NA ANALOGUE?


Mabadiliko katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojia kwenda katika mfumo wa dijitali ni utaratibu ambao unaendelea ulimwenguni kote. Mabadiliko haya yanatokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya masuala ya mawasiliano yaani International Telecommucations Union yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi. Makubaliano ya nchi wanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa analojia na kutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni 2015. 

Ili kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na pia kutoa muda wa kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka 2005 Serikali ilianza mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ambao ulihusisha wadau wote, wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa televisheni, hatua kwa hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo ya analojia. Kwa kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo:

Mwaka 2005:   Waraka wa kwanza wa mashauriano (consultative document) kuhusu umuhimu na faida za kuhama kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;

Mwaka 2006:   Waraka wa pili wa mashauriano na mapendekezo ya muundo wa leseni kwenye mfumo wa utangazaji wa teknolojia ya dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;

Mwaka 2007:   Kamati ya kiufundi inayoshughulikia uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali iliundwa;

Mwaka 2007:   Mkutano mkuu uliojumuisha vituo vyote vya utangazaji nchini ulifanyika Bagamoyo kupitisha maazimio ya mfumo wa leseni za utangazaji utakaotumika kwenye mfumo wa dijitali;

Mwaka 2010:   Kampuni tatu (3) zilipewa leseni za ujenzi wa miundombinu ya utangazaji ya dijitali. Kampuni tatu zilizopewa leseni za kusambaza matangazo ya dijitali ni Agape Associates Limited, Basic Transmission Limited, na Star Media (T) Limited. Kampuni hizo zilipewa leseni baada ya kuthibitisha kuwa zina uwezo wa kujenga miundombinu ya kurushia matangazo katika mfumo wa dijitali;

Mwaka 2010:   Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Mabadiliko ya Utangazaji toka mfumo wa analojia kwenda dijitali iliundwa. Kamati hii hukutana kila baada ya miezi mitatu kutathmini maendeleo ya ubadilishaji wa mfumo wa utangazaji;

Mwaka 2011:   Kampeni ya Kitaifa ya kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa Tanzania rasmi nchi nzima mwisho wa kutumia mfumo wa Analogue ni tarehe 31/12/2014 saa 23;59.
Tukahamia mfumo wa Digital,ambao huu wa ving'amuzi tulionao ijapokuwa ilikuwa mwisho ni tarehe 17/06/2015,kuhama mapema ni namna ya kuangalia je kuna changamoto gani na vipi wahusika wanakabiliana nazo.

+255789476655
Share:

2 Unasemaje..??:

Nassor Rajabu said...

Technologue imefanya vitu vingi vibadilike likiwa mojawapo la huu mfumo wa tv hivyo hatuna budi kuyapokea na kuyafurahia ili tuendane na Technologue..
Big up Mustapha

Anonymous said...

Baada ya kupitia hii blog ndipo nimegundua ni kwanini tumelazimika kuingia katika mfumo wa digital thanks bro!

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita