Jul 22, 2015

TV INSTALLATION
Mapendekezo ni ya mteja kwa maana mmiliki wa hotel/sehemu yeyote husika 
kwamba tv zikae ukutani ama mezani,kazi yetu ni kutoa ushauri kwa jinsi mazingira yalivyo,je muonekano mzuri ni upi tv kukaa mezani ama ukutani? ingawaje mara nyingi tv kukaa ukutani ndo huwa zinapendeza na salama pia.

CHANNELS INSTALLATION
Tunatoa nafasi kwa muhusika kusema channel anazotaka ambazo angependa kuziona zinapatikana,pia tunatoa ushauri kwa channel atakazo kama zimejitosheleza ama kuna umuhimu wa kupunguza ama kuongeza kutokana na uzoefu tulionao tunajua mapenzi ya wateja wengi wa hotel/office n.k. kwa channel zinazopendwa sana!
- Control room
Hapa tunahifadhi channel zote tunazohitaji,kisha tunazisambaza kwenye tv zote zilizopo kwa ubora mmoja nikiwa na maana quality ya picha ni moja kwa tv zote hata zikiwa 100.

- Remote Control
Kwa kila tv iliyopo kwa kila chumba itajitegemea kubadili channel kwa kupitia Remote ya tv husika bila kumbugudhi anayeangalia tv nyengine.

PROJECTOR INSTALLATION
Kama ilikuwa hujui Projector inatengenezwa kwa masaa maalum,nikiwa na maana ya kuwa mathalani projector imetengezwa  itumike kwa masaa matano ( 5 ) yakitimia masaa matano hakuna njia ya kurenew yale masaa kwa lugha nyepesi itakulazimu ununue projector nyengine.Tupo kwa ajili ya kutoa ushauri na kukufungia pia popote panapostahili.

REPAILING
Inapotokea unakutana na ujumbe mmojawapo kati ya hii ifuatayo jua ya kuwa fundi anahitajika,inaweza kuwa kiushauri ama kiufundi zaidi kwa fundi kufika eneo husika.Ila kwa ushauri wa awali angalia cable yako ipo sawa? angalia je connector yako imekaa sawa? kwa upande wa Receiver/Decoder/tv ama kutoka kwenye Dish ama chanzo chochote cha channel!
- Bad Signal
- Signal Weak
- No Signal
- No Channel
- No Program
- No Service
- Searching for Signal

BAADHI YA KAZI ZA HOTEL TULIZOFANYA:-
- Bahari Lodge
- JB Belmont
- Geraffe View Hotel
- Transit Motel

UZOEFU:-
Yapata miaka nane ( 8 ) Mustapha MaDish nimejikita ukanda huu,nafunga Dish Antenna aina zote kwa channel za bure na kulipia,nadeal na receiver/decoder aina zote,nina team kazi yenye vijana wenye uzoefu unaozidi miaka miwili kwenye taaluma ya ufundi.
Nimefundisha vijana wapatao 17 ambao kwa sasa wanaendesha maisha yao kupitia taaluma hii wengine wakiwa wameajiriwa Multichoice Tanzania ( DStv ) na wengine makampuni mengine.
Najua kiundani kuhusu ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania.


UNA SWALI..?
UNAHITAJI HUDUMA..?
MSAADA ZAIDI..!
PIGA SIMU +255 714 973 797

3:01 PM   Posted by Mustapha Hanya in with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Natamani huduma zenu ila sidhani kama nitamudu gharama

Anonymous said...

Malipo ya dstv kwa hotel inakuwaje wanalipaje kwa decoder kama 5 hivi!

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search