Aug 9, 2015


KUTOKA KWANGU KUJA KWENU:
Imezoeleka hii tabia hasa kwa wateja wa DStv na Azam tv wale ambao wenzangu na mie yaani wachumi sanaa! Ambao sijajua vizuri kuwa wanajua sana thamani ya pesa zao ama ni nini!?
Ila hii nadhani uswahili pia unahusika katika hili!
WATEJA WA AZAM TV:
                         Utakuta kama hakuna mpira mtu haangaiki kulipia king'amuzi chake anangoja inapofikia either kuna mechi kubwa ama ligi inaanza ndipo anataka kulipia hii siwezi kusema si sahihi kwakuwa pengine mapenzi ya mteja ni mpira tuu na ndo maana hakuna malipo ya ziada hata kama hujalipia miezi mingapi ila wanachoanguka wengi ni kushindwa kujua wanapaswa kulipia wakati gani!?
Kama ligi ama mechi unayotaka kuangalia inaanza leo inakupasa ulipia alau siku mbili kabla ya leo ili kuondoa usumbufu kama haitakuwa imefunguka katika kufatilia ili ufunguliwe lakini wengi wenu mnachofanya kama ni mechi leo saa 8 mchana wenyewe mnalipia leo hii hii tena saa 6 mchana kwa kutegemea saa 8 mchana itakuwa imeshafunguka,matokeo yake hakuna ambacho utapata zaidi ya karaha na kujikuta unazungumza maneno yote unamaliza na kuponda huduma za azam tv kwa nguvu zote kumbe uzembe ni wako mwenyewe.
Pengine uliwahi kulipia kwa mtindo huo na ikafunguka si wakati wote itafunguka wakati mwengine system inashindwa kufanya kazi ipasavyo na muda huo simu zote zinakuwa zipo bize kutokana na idadi ya wateja wengi wanafanya ambacho wewe umefanya.
WATEJA WA DSTV:
                         Mfano wa jana tu,simu zangu zote zilikuwa bize kwakuombwa kutoa msaada wa kuwafungulia wateja wa dstv ambao wamelipia lakini hakuna wanachoona,wengine walitoa ya moyoni kuwa tayari wameshajaza wateja kwenye sehemu zao wanazoonyesha mpira lakini bado hakuna kinachoonekana matokeo yake wanalalama watapigwa watu wameshatoa pesa zao!
Hivi kama wewe ni mfanyabiashara wa kuonyesha mpira kwanini usilipie kabla ya siku ya mpira ili kuondoa usumbufu!? Hivi unajua ukiwa mbabaishaji unapoteza hao wateja wako?
Pia kama unahama kifurushi ni lazima ulipia kifurushi unachotaka then unapiga simu ili ubadilishwe hicho kifurushi unachokitaka lakini nawe unangoja siku ya mpira ndo ufanye hivyo!
ANGALIZO:
                Hakuna siku ambayo kampuni za ving'amuzi si DStv si Azam zinakuwa bize kama siku za kuanza kwa mpira,hii si kwenye simu zao hata kwenye ofisi zao na wakati mwengine hata system inaelemewa.
USHAURI WANGU KWAKO:
                                   Lipia king'amuzi chako siku mbili kabla ya mechi ama tukio unalokusudia kuangalia hii itapelekea kuondokana na usumbufu,bila kufanya hivyo utaona huduma za king'amuzi husika hazifai kumbe wewe ndiye hufai.


+255789476655 | +255714973797

5 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hata hivyo nao wajipange ili tuweze kupata vitu kwa wati sio mpaka mambo ya kupiga piga simu ni usumbufu sana ukizimgatia tunalipa pesa nyingi

Anonymous said...

Highly descriptive article, I enjoyed that bit. Will there be a part 2?


Also visit my homepage interesting read

Anonymous said...

Hv kwnn unapenda kuzungumzia paytv pekee

Anonymous said...

Kama chanel za mpira zipo nyingi tu kuna risiva zinazofungua bila hata ya malipo

ally kambi said...

Msaada wako ni mkubwa sana aiseee...

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search