Oct 18, 2015

OCTOBER 25 | FANYA KWELINAJIVUNIA KUWA MTANZANIA
Popote nitasimama na kujivunia kuwa mtanzania mzawa,najivunia lugha yetu kiswahili najivunia na mengi mazuri yaliyopo nchini mwangu,nchi huru ambayo najisikia kufanya chochote wakati wowote pasi tu kuvunja sheria...
AMANI  IMESABABISHWA NA UPENDO
Ni jambo tunalojivua mpaka leo hii,sababu kubwa ikiwa ni upendo tulionao baina yetu.Daima tujitahidi kuidumisha amani hii tuliyonayo ambayo ni kama ndoto kwa baadhi ya mataifa mengine.
KIZAZI CHA DIGITAL
Kuna kundi kubwa la vijana ambao naweza kusema ni kizazi cha Digital,nikiwa na maana yakuwa ndio wenye chachu kubwa ya kutaka mabadiliko kuliko kizazi cha Analogue..
UNA KADI YA KUPIGIA KURA?
Zimebaki siku chache mnoo! swali langu ni kwamba una kikatio? ama unampigia kampeni tu mgombea unayempenda ila kura humpigii!!? Je umefikisha umri wa kupiga kura ama unabishana tu kuhusu mgombea unayeona anafaa!?
KWANINI UNAMCHAGUA!?
Unayekusudia kumchagua siku ya kupiga kura october 25,umejiuliza ni kwanini unamchagua!? Unamfahamu? Umekula pesa yake? Unaamini atatekeleza kile alichoahidi? Unampenda tu? Ama kwanini!!?
OCTOBER 25 USIFANYE MAKOSA
Kura yako itasababisha kile unachokitarajia kutokea kitokee,unahitaji tutoke hapa tulipo tuelekee hatua nyengine nzuri zaidi? kura yako ndio itakayoleta mabadiliko hayo!
Tukapige kura tuwachague wale viongozi ambao tunaona watatuletea mabadiliko,watakaotuletea maendeleo na sio vinginevyo.
TUKUBALI MATOKEO
Uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti na miaka yote kiukweli kabisa,mwaka huu ile hamasa imekuwa kubwa mno naweza kusema kile kizazi cha Digital hakitaki mchecho wanachotaka kuona mambo yanaenda sawa na si ubabaishaji.Kama ambavyo tunatokea wengi kwenye kampeni tunapaswa kutokea wengi kwenye kupiga kura pia.Jambo la kuzingatia ni kwamba tukubaliane na matokeo yatakayotokea kwa zile kura tutakazopiga.
Ili tuweze kuendelea kuilinda amani yetu tuliojaaliwa na Allah.
+255 MUNGU IBARIKI TANZANIA
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: