Nov 1, 2015


Swali ambalo kila kukicha nakutana nalo kutoka kwenu..
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vilivyopo Tanzania ili niweze kukwambia kilicho bora..
Azam tv
 Continental
Coconut Digital tv
DStv
Digitek
Easy tv
Startimes
Ting
Zuku tv
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vyote vina ubora wake na mapungufu yake,itakapotokea umemiliki king'amuzi kimojawapo kati ya hivyo lazima utatoa sifa na mapungufu pia ila tatizo linakuja pale mapungufu yanapozidi sifa jibu linakuwa hakifai ila kama itatokea sifa zikazidi mapungufu jibu linakuja ndicho king'amuzi bora.
Ili ujue ni king'amuzi gani bora inapaswa kutambua wewe muhitaji vifuatavyo:-
 • Unataka kuangalia nini? ( Unapendelea channel gani )
 • Unataka kuangalia picha katika ubora upi?
 • Uwezo wako kifedha wa kununua king'amuzi na kufanya malipo ya mwezi?
 •  
Ukishajielewa wewe mwenyewe ndipo unapaswa kufanya hili la pili:-
 • Tafuta chaguo lako lilipo ( Unachotaka kuangalia kipo king'amuzi gani )
 • Ubora wa kampuni husika na Product ( Huduma zitolewazo ni katika misingi inayotakiwa )
 • Uliza kwa mtu ama watu wanaojua ( wanaotumia/waliowahi kutumia ) king'amuzi unachohisi kinakufaa ili kujiridhisha kabla ya kununua.N.B:usiulize kwenye kampuni husika kabla hujauliza kwa wanaotumia kwakuwa kama kampuni inayouza hicho king'amuzi hakitakupa jibu sahihi ila watakupa jibu la kibiashara ili ununue.
 • Uliza hapa +255789476655 tunajua ving'amuzi vyote kiundani zaidi,jibu utakalopata hapa lifanyie kazi.
 •  
King'amuzi gani unachopaswa kununua baada ya kuzingatia hayo:-
 • Ambacho kina Products nzuri na imara.
 • Ambacho kinajali wateja  
 • Ambacho matangazo yake hayakatikati kira mara pasipokuwa na taarifa.
 • Ambacho kina channel nzuri na picha safi.
 •  
Kila king'amuzi kinajitahidi kufanya kila wawezalo ili wawe wabora,wingi wa ving'amuzi umesaidia hili hivyo kila leo uboreshaji unafanyika kama unaona king'amuzi unachotumia hawana dalili ya kuboresha huduma zao unangoja nini kuhama!?
Kuna king'amuzi kilikuwa na wateja wengi sana lakini sasa ama kila kukicha idadi ya wateja inapungua,unadhani ni kutokana na nini? huduma mbovu na kutotaka kubadilika,hili makampuni mengine mjifunze laa sivyo kila kukicha watabadilishwa Ma sales Manager
+255 789 476 655 
1:29 AM   Posted by Mustapha Hanya with 7 comments

7 Unasemaje..??:

Anonymous said...

I was curious if you ever thought of changing the layout of your site?
Its very well written; I love what youve got to say.
But maybe you could a little more in the
way of content so people could connect with it better. Youve got an awful lot of text for only having one
or two pictures. Maybe you could space it
out better?

my weblog ... lasertest

Anonymous said...

Kaka unataka kuniambia wewe kwa ushauri na utaalamu wako hujui king'amuzi gani bora kwa kusema moja kwa moja kabla hujampa mteja wako mapendekezo yake!?

JOSEPH EMMANUEL said...

Naomba kujua kama azam TV sio local channel na Vp inalipiwa?

Anonymous said...

Dstv na azam ndio mpango ila kama salio la kuunga unga fanya kununua azam tu burudani kwa wote

Joery Joseph said...

Kwa kipato changu naona startimes ndio mpango mzima; nikilipia kifurshi cha sh 600 mambo fresh.

Joery Joseph said...

Kwa kipato changu startimes ndio mpango mzima; nikilipia sh 600 napata chaneli 38 mambo fresh.

Joery Joseph said...

Kwa kipato changu startimes ndio mpango mzima; nikilipia sh 600 napata chaneli 38 mambo fresh.

Call +255789476655

 • Text +255759091445

Follow

Search