Call / WhatsApp +255673378129

Nov 26, 2015

RATIBA YA AZAM TV

Ilikupata ratiba ya king'amuzi chako cha Azam tv:-
Chukua remote yako,bonyeza 1- menu..

2- Digital TV
 

3- Programme Guide 

4- Chagua channel unayotaka kupata ratiba yake ya wiki nzima kama inavyoonekana hapo juu! 
 
5- Ikiwa maelezo hayajaeleweka kwamsaada Zaidi piga +255789476655
Share:

Nov 25, 2015

KUZIMIKA KWA VING'AMUZI BILA TAARIFA KWA WATEJA!

Idadi ya simu ninazopokea kwa takribani wiki tatu mpaka leo hii ni wateja wa baadhi ya ving'amuzi ambavyo vimekata matangazo yao bila taarifa yeyote kwa wateja wao na kitu kibaya zaidi ushirikiano unakuwa sio mzuri kwa mujibu wa wateja wanaonipigia mimi!


Ving'amuzi vilivyokata ni ZUKU tv.
Ijapokuwa ikarejea hewani ila hakukuwa na taarifa yeyote ama kuwataka radhi wateja wao.
TING nao wakapotea hewani mpaka leo hii na mchezo ni ule ule hakukuwa na taarifa wala kuomba radhi kwa kwa nguvu ile wanayotumia kuuza ving'amuzi!

CONTINENTAL pia hawapo hewani!
Ubaya ambao unatokea hapa taarifa na kuwataka radhi wateja hakuna kwa nguvu ile wanayotumia kuuza king'amuzi na kwa bahati mbaya Continental wana nafasi nzuri ya kufikisha ujumbe kwa umma kupitia Startv ama RFA lakini matangazo yanayoendelea ni yale ya kuuza ving'amuzi!
ANGALIZO TOKA KWA MUSTAPHA MADISH:
Tatizo lililopo kwa Continental na Ting ni satellite waliyopo ya Amos 5:-
Jukumu la makampuni waliyopo Satellite hii walitakiwa watoe taarifa kwa wakati kwa wateja wao ili waendelee kuwa na imani nao kwa maana ipo wazi kifundi tunajua Satellite ya Amos 5 haipo tena imepotea hivyo ili Ting na Continental ni lazima wahame Satellite je watahamia Satellite gani hilo wanalijua wahusika.
Yapo matatizo ambayo huwezi kuyazuia kwakuwa najua vema mfumo mzima ulivyo,yapo ya kuepukika na yapo ambayo hayaepukiki,ila kinachopaswa kufanyika ni kutoa taarifa kwa wakati kwa wateja wenu na kwa umma kwa ujumla huku mkiendelea kutatua tatizo kwa wakati,kukaa kimya kwenu ni kupoteza imani kwa wateja wenu,inaonekana mnatoa huduma mbovu na hii inapelekea kufanya maamuzi ya kuamua kununua king'amuzi kingine!
+255789476655
Share:

Nov 19, 2015

UNATAKA KUJUA NINI KUHUSU DIGITAL TV ?



Yapo mengi ambayo siwezi kuyamaliza kwa siku moja na pia siwezi kuyamaliza ikiwa sijajua ambacho wewe ungependa kujua kuhusu ulimwengu huu wa Digital tv na hata ukihitaji kujua yale ya Analogue tv nipo tayari kukujuza kwa kina kabisa!
Ni nini ambacho ungependa kukijua yawezekana kuhusu king'amuzi chochote kati ya vilivyopo Tanzania ama vinavyotumika Tanzania ingawaje ninauzwa nje ya nchi.Hata kama swali halihusiani na ving'amuzi ila tu linahusiana na ulimwengu huu wa Digital tv nnachoweza kusema karibu alau tuwekane sawa.

NIULIZE:
  • Chochote ambacho ungependa kujua ikiwa kutokea kule tulikotoka Analogue tv ama hapa tulipo Digital tv.
  • Jambo lolote la kiufundi ambalo linakutatiza katika ving'amuzi vyote vilivyopo.

Ili na wengine wanufaike na majibu ya maswali yatakayoulizwa naomba muulize kwenye sehemu ya ku comment nami nitajibia hapo ili maswali yasijirudie!
Share:

Nov 16, 2015

DSTV HUDUMA KWA WATEJA NA KUPATA MAFUNDI WA DSTV


Je unatumia DStv? ama unahitaji kujiunga na DSTV? 
Karibu kwa kufata utaratibu huu:-

IKIWA UNATUMIA DSTV:
  • Umelipia na bado hupati channel?
  • Picha inakatakata ama haionyeshi kabisa
  • Unataka kuhama toka nyumba moja kwenda nyengine
  • Unahitaji kuongeza Decoder nyengine ama kubadili
  • Unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu bei mpya za vifurushi
  • Unahitaji kujua chochote kuhusu huduma za DStv
  • Unahitaji Fundi 
  • Msaada wowote wa kiufundi
Dish ya DStv ikiwa kwenye setting!

Fundi akifanya ufundi wake!

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi! 

UNAHITAJI KUJIUNGA NA DSTV
  • Kujua Bidhaa zote za DStv
  • Kujua bei halisi/Offer ya kununua king'amuzi
  • Kujua bei halisi ya vifurushi Bofya Hapa
  • Kujua bei ya Ufundi
  • Kujua namna ya kuweza kuunganishwa
  • Kupata huduma ya kuletewa ulipo na kulipia baada ya kuletewa
  • Ikiwa umenunua na hujafungiwa ili upate fundi popote ulipo Tanzania
  • Yote yanayohusu DStv

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi!


Share:

Nov 1, 2015

VIFURUSHI NA CHANEL ZA STARTIMES



Ni moja kati ya makampuni ambayo yanamiliki ving'amuzi aina mbili tofauti kimasafa,nikiwa na maana ya kuwa kuna aina mbili ya Decoder za startimes:
  • StarTimes ya Antenna
  • StarTime ya Dish
Kwa kukurahisishia startimes wakati wanaanza hapa nchini walianza na mfumo wa kutumia Antenna tu,mfumo huu ukawa na lawama nyingi sana katika swala zima la kukatakata kwa picha wakaja kuboresha kwa kuleta na mfumo wa Dish ingawaje hata ule mfumo wa Antenna nao kwa sasa upo vizuri umeboreshwa!

Hivi ndivyo vifurushi vya StarTime:-

KWA KING'AMUZI CHA DISH

1- KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 11,000 Kwa mwezi
Tsh 4,000 Kwa wiki
Tsh 1,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2- KIFURUSHI CHA SMART
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 21,000 Kwa mwezi
Tsh 8,000 Kwa wiki
Tsh 2,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-STARTIMES SPORT PLUS ( Cha ziada )
Ina channels 4+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4- KIFURUSHI CHA SUPER
Ina channels 100+ bora!
Bei yake ni Tsh 36,000 Kwa mwezi
Tsh 12,000 Kwa wiki
Tsh 3,600 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5- STARTIMES CHINESE PACKAGE
Inajumuisha kifurushi cha Smart
Ina channels 84+ bora!
Bei ni Tsh 43000
Bofya hapa kujua channels zilizopo katika kifurushi hiki!

6-STARTIMES INDIAN PACKAGE 
Sasa inapatikana kama kifurushi cha ziada
Ina channels 8+ bora!
Bei ni Tsh 18000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

KWA KING'AMUZI CHA ANTENNA

1-  KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 9,000 Kwa mwezi
Tsh 3,000 Kwa wiki
Tsh 900 Kwa wiki
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-  KIFURUSHI CHA MAMBO
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000 Kwa mwezi
Tsh 6,000 Kwa wiki
Tsh 1,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-  KIFURUSHI CHA UHURU
Ina channels 80+ bora!
Bei yake ni Tsh 20,000 Kwa mwezi
Tsh 7,000 Kwa wiki
Tsh 2,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!




Kwa Maelezo zaidi
Instagram @mustaphamadish
Call / Whatsapp / Text 
+255 658 046 655
Share:

KING'AMUZI GANI BORA TANZANIA!?


Swali ambalo kila kukicha nakutana nalo kutoka kwenu..
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vilivyopo Tanzania ili niweze kukwambia kilicho bora..
Azam tv
 Continental
Coconut Digital tv
DStv
Digitek
Easy tv
Startimes
Ting
Zuku tv
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vyote vina ubora wake na mapungufu yake,itakapotokea umemiliki king'amuzi kimojawapo kati ya hivyo lazima utatoa sifa na mapungufu pia ila tatizo linakuja pale mapungufu yanapozidi sifa jibu linakuwa hakifai ila kama itatokea sifa zikazidi mapungufu jibu linakuja ndicho king'amuzi bora.
Ili ujue ni king'amuzi gani bora inapaswa kutambua wewe muhitaji vifuatavyo:-
  • Unataka kuangalia nini? ( Unapendelea channel gani )
  • Unataka kuangalia picha katika ubora upi?
  • Uwezo wako kifedha wa kununua king'amuzi na kufanya malipo ya mwezi?
  •  
Ukishajielewa wewe mwenyewe ndipo unapaswa kufanya hili la pili:-
  • Tafuta chaguo lako lilipo ( Unachotaka kuangalia kipo king'amuzi gani )
  • Ubora wa kampuni husika na Product ( Huduma zitolewazo ni katika misingi inayotakiwa )
  • Uliza kwa mtu ama watu wanaojua ( wanaotumia/waliowahi kutumia ) king'amuzi unachohisi kinakufaa ili kujiridhisha kabla ya kununua.N.B:usiulize kwenye kampuni husika kabla hujauliza kwa wanaotumia kwakuwa kama kampuni inayouza hicho king'amuzi hakitakupa jibu sahihi ila watakupa jibu la kibiashara ili ununue.
  • Uliza hapa +255789476655 tunajua ving'amuzi vyote kiundani zaidi,jibu utakalopata hapa lifanyie kazi.
  •  
King'amuzi gani unachopaswa kununua baada ya kuzingatia hayo:-
  • Ambacho kina Products nzuri na imara.
  • Ambacho kinajali wateja  
  • Ambacho matangazo yake hayakatikati kira mara pasipokuwa na taarifa.
  • Ambacho kina channel nzuri na picha safi.
  •  
Kila king'amuzi kinajitahidi kufanya kila wawezalo ili wawe wabora,wingi wa ving'amuzi umesaidia hili hivyo kila leo uboreshaji unafanyika kama unaona king'amuzi unachotumia hawana dalili ya kuboresha huduma zao unangoja nini kuhama!?
Kuna king'amuzi kilikuwa na wateja wengi sana lakini sasa ama kila kukicha idadi ya wateja inapungua,unadhani ni kutokana na nini? huduma mbovu na kutotaka kubadilika,hili makampuni mengine mjifunze laa sivyo kila kukicha watabadilishwa Ma sales Manager
+255 789 476 655 
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita