Call / WhatsApp +255673378129

Dec 6, 2015

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI DSTV


Wateja wengi wa DStv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue vifurushi vya Dstv kwa Kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha DStv Bomba  Tsh 23,500 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha DStv Compact  Tsh 84,500 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-

1 - Washa Decoder yako,kisha weka channel namba 200.
2 - Lipia Tsh 84,500 
3 - Piga nambari 0768988800 ( Atakayepokea mwambie kuwa unahitaji kubadili kifurushi toka DStv Bomba kwenda DStv Compact nae atafanya hivyo na itapokea ndani ya dk 5 tu )

Unaweza kubadili kifurushi kwa kufata utaratibu huu kwa kifurushi chochote kile na unaweza kufanya zoezi hili hata kabla kifurushi chako hakijaisha!

+255789476655
Share:

Dec 5, 2015

EMANUEL TV | TB JOSHUA

 Ni mkristo gani ambaye ni muangaliaji wa tv na haijui Emmanuel tv? ama hamjui TB Joshua?
Pastol wa kanisa la mataifa yote..
Emmanuel tv ni tv ambayo ina wapenzi karibu dunia nzima,ni tv kubwa sana ya dini ambayo makao makuu yake ni Lagos Nigeria,imeanzishwa 8/3/2006 mmiliki akiwa ni Emmanuel Global Network,Lugha inayotumika ni English,Inarusha matangazo Africa,North/Central America na Europe!
Binafsi na team yangu tumeshafunga sana madish ili wadau waangalie hii tv inapatikana bure kama utafunga kwa kupitia Dish ndogo/kubwa na receiver ya kawaida tu unapata zaidi ya channel 65 zote zikiwa free ikiwemo hii Emmanuel tv! Ila hata katika baadhi ya ving'amuzi Emmanuel tv inapatikana ila huko ni lazima malipo ya mwezi yahusike vinginevyo huwezi kuiona!

Kwa maelezo zaidi jinsi ya kuipata channel hii na nyengine za Dini!
+255 789 476 655





Share:

Dec 3, 2015

FUNDI DISH HUJISIKII VIBAYA | KWA UCHAFU HUU!?

 Lawama zimekuwa ni nyingi kuhusu Ving'amuzi kusumbua,ambapo Ving'amuzi vinavyolalamikiwa wala havina usumbufu huo,katika kuchunguza nimegundua ya kuwa mafundi husababisha Ving'amuzi vionekane vinasumbua hata kama havina sifa hiyo ijapokuwa kweli kuna Baadhi ya Ving'amuzi vinasumbua ukiachilia uwezo wa fundi..
Baadhi ya Dish nilizowahi kukutana nazo na nikabahatisha kupiga picha ni hizi hapa chini:-

 Dish ya ZUKU tv
Badala ya fundi kutoboa na Drill yeye alichofanya ni kutafuta mawe na mbao na kufanya alichofanya kama ambavyo macho yenu yanaona hapo,matokeo yake kila baada ya muda mfupi picha itakuwa inakata kata ama hata kupotea na matokeo yake fundi hakauki kwako mwisho wa siku king'amuzi hiki kinasumbua!
 Hizi ni Dish za Azam tv
Nilikutana nazo pale Ubungo National Housing,hii ya mbele ndio mpya kwa muonekano na ya kule mwisho ya siku za nyuma kidogo,kilichofanyika hapa ni kile kile uzembe wa fundi wa kutokutoboa na Drill!

Alichofanya fundi ni kutafuta misumari ya zege na kugonga mpaka nadhani alijibonda midole kwa maana zege hili sio la kitoto..

 Baada ya kukata misumari kadhaa maana ulishindwa kuingia wote akaonelea atafute vitu vya kuweka ili kuweza kukaza kwakuwa msumari hauwezi kuingia wote,juu ya kichwa cha msumari kumewekwa bolt kwa ili pia kuweka mkaze ambao haijasaidia chochote..

 .....!!

 Kwakuwa kazi yote aliyoifanya haijasaidia kitu fundi huyu akaonelea atafute na kamjiti ili kuizuia Dish hii isishuke na kupoteza signal..

 Fundi wetu huyu akamalizia kwenye kuchomeka cable kwenye lnb,ukiachilia uchafu alioufanya hapo pia kuna kitu hajakifunga hapo ambacho kazi yake ni kufunika kabisa hayo maungio ya hiyo cable,je unayajua madhara ya ufundi huu..!!??

 Kazi ya fundi hiyoo...!!!

 Yametafutwa mawe yalipo yakapangwa kwa uchungu ili kuhakikisha signal zinapatikana na hazipotei..
Ah jamani kweli hii hata hujisikii vibaya bwana fundi..!!??

 Ile ya zege ikagongwa hapa kwa mbwembwe balaa..

 Hivi mteja wako unayemfungia ameona kazi hii?

Hii ni maeneo ya Kimara ila hii cha ajabu ni kwamba ilipofungwa mteja anaona kila kitu jinsi ilivyo sasa ambacho nimeshindwa kuelewa ameridhika na uchafu huu ama vepe!
 Hii ni Dish ya DStv

 Macho yako yameona nini hapo...!?

 Ni wazi kuwa ukuta huo haufai kubeba hii dish ila alichofanya bwana fundi akatumia ufundi wake kuonyesha yakuwa hata kama ukuta haufai yeye anauwezo wa kufanya ukafaa..

 Fundi na ufundi wao..!

 Hapa uhakika wa signal hakuna kabisa...

 Hii nadhani inatokea kwa mafundi dish wa Tanzania tu!


Hapa utalaumu King'amuzi unachotumia ama fundi aliyekufungia?
Nnachoweza kukusihi angalia sana kazi anayokufanyia fundi wako zinafanana na hizi?
JE UNAHITAJI FUNDI KWENYE KAZI SAFI TOFAUTI NA UCHAFU HUU KWA AJILI YA KING'AMUZI CHOCHOTE UNACHOKIJUA WEWE?
PIGA +255 789 4766 55



Share:

Dec 1, 2015

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI AZAM TV


Wateja wengi wa Azam tv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue Vifurushi vya Azam tv kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Azam Pure Tsh 15,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Azam Plus Tsh 23,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Lipia kwanza Tsh 23,000 kisha chukua simu yako bonyeza *150*50*5# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu Azam tv
Chagua
  1. Kiswahili <
  2. English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
  1. Angalia salio
  2. Badili kifurushi <
  3. Sajili Huduma Mpya
  4. Endeleza Kifurushi Cha Nyongeza
( Unachagua Badili kifurush,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata nia:-
  • Tafadhali ingiza namba ya Smartcard
( Weka namba za Smartcard yako,kisha una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
  1. Pure 15,000
  2. Plus 23,000 <
  3. Play 28,000
  4. Kihindi Pekee 16,000
( Unachagua namba 2,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
  1. Badili sasa hivi <
  2. Badili baada ya kifurushi kuisha
( Unachagua namba 1,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-

Asante. Ombi lako linashughulikiwa. Utapata ujumbe muda si mrefu.AZAM TV

Kisha utapokea ujumbe mfupi kwenye simu yako unaotoa maelezo kama ombi lako limefanikiwa ama laa!!
Hii ni jinsi ya kuhama toka kifurushi cha Azam Pure kwenda kifushi cha Azam Plus.Utaratibu wa kuhama kifurushi ni huu kwa vifurushi vyote na ikitokea umelipia Tsh 23,000 na haujahama kifurushi itafunguka kifurushi kile kile cha Tsh 15,000 na kubaki kwenye a/c yako Tsha 5,000.Unaweza ukabadili kifurushi ndani ya masaa 72 kwa lugha nyepesi siku tatu na ikitokea imezidi hapo huna budi kupiga simu ili wakusaidie zaidi!
Zoezi hili uhakikishe king'amuzi chako umekiwasha kisha ndipo unafanya zoezi hili na inachukua dk 5 mpaka 20 kubadilika kifurushi na ukitaka kujua zoezi lako limefanikiwa baada ya muda Angalio Salio kwa kutumia utaratibu wa hapo juu!
Kwa uchache huu nadhani nimekusaidia kitu!

+255 789 476 655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita