Apr 15, 2016

AV CABLE NI NINI!?


A inasimama badala ya Audio - Sauti
V inasimama badala ya Video - Picha
Zinakuwa nyaya tatu zenye rangi tatu tofauti:-


Nyekundu - Sauti Kulia
Nyeupe - Sauti Kushoto
Nyano - Picha


Hivyo tafsiri nyepesi ni kwamba AV CABLE ni waya unaosafirisha Sauti na Picha kutoka kwenye kifaa chochote kinachoweza kutoa picha na sauti na kuingiza kwenye TV,kifaa hicho kinaweza kuwa DVD,King'amuzi,n.k.

Cable hii hutumika kwenye TV yenye AV Port yaani ile sehemu ya kuchomekea AV ambapo napo unachomeka kwa kufata rangi kama uvyoona hapo chini!


Zipo tv ambazo hazina AV port ama hicho kifaa ambacho unataka kutumia AV cable hakina AV Port ufanye nini ili uweze kuendelea kutumia AV cable ama Cable nyengine?
Unapaswa uangalie TV/DVD/King'amuzi kina Port gani badala ya AV Port?
Ufanye nini ikiwa TV yako ina AV port moja ama mbili nawe una vifaa zaidi ya viwili unataka kutumia pasipo kuchomoa chomoa AV cable?
Unapaswa kutumia kifaa kinachoitwa AV SELECTOR ili kutaka kujua kinavyofanya kazi Bofya Hapa

mustaphamadish@gmail.com
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Hii ndio sehemu pekee huwa napata info kamili kuhusu huu ulimwengu wa Digital kaka endelea kutupa huu ufahamu

Anonymous said...

TV yangu haina sehemu ya AV natumia cable gani hapo?