Jan 10, 2017

KWA MARA YA KWANZA KWENYE TV YAKO | 2017 SIGNAL QUALITY

Nia ilikuwa muda mrefu hatimae sasa ime ama inatimia.. Awali nilitazamia jina liwe Mustapha MaDish kama ilivyo hii blog lakini baada kukutana na wadau kushauriana ikaonekana Signal Quality ndio litakuwa jina sahihi la kipindi..
Kipindi kitakuwa na Segment mbili:-
  • Site sytine
  • Kwa Kina
SITE SYTINE
Yale yote ya kiufundi yanayohusu king'amuzi chako yatapatiwa ufumbuzi kwa vitendo hapa,uatapata Ushauri,Elimu na Msaada wa kiufundi pia kama king'amuzi chako ulikfungiwa na #FundiKalipua utapata nafasi ya kipekee kufungiwa upya na ile timu ya kina #FundiMakini bureee!! Jukumu lako litakuwa ni kupiga picha Dish yako tu na kusema wapi ulipo na kutufikishia sisi kisha timu yetu itakufikia bila shaka kumaliza tatizo lako!!

KWA KINA
Maelezo na ufafanuzi kwa yale yote yanayokutatiza kuhusu ulimwengu wa Digital tv utapata kusikia hapa na wahusika pia maswali yako utakayouliza majibu utayapata hapa!!

Show hii itaanzia Dar es salaam kisha itahamia mikoani tutaifikia mikoa yote Tanzania ili sote kwa pamoja tuwe tumehamia katika ulimwengu wa Digital kwa vitendo huku tukiujua na kuhufurahia!

ZAWADI
Kwa kila kipindi zawadi ya king'amuzi itakuhusu kwa kujibu maswali yetu yatakayokuwa rahisi tu ama hata ukitushawishi kukupa king'amuzi tutakupa!

Mimi si ndio mwenyeji wako hofu ondoa, cha kufanya pitia pitia hii blog ili ujue:-
  • Lini kitaanza
  • Kituo gani cha tv kitaonekana
  • Zawadi ya king'amuzi gani utapata
  • Utafungiwa upya ikiwa unatumia king'amuzi gani? 
  • Tunaanzia wapi
  • Na maswali mengine unayo wewe..
Kwa maelezo zaidi +255789476655
Ahsante kwa kutembelea blog yangu na nashukuru kwa kusoma Post hii,naimani kipo ulichojifunza.. Jisikie huru kuuliza maswali,kutoa maoni,kuomba ushauri ama kuomba msaada iwe kiufundi n.k Milango ipo wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki nami/nasi ili kutimiza lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi ambayo imehamia katika ulimwengu wa Digital tv huku wananchi wake wakiwa na uelewa wa kutosha na wanafurahia pia. KARIBU!!

Related Posts

0 Unasemaje..??: