Jun 26, 2017

 Hapa ni kwenye jengo la Dar Free Market. 
Hizi ni baadhi tu ya dishi zilizopo hapa,kutokana na taaluma tuliyonayo haikupaswa kufungwa dishi zote hizi...!
Awali ilikuwa Antenna zile za kawaida zilikuwa zinaonekana kama uchafu pindi zikaapo nyingi jengo moja,pia na jinsi zilivyofungwa kutokana na kila mtu na ufundi wake na aina ya Antenna yake..!!
Leo picha ile imehamia kwenye madishi.. si tu kuonekana kama uchafu kwenye jengo moja yanapofungwa madish zaidi ya kumi na mbaya zaidi yote yanaweza kuwa ya kampuni moja..
Na ukija kwenye swala la kiufundi ndipo mwenye jengo ukipata bahati ya kutembelea yalipofungwa hayo madishi utatamani kutoa katazo yasifungwe tena madishi na yaliyokuwepo yatolewe maana wasije wakakuangushi jengo lako....Maana mafundi kina sie tukipewa uwanja wa kujichagulia pa kufunga dishi wee...!!
Sasa solution sisi tunayo ambayo itaondosha wingi ama uchafu wa madishi katika jengo lako..
Tunachofanya ni kufunga dishi moja ambalo litabeba ving'amuzi vya jengo zima..kama ni wapangaji wako watakachopaswa kufanya wao ni kuja na ving'amuzi vyao tu na wanapohama wanahama na ving'amuzi vyao tu...
Hii unaionaje..!?
Kwa maelezo zaidi tupigie:
+255789476655
2:04 PM   Posted by Mustapha Hanya with 1 comment

1 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Mkuu wewe ni zaidi ya Mtaalamu,tunashukuru kwa elimu hii na tunakuomba usichoke kaka uendelee kutupa hii elimu mungu akuzidishie..

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search