Sep 7, 2017


ILI UFANIKIWE...  NIMEJIFUNZA KUZINGATIA MOJA KATI YA VITU MUHIMU.. NI KUPENDA UNACHOFANYA..
..... Hapa siangalii sana napata bei gani ingawaje pesa ndio ambayo hasa tunaitafuta.. Nna mengi ya kuzungumza hapa ila leo somo liwe moja tu kwa Vijana wenzangu na wote ambao mnataka kupata mafanikio katika kile mkifanyacho... Mpende mnachokifanya.. Ukipenda unachokifanya utakifanya kwa juhudi zako zote na wala hautaangalia wanaokukwamisha wanazidi kila kukicha.. Nilipoanza ilikuwa kama utani isipokuwa kwakuwa nilikuwa na mapenzi ya dhati na kazi yangu hivyo wala sikukata tamaa.. nilisimamia ninachokiamini na kujifunza zaidi.. mpaka leo hii idadi ya wanafunzi nilionao wala hakuna ulazima wa mimi kwenda site tena kufunga hata kadishi kamoja.. ningewatuma na bado kupitia wao ningeingiza pesa... Lakini katika vitu nisivyovipenda ni kukaa ofisini... mimi napenda muda wote kuwa site na ndo sababu mpaka leo hii utakapopata wasaa wa kutembelea office yetu ni mara chache sana kunikuta kwa Office nimekaa!
4:42 AM   Posted by Mustapha Hanya in , , with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Anonymous said...

Kaka office ipo wapi!?

Mustapha Hanya said...

Dar es salaam, Magomeni Mapipa, Idrisa street no.110

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search