Call / WhatsApp +255673378129

Showing posts with label Hotel Installation. Show all posts
Showing posts with label Hotel Installation. Show all posts

Nov 23, 2017

DISH 3 | DECODER & RECEIVER 18 | CHANNELS 18 | KWA KILA TV


Hotel - Tv system installation:- 
Hii ni hotel ina flow zipatazo tano ina zaidi ya room 50, ina ukumbi wa mikutano,sherehe, ina restaurant, ina bar na kuna sehemu ya Disco pia. Hapa tulichofanya ni kufunga tv ambazo ni zaidi ya 60 tv ambazo kila moja inapokea channels 18 na kila tv inajitegemea,nikiwa na maana mtumiaji anaweza akabadili channel bila kumuingilia mwengine ( tv nyengine ).




Mfumo uliotumika
  Baadhi ya Vifaa vilivyotumika:-
  • Dish ya FTA
  • Receiver kwa channel za Free
  • Dish ya DStv
  • Decoder za DStv
  • Dish ya Azam tv
  • Decoder za Azam tv
  • Signal Ampl.
  • Splitters
  • Multiswitch
  • Cable 
  • Connectors


Dish zimefungwa tatu, mbili zikiwa ni za kulipia na moja ikiwa ni ya channel za bure,Signal inayotoka kwenye Dish inaingia moja kwa moja kwenye chumba maalum, ambapo tunaita control room, sehemu ambayo decoder na receiver zote 18 zinafungwa hapo na sehemu kubwa ya mfumo mzima unafungwa hapo, kisha zinatoka cable ambazo zinakuwa zimebeba channel 18 na zote zinaishia kwenye tv ambazo zipo vyumbani na kwengineko kwenye jengo la hotel.

Hii ni Control Room sehemu ambayo ile connection muhimu yote tumeimaliza hapa

Kwa maelezo zaidi +255789476655
Whatsapp+255784378129
Face Book


Share:

Aug 9, 2017

KUPATA CHANNELS ZA BURE KWENYE HOTEL/LODGE

 Ili uweze kupata channels za Local ( Tanzania ) kwa kupata habari na vipindi vya nyumbani bila kufanya malipo ya mwezi,hapo hapo kila tv ikijitegemea yenyewe bila kuingiliana na nyengine kwa kila chumba,huku idadi ikiwa kuanzia channel sita ( 6 ) na kuendelea,unapaswa kufanya yafatayo:-


Unapaswa upate vifaa
  • Dish kubwa ya c band
  • LNB ya single solution
  • Receiver kwa idadi ya channels utakazo
  • Cable
  • F connectors
  • Multiswitch
  • Televes
  • Splitter
  • RF connector
  • N.k
 Upate Mafundi wanaojua kazi. #FundiMakini.

Mfumo huu utakuwezesha kuona Channel bila kufanya malipo ya kila mwezi,gharama yako ni mara moja tu kwenye Installation!
Moja ya kazi zetu safi 'King D Hotel'


Kwa maelezo zaidi na kupata mafundi,ushauri na vifaa
Whatsapp+255784378129
Piga +255789476655
Insta @mustaphamadish


Share:

Jul 22, 2015

HOTEL TV SYSTEM INSTALLATION

TV INSTALLATION
Mapendekezo ni ya mteja kwa maana mmiliki wa hotel/sehemu yeyote husika 
kwamba tv zikae ukutani ama mezani,kazi yetu ni kutoa ushauri kwa jinsi mazingira yalivyo,je muonekano mzuri ni upi tv kukaa mezani ama ukutani? ingawaje mara nyingi tv kukaa ukutani ndo huwa zinapendeza na salama pia.

CHANNELS INSTALLATION
Tunatoa nafasi kwa muhusika kusema channel anazotaka ambazo angependa kuziona zinapatikana,pia tunatoa ushauri kwa channel atakazo kama zimejitosheleza ama kuna umuhimu wa kupunguza ama kuongeza kutokana na uzoefu tulionao tunajua mapenzi ya wateja wengi wa hotel/office n.k. kwa channel zinazopendwa sana!
- Control room
Hapa tunahifadhi channel zote tunazohitaji,kisha tunazisambaza kwenye tv zote zilizopo kwa ubora mmoja nikiwa na maana quality ya picha ni moja kwa tv zote hata zikiwa 100.

- Remote Control
Kwa kila tv iliyopo kwa kila chumba itajitegemea kubadili channel kwa kupitia Remote ya tv husika bila kumbugudhi anayeangalia tv nyengine.

PROJECTOR INSTALLATION
Kama ilikuwa hujui Projector inatengenezwa kwa masaa maalum,nikiwa na maana ya kuwa mathalani projector imetengezwa  itumike kwa masaa matano ( 5 ) yakitimia masaa matano hakuna njia ya kurenew yale masaa kwa lugha nyepesi itakulazimu ununue projector nyengine.Tupo kwa ajili ya kutoa ushauri na kukufungia pia popote panapostahili.

REPAILING
Inapotokea unakutana na ujumbe mmojawapo kati ya hii ifuatayo jua ya kuwa fundi anahitajika,inaweza kuwa kiushauri ama kiufundi zaidi kwa fundi kufika eneo husika.Ila kwa ushauri wa awali angalia cable yako ipo sawa? angalia je connector yako imekaa sawa? kwa upande wa Receiver/Decoder/tv ama kutoka kwenye Dish ama chanzo chochote cha channel!
- Bad Signal
- Signal Weak
- No Signal
- No Channel
- No Program
- No Service
- Searching for Signal

BAADHI YA KAZI ZA HOTEL TULIZOFANYA:-
- Bahari Lodge
- JB Belmont
- Geraffe View Hotel
- Transit Motel

UZOEFU:-
Yapata miaka nane ( 8 ) Mustapha MaDish nimejikita ukanda huu,nafunga Dish Antenna aina zote kwa channel za bure na kulipia,nadeal na receiver/decoder aina zote,nina team kazi yenye vijana wenye uzoefu unaozidi miaka miwili kwenye taaluma ya ufundi.
Nimefundisha vijana wapatao 17 ambao kwa sasa wanaendesha maisha yao kupitia taaluma hii wengine wakiwa wameajiriwa Multichoice Tanzania ( DStv ) na wengine makampuni mengine.
Najua kiundani kuhusu ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania.


UNA SWALI..?
UNAHITAJI HUDUMA..?
MSAADA ZAIDI..!
PIGA SIMU +255 784378129

Share:

Jun 29, 2013

TRANSIT MOTEL TENA!


TRANSIT MOTEL AIRPORT 

Nilianzia pale uwanja wa ndege na kisha nikaenda fanya ya kupendeza palee njiapanda ya sitakishari!
Kazi niifanyayo ndo inapelekea mwengine akosolewe maana huwa lazima mteja awe nae kama fundi penye tatizo namsomesha mpaka anaelewa n hata anapotoa pesa yake anajua inatoka kwa mahitaji gani!
Binafsi huwa najisikia furaha kuona namfanyia kazi mtu na mwisho wa siku yeye anapata kile alichokitegemea ama zaidi,kicheko chake mwanya mwengine kwangu!
Nikachukua vyangu na kuaga huku nikikaribishwa tena wakati mwengine!

TRANSIT MOTEL UKONGA
Share:

Jun 6, 2011

Transit Motel Airport

 Baada ya kusababisha Transit Motel ya ukonga kazi ikahamia Transi Motel ya air port na kazi ikawa ni moja tu kufanya TV zionyeshe kwa uzuri ili mteja aweze kidhi haja yake kwa kile anachotaka kukiona..!!

Nikaanza ingia chumba mpaka chumba na hiki ni chumba kimojawapo kati ya vyote vizuri vilivyopo..!!

 Mpaka hapa nikapita,wanapaita RECEPTION kwa niliowaacha ni mapokezi huwezi ingia mpaka upitia hapa


Hapo tayari kwa matumizi ya wageni kama si wenyeji ili maisha yaendelee huku ukiangalia TV ikiwa clear kabisa,ukipuliziwa na AC na pia ukitaka chakula ama kinywaji chochote unapiga tu simu unaletewa chumbani kama hautahitaji kutoka nje..!!
Nami nikachukua kila kilichochangu mwendo nikachapa..!!



Share:

May 31, 2011

TRANSIT MOTEL Ukonga kama kawa kama dawa...!!


 Ilinichukua siku mbili kufanya nilichofanya na kuacha TV za vyumba vyote zikiwa clear kabisa..!!
Inaitwa TRANSIT MOTEL hii ipo ukonga pale njia panda ya kwenda segerea..!!
 Hiki ni chumba kimojawapo kati ya vyote nilivyopita pita na kuacha TV za vyumba vyote vikiwa clear kabisa


Hapa ndipo mapokezi ukifika hapa lugha ambayo utakutana nayo ukiambiwa vyumba vimejaa utajilaumu sana,maana ni mapokezi mazuri na ukarimu ndani yake..!!
Napo kuna TV hivyo nayo pia nikaiweka clear kabisa..!!


 Mito ipo miwili inamaana ukiwa na mwenzako ndo mpango zaidi ila hata ukila alone TV yako itakuburudisha na kukufanya ukajisia uko home..!!

 Hapa ndipo kwenye mlango wa kuingilia...!!!
Imetulia kimuonekano na hata huduma zao na kila chumba kina AC,TV,SIMU vyumba vyote ni self na kama unausafiri utapark ndani ya geti zaidi ya yote bei zao ni kama buree..!!
Tarehe 31 yangu ya leo nimeimalizia hukooo...!!
Share:

May 28, 2011

BAHARI LODGE nimesababisha..!!



Ilikuwa Alihamisi na Ijumaa nilikuwa pale maeneo ya Bahari beach,wenyewe wanapaita njia panda ya kwenda bahari beach hotel dar es salaam,hapa kuna lodge moja ya kisasa safi sana inaitwa BAHARI LODGE..!!
Issue ilikuwa Local hazionyeshi kwa TV zote nami nilihitajika kusababisha hilo ili mmiliki na wateja waendelee kula bata kwa furaha kwa kupata walichokihitaji..!!

 Hii ni mojawapo ya room za hapa Bahari Lodge..!!
Ikawa zinapatikana Local channels zifuatazo:-
ITV
EATV
CAPITAL
TBC
TV TUMAINI
AGAPE
STAR TV
CHANNEL TEN
C2C.
Pia na DSTV kama ambavyo niliikuta,nami nikachukua kila kilicho changu na kushaa...!!


Share:

Nov 21, 2010

C Band Single Solution Cable!!


 Hii ni kwa wale wanaokaa sehemu zenye shida kupatikana Signal,kama mabondeni,karibu na minara ama wamezungukwa na mitambo mitambo!!
C band hii hutumika kwenye Dish ya C band tu ijapokuwa kuna KU ambazo zinahimili interference pia kama ilivyo hii isipokuwa mara nyingi KU hata kwenye interference inakama Signal vizuri!!
Tazama tofauti yake kimuonekano:

Hii ni C Band Single Solution Cable

Hii ni C Band ya kawaida
Pia katika uingizaji wa freeguency kuna tofauti kati ya c band ya kawaida na c band single solution!!
Ambapo kwa single solution unatoa 600 za upande mmoja.
Mf: frequency ya ITV,EATV,CAPITAL-F3642 S8545V (F3042 S8545V),hivyo za V zote unatoa 600 isipokuwa za H hutoi!!!
Share:

Oct 10, 2010

GERAFFE VIEW HOTEL - DAR

Kwenye ukumbi ambao upo baharini wanapaita JET 1,kilichotakiwa hapa ni kufunga Flat Screen na Dstv,nami bila hiyana kama kawaida ile mikono salama ukafanya yake!
* Geraffe View Hotel (DSTV)


 Katika ukumbi huu wa JET 0ne As usually.





 Nafunga Dish sasa!! 

 

 Hapa natafuta signal baada ya kufunga Dish.

  Ni DSTV kama inavyoonekana katika FLAT SCREEN hii. 

+255784378129| Technical Support
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita