Call / WhatsApp +255673378129

Showing posts with label Star times. Show all posts
Showing posts with label Star times. Show all posts

Dec 2, 2016

TV E TANZANIA | KWENYE KING'AMUZI CHAKO



Siku zote ili ufanye vizuri ni lazima upate mpinzani na ndicho kinachotokea hapa..
Historia inaonyesha Clouds Fm ilifanikiwa kuzipoteza radio ambazo alizikuta katika swala la burudani na kupelekea kuunyanyua kwa kiasi kikubwa music wa Bongo Flavour,mpaka ikafikia hatua hata kwa wasanii wa music huo ukienda kinyume na matakwa ya uongozi wa radio hiyo kinachotokea ni kupotea katika game ya Bongo Flavour hapo hapo bado kuna malalamiko mengi ya kwamba kuna unyonyaji!
E - Fm radio,ndio radio pekee inayoonekana imekuja kuleta upinzania mkubwa kwa radio Clouds Fm katika swala zima la burudani.. E - Fm radio wamefanikiwa kuufanya music wa Singeli kuwa biashara.. ukiacha hilo kwa mtazamo wa haraka haraka tu ni kwamba mmiliki wa E - Fm anakijua sana anachokifanya kwakuwa yupo kwenye ukanda huo muda mrefu hivyo alichoangalia udhaifu wa wengine nae akaongeza ubunifu na ndicho kinachompa na kitakachompa mafaniko zaidi..
E - Fm imepelekea kuzalisha TvE - Tanzania ni hatua nzuri sana na ya kupongeza mno..
TvE - Tanzania inapatikana kwenye ving'amuzi vifatavyo kwa sasa:-
  • Azam Tv - channel namba 115
  • DStv - channel namba 295
  • StarTimes channel namba 115
Binafsi nawatakia kila la heri katika kuboresha ili kutuongezea machaguo wapi tuangalie ama kusikiza
+255789476655
Share:

Mar 24, 2016

NINI UFANYE KING'AMUZI CHAKO KIKIPOTEZA SIGNAL!!


Ukiona neno NO SIGNAL ama kwa kukurahisishia ukiona hupati picha kwenye King'amuzi chako na unapata ujumbe ambao hauhusiani na malipo ujue kuna tatizo la Signal lakini utathibitisha vipi kujua kama ni kweli tatizo ni Signal.
> Kila King'amuzi kina channel ya/za bure ( hapa simaanishi Local channel ) ambapo hata ikiwa malipo yako ya mwezi yamekata utaendelea kuangalia tu huwa hazikati,hivyo yakupasa uzijue Channels hizo ili unapoona umepata ujumbe huuelewi jaribu kuweka channels hizo uone zitaonyesha!? Ikiwa zitaonyesha maana yake tatizo sio signal,tatizo litakuwa ni malipo na ikiwa hazitaonyesha jibu lake tatizo ni Signal.Nimejaribu kuwajuza njia hii ya kienyeji kutokana na wengiwetu hizi lugha zilizokuja na ndege ni mtihani nami nimegundua hilo hivyo sitawaacha nitaenda nanyi sambamba!

Cha kufanya ukishajiridhisha kuwa tatizo ni Signal:-
  • Angalia Signal Cable ( waya inayotoka kwenye Dish/Antenna ) ipo sawa?
> Hakuna sehemu iliyochunika/kukatika
> Imechomekwa sawa kwenye King'amuzi chako sehemu ya lnb in/Antenna
> Imechomekwa sawa kwenye Dish/Antenna ya hicho king'amuzi
> Signal Cable ( Coaxial Cable ) Ina nyaya mbili ndani ambazo hazipaswi kugusana ( Siku nitawaeleza kazi za hizo nyaya )

Ikiwa umeona kupo sawa huna budi kuwasiliana na fundi wako ikiwa unamkumbuka ama unaweza kuwasiliana na kampuni husika ya king'amuzi ukikosa msaada piga namba hii +255789476655.

Tatizo linaweza likawa ni nini baada ya hatua za awali kuzifata?
> Yaweza kuwa Dish ama Antenna imepoteza muelekeo wake
> Yaweza kuwa kama king'amuzi cha Dish lnb kufa
> Yaweza kuwa AC ya signal kwenye king'amuzi imekufa
Zaidi ya yote ili kupata uhakika wa nini tatizo ni fundi atakapofika sehemu ya tukio!

IKIWA UMEFANYA MALIPO NA HUPATI PICHA Bofya Hapa

mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
Share:

Nov 3, 2014

USISUMBUKE | PIGA +255658046655 | TUNAKUFATA ULIPO

Nilichogundua ni kwamba nina wadau wengi sana ambao haipiti siku bila kutembelea haka kablog chetu na kupata mawili matatu kuhusu ukanda huu..
Wengi mnataka kujua habari za ving'amuzi na huduma kwa ujumla..
Ufumbuzi wa ving'amuzi vyote upo kwenye haka kablog,maana yake ukishindwa kuelewa simu inahusika,ukipiga tu jua shida yako imeisha!


KWA KUWAJALI WATU WANGU...
Nimeanzisha huduma ambayo haikupi usumbufu na ni rahisi kwako!
Natekeleza maana ya huduma mtandaoni,kama tujuavyo huu ni wakati wa Digital hivyo lazima twende kidigital zaidi...
Swali unapenda/unataka king'amuzi gani kati ya hivi:-
DStv/Azam tv/Digitek/Continental/Zuku tv/Star times.
Piga simu sema unataka kipi,tunakupa ushauri na kisha utaletewa mpaka ulipo
Tukifika unalipia na kufungiwa papo hapo!
Ila hii ni kwa wakazi wa Dar es salaam tu!
Piga sasa +255784378129
TUMEBOBEA KUFUNGA KWENYE:-
HOTEL/APARTMENT/MAOFISINI NA MAJUMBANI.
BAADHI YA WALIONUFAIKA NA HUDUMA ZA MUSTAPHA MADISH:-
TRANSIT MOTEL/JB BELMONT/GERRAFE VIEW HOTEL/IKULU-OFFICE YA WAZIRI MKUU/PSPF/BAHARI BEACH LODGE/N.K.
Share:

Oct 27, 2014

VING'AMUZI VISIVYO NA MALIPO

Nilichogundua ni kwamba watanzania wengi wanapenda ving'amuzi rahisi,rahisi kwenye kununua na katika ulipaji wa kila mwezi na pindi linapotokea swala la kutokuwa na malipo ya mwezi inakuwa ndio unafuu zaidi,kwasababu wanzania wengi wenzangu na mie...
DIGITEK

Hiki hakina malipo ya mwezi kwa mujibu wa wao wenyewe,ukinunua kwa tsh 110,000/= 
Inakuwa umemaliza labda gharama yako itazidi ikiwa unahitaji na Antenna.
CONTINENTAL

Hiki nacho sio kama hakina ila kipo hivi,ukinunua unaangalia na kuanza kulipia baada ya miezi 12 yaani mwaka mmoja,ingawaje mpaka sasa malipo hayajaanza kufanyika.
Ya Antenna tsh 75000/=
Ya Dish tsh 105000/=

TULIPOTOKEA....
TING pia haikuwa na malipo ya mwezi ilikuwa ukinunua umenunua,lakini sasa malipo mwanzo mwisho...

MAONI | USHAURI | HUDUMA | +255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita