Leo nimeonelea niongelee hili jambo kwakuwa ukiachilia kuliona sehemu mbali mbali pia nimekuwa nikulizwa kama kuna umuhimu wa wenye ving'amuzi vya madish kuweka makopo?
Jambo la awali la kuzingatia king'amuzi kiwe cha Dish ama Antenna kina namna ya ufungaji wake kwa kutumia vifaa vyote vilivyomo kwenye set ya king'amuzi hicho,ikitokea kimojawapo umekiacha ndipo unajikuta nafasi ya kile ulichokiacha inachukuliwa na KOPO!
Kutumia KOPO kunatokana na sababu hizi:-- Tuanze kiufundi
Hapa unamshawishi mteja atafute kopo lilipo ili aweze kufunika akiamini atasaidia angalau kuepusha gharama za kuita ita fundi.
Ukifunga hivi ni kipi ambacho kitamshawishi mteja aongezee ufundi wake wa kuweka kopo?
Fikra za watanzania wengi wanaamini wakifunika na kopo husaidia:-
- Huzuia kunguru kufanya uharibifu
- Husaidia picha kutokupotea wakati wa mvua
Kupotea kwa Picha kwa dish ndogo kipindi cha mvua ni kawaida kutokana na uwezo mdogo ili kuepuka hili inakulazimu kutumia Dish kubwa ama lnb maalum na kuhusu kunguru fundi akifanyakazi yake vema kunguru hata abembee vipi hawezi kufanya uharibifu!
mustaphamadish@gmail.com