Call / WhatsApp +255673378129

Oct 19, 2010

MAFUNDI DISH AINA ZOTE

UNAHITAJI MAFUNDI WA KUFUNGA DISH KWA CHANNEL ZA BURE AMA KULIPIA!?
Upo mkoa gani,swali la kwanza la mimi kutaka kujua!
Kama upo Dar es salaam utapata fulsa ya kuhudumiwa nami ama moja ya wataalam wangu ila kama upo nje ya Dar es salaam nitakuunganisha na mafundi wenzetu walio katika mikoa hiyo na utapata huduma kanakwamba umehudumiwa na Mustapha MaDish!
Cha kufanya piga namba: +255 714973797
KARIBU!
Share:

Oct 10, 2010

Sanaa Mapenzi Yangu!!

Sifanyi sababu fulani anafanya ingelikuwa hivyo kitaambo ningelikuwa miongoni mwao,ila mapenzi yangu toka ku moyo zaidi ya yote Vipaji nilivyojaaliwa nataka kuvitendea haki.
Kimbia ukimbiavyo lakini mi nanyata so kama huna pumzi ntakukuta na kukuacha njiani,ntafika nikikungoja kukukaribisha lakini kamwe huwezi kuiba kipaji cha mtu!!
Share:

GERAFFE VIEW HOTEL - DAR

Kwenye ukumbi ambao upo baharini wanapaita JET 1,kilichotakiwa hapa ni kufunga Flat Screen na Dstv,nami bila hiyana kama kawaida ile mikono salama ukafanya yake!
* Geraffe View Hotel (DSTV)


 Katika ukumbi huu wa JET 0ne As usually.





 Nafunga Dish sasa!! 

 

 Hapa natafuta signal baada ya kufunga Dish.

  Ni DSTV kama inavyoonekana katika FLAT SCREEN hii. 

+255784378129| Technical Support
Share:

Easy TV

Kwa Tsh 200,000/=
Unapata na miezi mitatu bure!!
Inajumuisha Decoder,Antenna,Cable na Installations!
Kwa mwezi unalipia 9000/= unapata jumla ya Channels zote!
EASY TV ina jumla ya channels 32 ila zinazoonyesha ni 30 tu.
Movie 1
Movie 2
Movie3
Movie Arabic
Aljazeerah
CNN
BBC
CCTV4
UBC
Citizen
TBC 1
Star TV
Channel 10
Capital
EATV
TVZ
ITV
Clouds TV
EWTN/TV Tumaini
Mliman TV
Emmanuel TV
Peace TV
Channel V
Xing kong
Ph'x China
JSC document
JSC sport
MTV
Child
Share:

LOCAL CHANNELS

FULL INSTALLATIONS
 In Hotel.Apartment.Office.Home
Materials:
              1.Receiver
              2.Satellite Dish Antenna c band
              3.Cable
              4.LNB c band
              5.F connectors.
+ Installations
= 6 Total Local Channels.
As: TBC1,ITV,CAPITAL,EATV,CHANNEL 10,STAR TV.
Pia unapata MOZAMBIQUE (Channels 3)

Satellite Dish Antenna for Local Channels.
REPAIRING:
            * Bad signal
            * Move from 1 place to another
            * More Channels through Local S.D.Antenna.

MATERIALS:


Share:

Oct 9, 2010

DSTV EXTRA VIEW

Ni huduma ambayo haina muda mrefu sana ambayo naweza nikasema ni mpya toka DSTV inakuwezesha kuona channel 2 tofauti kwa wakati mmoja kwa kutumia decoder mbili ila a/c moja kinachozidi ni $10 tu ya malipo ya mwezi,pia unatumia dish moja ila LNB inakuwa ya njia 2 maana kila decoder inakuwa na signal yake.Hii kama utatumia decoder zote za single view lakini pia Extra view inapatikana kwenye HD pia ila decoder ya pili lazima iwe single view na ukitumia HD,LNB yake inakuwa zaidi ya njia 4.
Hii ni HD decoder na single view decoder kwa pamoja unapata Extra view service
Share:

Oct 7, 2010

HOTEL INSTALLATIONS

Tunachofanya ni kukubaliana na muhusika channel zipi anahitaji kutokana na mapenzi ya wateja,nikimaanisha channel pendwa,baada ya hapo tunainstall channel idadi iliyotakiwa then tunatengeneza master chumba maalumu,tukiwezesha vyumba vyote vya hotel kuingia channel zote zilizohitajika na kufanya kila mteja aliye chumba alichopanga kujibadilishia channel apendavyo kwa kutumia remote ya TV chumbani kwake,huku channel zikiwa na quality ya digital pasipo chembe ya chenga.
Share:

APARTMENT INSTALLATIONS

Wengi wanapenda kufunga DSTV huku local na channel nyengine zikiachwa kwa wapangaji wenyewe kama wanahitaji kutokana na ukweli kwamba wapangaji wengi wa Apartment si wenyeji wa Tanzania hivyo hawaoni umuhimu wa kuangalia channel za nyumbani wakiamini TBC inawatosha ambayo inapatikana kwenye DSTV.Ambacho kinafanyika tunainstall Dish 1 ama 2 mbili kwa apartment nzima,nikimaanisha nyumba zote za wapangaji wa humo kutakuwa na connection ya DSTV ambacho yeye anafanya ni kukunua DSTV decoder tu ambayo hata akihama anaweza kuhama nayo.Hii pia inafanya mazingira ya apartment husika kuwa nadhifu na muonekano mzuri kwa kupunguza wingi wa madish,njia hii inawezekana kwa channel za local ama nyengine pia inategemea na wapangaji husika ama mmiliki wa apartment.
Share:

C BAND SINGLE SOLUTION CABLE

Hiki ni kifaa ambacho kinauwezo wa kukabiliana na interfierence sehemu zilizo na minara mitambo mitambo nk.Pia kuna channel ambazo hazipatikani mpaka utumie Single solution cable c band LNB haijarishi kama kuna interfierence ama laa.
Share:

TOFAUTI YA RECEIVER NA DECODER

Decoder ni kifaa kinachopokea Channel ambazo zipo fixed kwa mfano DSTV,ni lazima ziwe zinalipiwa na kampuni husika,hii inamaana huwezi kupata bure labda wenyewe waamue hivyo ama upite wizi.
 Receiver ni kifaa kinachopokea channel zote zilizopo kwenye satellite,haijarishi kama ni fixed ama zipo zipo tu,ila hii inategemea na muelekeo na setting husika ikizingatiwa freequence.Haina maana kwamba hata zile za kulipia utazipata bure,zipo ambazo utazipata kutokana na ukubwa wa dish na muelekeo na huwa sio zote.
Pia kuna Receiver zinazotumia smart card hivyo unaweza ukapata channel zote za kulipia mf: channel za DSTV unaweza ukapata bila kutumia decoder zao,kitakachokulazimu ni kununua smart card yao.
Share:

Baada kufa GTV...!!

Ni wazi kwamba ni watanzania wengi wameathirika na uyeyukaji wa GTV wamejikuta wamebakia na Decoder wasijue wazifanyie nini huku wengine wakijipa imani ya kuwa ipo siku watarejea....!!
Decoder ya GTV unaweza ukaitumia kwa kutumia dish lake lile lile unaweza ukaona channel zipatazo 13 FREE,ambazo ndani yake kuna kama MBC1,2,3 ambazo zinonyesha movie sometimes mpira ambao unakuwa live ila si mechi zote,wala ligi maalumu inakuwa wenyewe tu wakijisikia kufanya hivyo wanafanya.Ukiacha njia hiyo kuna jamaa yangu mmoja ambaye nakili kusema ya kuwa amenizidi ung'amuzi kiasi kwamba amefanikiwa kuflash GTV decoder na ikawa receiver ambayo inapokea channel yeyote kutokana na matakwa yako...!!
Dish la GTV pia unaweza ukatumia kwa DSTV ama channel za Gospel ama nyengine kwa sababu Dish haichagui Receiver ama Decoder ni ufundi wa fundi tu.
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita