Call / WhatsApp +255673378129

Dec 30, 2014

NAWATAKIWA KILA LA HERI | BYE 2014 | KARIBU 2015



Namshukuru sana Allah,ni yeye ndiye aliyefanya mpaka sasa nipo hapa,wengi walitamani waifikie siku hii lakini kwa mapenzi yake hatupo nao,mpaka kufika hapa nasema Alhamdulllah!
Nakushukuru wewe mdau wangu ambaye haipiti siku bila kutembelea haka kablog chetu na kila ambaye unatembelea maana bila ya wewe wala nisingeweza kupata ambacho nakipata,ushirikiano wetu umeleta na unaendelea kuleta meengi mafanikio kwangu katika kazi yangu hii!


Sikukuu ambayo naweza kusema yenye nyimbo nyingi na mapambo imepita,wengi tukiijua kama x mass lakini sababu kuu ya kuwepo sikukuu hii ni kukumbukia siku ya kuzaliwa kwa yesu kristo!
Mwaka 2014 ndo umeishia,mwaka ambao kila mtu ana yake ya kuzungumzia mwaka huu,yanaweza kuwa mazuri ama mabaya lakini mwisho wa siku mwaka ndo umeshakatika hivyo,kama hatujatimiza yale ya msingi tuliojipangia ni jukumu letu kuangalia tulifail wapi na kisha kujipanga ili alau mwaka 2015 uwe mwaka wa mafanikio..
Mwaka huu katika ukanda wetu ndo mwaka wa mwisho kutumia Analogue,nchi nzima mwendo utakuwa ni Digital tu,ijapokuwa kuna changamoto kubwa ktk swala la network sehemu kubwa ya nchi yetu bado ni tatizo,nikizungumzia swala la mitandao ya simu,maana udigital bila ya network ni mtihani mkubwa sana,tukiacha swala la network wapo watanzania ambao mpaka sasa hawana king'amuzi na kila mtu anasababu yake,wapo ambao hawana uwezo wa kununua kabisa,wapo ambao bado wanajichanga,wapo ambao hawajui wanunue king'amuzi gani!
Mwaka 2015 mwaka ambao nitatoa ving'amuzi visivyo na idadi kwa watanzania karibu nchi nzima,kwa wale wasiokuwa na uwezo na wakafanikiwa kunishawishi mimi kufanya hivyo!
La msingi ni wewe na umwambie umpendae kwa pamoja mfatane na mimi kila hatua ntakayokuwa napiga ili niweze kukufikia na kuweza kumaliza tatizo lako!
MUSTAPHA MADISH TV SHOW

Nakutembelea ulipo,nakuuliza maswali machache tu,unauliza unachojisikia,ukinishawishi nakupa king'amuzi bureee hii ikiwa pamoja na kufungiwa papo hapo,pia kama tayari una king'amuzi na una shida za king'amuzi chako nakumalizia tatizo papohapo.
KUTOKA KWANGU KUJA KWAKO MPENDWA...
Kushindwa kufanya kila ulichopanga kufanya katika mwaka huu,maana yake si kushindwa kufanya milele,chukulia kama safari uliyochelewa kufika lakini jitahidi uwezavyo mpaka ufike hivyo mwaka 2015 jitahidi ufanye kila ambacho ulipanga kufanya mwaka huu na ukashindwa,kaa leo jiulize wapi ulikosea na kisha sahihisha makosa yako ili mwaka 2015 usiishe bure!
Zaidi ya yote nawatakia heri ya mwaka mpya!
Share:

Dec 11, 2014

MUSTAPHA MADISH | TV SHOW


Hii ni hatua nyengine nzuri zaidi kwangu na kwa wadau wangu wale wa zamani na wapya pia..
Lengo likiwa lile lile kuwaelimisha yote yanayohusu ving'amuzi,kuwaonyesha kilicho bora ili ukiepuke kilicho feki..
Ingawaje kwenye blog hii sijawahi kutoa zawadi ila kipindi kitahusisha zawadi zisizo na idadi..
Utapata kujua undani wa Digital na ving'amuzi kwa ujumla..
Nitaweza kuwasaidia wale wote wenye matatizo ya ving'amuzi bila malipo..
Na kila kipindi kimoja nitakuwa natoa king'amuzi kimoja/ama nakulipia malipo ya mwezi kwa yeyote ambaye atanishawishi kufanya hivyo..
Nategemea kutoa na tv (flat screen ) kwa wadau wangu ambao hawatakuwa na tv,ingawaje hili bado naendelea kulifanyia kazi..
Ingawaje nitaanza na Dar es salaam lakini pia nitakuwa na tour ya mikoa karibu yote Tanzania..
La kufanya ili nafasi hii isikukose ni kufatana na mimi hapa...
Lini show inaanza???
TV gani show ya Mustapha MaDish itarushwa??
Kwa wiki mara ngapi??
Na mengineyo kibao..!!
Fuatana na mimi kupitia blog hii....
Ama kwa facebookMustapha MaDish tv

MUSTAPHA MADISH | mustaphamadish@gmail.com | +255789476655

Share:

Dec 8, 2014

KUWENI MAKINI | ANAJIITA MUSTAPHA MADISHI | FACEBOOK

Mustapha MaDish mwenyewe.
Kuna wanaodhani ilikuwa ni jambo la siku moja tu na nikaweza kufika hapa ama kufanya meengi kwa wakati mmoja,ama kupata kupokea simu kwa siku mpaka unafanya kutembea na charg!
...haikuwa rahisi hivyo,ilihitajika kwanza kupenda nnachofanya,juhudi na maarifa vilihusika sana..
Ni kawaida hasa wabongo sijajua nchi za wenzetu,ambapo wewe unaumiza kichwa ili ufikie lengo fulani inapofikia either umefika ama unakaribia anatokea mtu ama watu ambao nao wanafanya kama unachofanya mbaya zaidi wanacopy na kupaste kila kitu..
Napenda kuona napata ushindani,nalipenda hili sababu linaniongezea chachu ya kunifanya nifanye kilichobora ili niwe mbora zaidi..
Pengine ndugu zangu mnaweza jisikia vibaya mkadhani naongea hivi kwakuwa mmeanzisha blog kama yangu,vile ambavyo nafanya mimi ndivyo mnafanya ninyi,binafsi najisikia fahari kwakuwa nimeonyesha njia,njia ambayo mpaka naigwa basi ni nzuri na bila ubishi si tu kwa kupitia blog yangu nimehusika moja kwa moja kwa kuwafanya mkaanzisha hizo blog,najua mnajua kwanini naongea hili,ingawaje wengine kana kwamba mnataka ligi na kusahau mimi ni mwalimu wenu tena kwa vitendo kwa kile mnachofanya,si kwa kujifunza kupitia mimi tu kwakuona bali nilianza kuwafundisha kuliunda dish ikaja kutafuta signal na sasa mmekuwa mafundi..
ILA BADO MNACHOJUA NI THERUTHI UKANDA HUU KUNA MEENGI MSIOYAJUA NA USHIRIKIANO NDIO NJIA PEKEE YA KUKOMAA KATIKA FANI HII...
Hampaswi kuleta ligi nami la msingi mnishukuru kwa kuwapa ujuzi ambao hata nife leo still mtabakiwa nao ingawaje kamwe mwanafunzi hawezi kumpita mwalimu kwa maana hakuna mwalimu anayetoa kila alichonacho...
Ila aliyenifanya niandike post hii ni huyu kijana nayejiita MUSTAPHA MADISHI kwenye facebook,awali nilipoambiwa nilichukulia kawaida tu ila sasa nimegundua watu wangu wanaenda sehemu si sahihi,lengo wanataka kunipata mimi matokeo yake wanampata mtu mwengine..
Facebook nina PAGE INAYOITWA MUSTAPHA MADISH SINA A/C YA MUSTAPHA MADISHI,A/C YANGU YA FACEBOOK INAITWA MUU ESMAILY 
TOFAUTI NI NINI HAPA?
PAGE YANGU YA MUSTAPHA MADISH haina I mwisho.
A/C YA MUSTAPHA MADISHI FAKE ina I mwisho.
Kuwa makini sana.
MAWASILIANO YANGU:
+255789476655
mustaphamadish@gmail.com

MUSTAPHA MADISH | +255789476655
Share:

Dec 7, 2014

GRAND CONFECTIONARY BAKERY LTD | ZUKU INSTALLATION


Hapa ni maeneo ya Keko Mwanga jengo la pili toka Lab Equipment,nazungumzia Bakery ya Grand Confectinary wala si la kujiuliza walitupataje ama kwanini tumefika hapa!
Mwendo ni ule ule wa kupiga no.+255789476655 unachagua king'amuzi utakacho,unasema ulipo kisha sisi tunakufata ulipo,unafungiwa na kulipa papo hapo!


Kwakuwa kazi safi ndo jadi yetu,kwanini usimwambie umpendae kama hii ndo nyumba ya ving'amuzi,gharama zetu ni za kawaida sana ambazo kila mtanzania anaweza kumudu!

MUSTAPHA MADISH | +255789476655
Share:

Dec 6, 2014

AIRTEL DIGITAL TV | KING'AMUZI CHA AIRTEL


La kwanza ambalo utajiuliza  mitandao ya simu nayo inachangamkia fursa!?
Ikumbukwe ya kuwa mwaka ndio mwaka wa mwisho kutumia Analogue,ifikapo tarehe 31 mwezi huu,saa 23:59 tunachotakiwa labda kuizungumzia Analogue tu lakini si kudeal nayo...
Lakini ambapo tunaelekea kuisahau kabisa Analogue leo hii mtu ukimuuliza ni nini maana ya Digital hajui na mwengine anajua ni King'amuzi tu kamaliza...
Kuingia mfumo wa Digital pekee bila kuhusisha Analogue ndipo imetulazimu kutumia Ving'amuzi na sababu hii ndio iliyopelekea kukawa na ving'amuzi kibao vipya achilia mbali vile vikongwe..
Airtel Digital Tv..
Hiki nacho ni king'amuzi kama ilivyo ving'amuzi vyengine vya kulipia..
Inatumia Satellite ya SES-7  Nyuzi 108.2E
Ina channels 383 ambapo za HD ni 25
Decoder yake inauwezo wa kurekodi masaa 150
Ijapokuwa mtandao wa Airtel upo hapa kwetu Tanzania lakini king'amuzi hiki kinatumia India tu kwa sasa,sina lolote la kuzungumza kama je na Tanzania kitakuja king'amuzi hiki..
Kwa maelezo zaidi kuhusu king'amuzi hiki Bofya Hapa


+255789476655 | MUSTAPHA MADISH
Share:

Dec 2, 2014

DCB HQ| DIGITEK INSTALLATION


Hapa ilikwisha fungwa Digitek muda tu ila kutokana na ujenzi wa kupanisha ghorofa mbili zaidi iliwalazimu kuitoa Antenna ilipofungwa awali na kungoja mpaka ujenzi umalizike ili itafutwe pa kufunga tena ili burudani iendelee kama ilivyo awali!
Safari hii wala sikuiweka juu kabisa kama ilivyo awali,tukafanya ya kufanya wazungu wa Digitek wakarudi kisha tukachapa mwendo!

INSTALLATION OF TV SYSTEM | IN OFFICE | IN HOTEL | +255789476655
Share:

Dec 1, 2014

ITV KWENYE DSTV

Ni mapenzi ya wateja wengi wa DStv pindi watakapoona ITV ikiwa inapatikana kwenye king'amuzi hicho na hii pia itapelekea kuwashawishi wengine ili waweze kujiunga na familia ya DStv!
ITV ni miongoni mwa channel za Tanzania zinazopendwa sana licha ya vipindi vyake na kwa habari pia,hii ndo sababu iliyopelekea kuwa na wapenzi wengi sana ndani na nje ya Tanzania.
IMESHAINGIA BOFYA NO.293!
Ili uweze kuona ni rahisi sana kama tayari umeshakuwa mteja wa DStv bofya no.293 ila kama bado hujawa mwana familia wa DStv hujachelewa piga no.+255789476655 ili upate njia rahisi ya kuwa mwanafamilia wa DStv ukiwa hapo hapo ulipo tunakufata!
Kwa mujibu wa wadau wangu DStv itakuwa imebakisha channel moja tu muhimu ambayo ni Clouds tv,hivyo kama nayo itapatikana kiu ya wadau itakuwa imekata!


HUDUMA ZOTE ZA DSTV | TUNAKUFATA ULIPO TUNAKUUNGANISHA | 0789476655
Share:

ZUKU PACKAGES | VIFURUSHI VYA ZUKU


Lengo la kuwa na vifurushi tofauti ni kutoa fulsa kwa kila mdau kuweza kununua na kufanya malipo ya mwezi kutokana na uwezo wake.
Hivi ndivyo vifurushi vya Zuku,idadi ya channel na bei kwa ujumla:-

KUPATA BEI NA VIFURUSHI VIPYA VYA ZUKU TV BOFYA HAPA
1-ZUKU SMART PACKAGE
Ina channel 30 safi.
Malipo Tsh 10,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-ZUKU CLASSIC PACKAGE
Ina channel 69 safi.
Malipo ni Tsh 18,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-ZUKU PREMIUM PACKAGE
Ina channel 100 safi.
Malipo ni Tsh 25,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 27 safi.
Malipo ni Tsh 24,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

RADIO
Ina channel 50 safi.
Bofya Hapa kujua Radio zilizopo!

+255 789 476 655
Share:

Nov 26, 2014

MIEZI MITATU BURE | TOKA KWANGU | KUJA KWAKO


Cha kwanza unachojiuliza ni miezi mitatu ya bure toka kwangu kuja kwako ni ya nini!?....
Nagawa ving'amuzi....?
Nawalipia Malipo ya mwezi.......??
Nafunga ving'amuzi bure.......??
Jibu lake ni rahisi sana....!!


1.Chukua simu yako bofya no.+255789476655
2.Chagua king'amuzi ukipendacho
au sema channel upendazo ili upate ushauri king'amuzi gani sahihi kwako.
3.Tayari una king'amuzi ila una tatizo la signal,picha inakatakata.
4.Unataka kuhama na king'amuzi chako?
5.Umenunua king'amuzi chochote popote na unahitaji kufungiwa?

MIEZI MITATU
Ikiwa tutakufungia king'amuzi chochote..
Iwe kipya,umenunua kwetu ama laa!
Iwe cha zamani ila tumekuja kukurekebishia!
Iwe tumekuhamisha toka sehemu moja kwenda nyengine!
Utapata huduma bure ndani ya miezi mitatu baada ya kukufungia/kukurekebishia kwa mara ya kwanza.
Hii ni kwa wateja wote kuanzia tarehe 01/12/2014
Hii inatokana na kujua ambacho nakifanya na kuwa na uhakika nacho ijapokuwa hata makampuni mengine ya ving'amuzi wanatoa miezi mitatu baada ya hapo unalipa pesa kila fundi anapokuja..
Kwanini ulipe mara kwa mara kwa fundi wako?
Lipa mara moja pata huduma miezi mitatu bure!
Ila hii ni kwa ving'amuzi vyote vinavyotumia Dish!
Iwe DSTV,ZUKU TV,AZAM TV,STARTIMES,CONTINENTAL
Ntabaki kuwa mbora na wengine watafata daima milele!
Ulipo nipo nawe piga sasa +255789476655
mustaphamadish@gmail.com
Share:

Nov 23, 2014

OFFER YA STARTIMES TSH 59000/=


Tarehe 24/11/2014 rasmi offer inaanza kwa wateja wote wapya!
Hii inakuwa inajumuisha na malipo ya mwezi mmoja!
Swai ambalo ungetamani kuniuliza ni je Startimes hiyo ni ya Dish ama Antenna!
Jibu ni kwamba hii ni offer kwa Startimes ya Antenna!
Wakati ni wako kuchangamkia hii offer

YOTE KUHUSU STARTIMES | PIGA +255789476655
Share:

Nov 19, 2014

OFFER YA DSTV EXPLORA


Hii maana yake Multichoice Tanzania ( DStv ) imekusudia kila mtu apate kilicho bora kwa bei nafuu na kwa wakati !
Kwa sasa ili umiliki Decoder ya Explora sio lazima mfuko wako uwe umetuuuna la!
Kwa Tsh 281,000 tu unapata Decoder yako ya Explora!
Unazijua sifa za Explora wewe!?



PIGA SIMU +255789476655 | YOTE KUHUSU DSTV
Share:

Nov 14, 2014

AZAM TV | UBUNGO FLAT

Hapa bada niwe tu mkweli,awali nilikuja kufunga Continental ya Dish ila mteja wangu huyu alinunua mwenyewe Decoder ambapo dish alikuwa nayo nilichofanya ni kufanya yangu ili Channel za Continental ziweze kumwagika bila chenga!
Yap nikafanya ya kufanya zikajaa ambapo idadi ikafika kama 90 hivi zote zikiwa buree!!
Ila kilichotokea ndicho kilichopelkekea huyu mteja kuuliza king'amuzi kingine na ndipo akaangukia kwenye hii Azam tv....!!

Mashine ikipambana na zege..

Nguvu kidogo...

Hapa mteja atanisahau!

Sababu ya kuwa tofauti na wengine..

...............!!



Baada ya hapo unadhani ntamalizaje kama si kama hivi:-
KUPATA AZAM TV | PIGA +255789476655 | TUNAKULETEA ULIPO.
Share:

UNAIJUA CABLE TV !?


Maswali yamekuwa meengi mkitaka kujua cable tv inafanyaje kazi na huku wengine mkitaka kujua namna ya kuanzisha cable tv zenu huku mkitoa ushuhuda jinsi zilivyo na wapenzi hasa mikoani kwakuwa ni rahisi sana tofauti na huduma nyengine za ving'amuzi...!!
Je kweli ni rahisi!?
Je unaweza ukaanzisha cable tv yako??
Unajua cable tv ni nini?
Nipo hapa kukujuza yote yanayohusu mambo ya tv channels,hivyo ni jukumu lako kuuliza na hata kutoa maoni yako...
Nitazungumzia CABLE TV kinagaubaga lakini naomba iwe ahadi isiwe leo,ambacho unapaswa kufanya ni kufatana nami ili usipitwe na kapost hicho hiyo siku ikifika!
JIFUNZE KUHUSU VING'AMUZI | PATA HABARI | PATA HUDUMA BORA

Share:

Nov 12, 2014

OFFER YA DSTV BADO INAENDELEA | TSH 99,000/=

 Setting zikiendelea..
Hapa ni mbezi,unaingilia maramba mawili ila huko mbele nimesahau panaitwa Mbezi gani,kwakuwa kile cha umuhimu kutakiwa kufanya nimefanya kwa usahihi kabisa hivyo tukishare picha sio mbaya!




KUUNGANISHWA NA DSTV | MAFUNDI WA DSTV | PIGA +255789476655
Share:

Nov 8, 2014

WEWE NI FUNDI MADISH | HII INAKUHUSU SANA


Hapa nazungumzia wale ambao wapo kitambo na ambao wamejiunga hivi karibuni ama hata kama unataka kuingia ukanda huu kwa mikono miwili nakukaribisha na hii post inakuhusu sana zaidi ya yote ukiyachukua yangu na kuyafanyia kazi majibu utanirejeshea!
Ufungaji wa Dish ya Azam tv..
Hivi karibuni nilikuwa pale Tandika Flat,katika ile huduma piga simu tunakufata ulipo..
Ilihitajika Azam tv nasi tukatekeleza,tulipofika kazi ikaanza kwa kuangalia pa kufungia Dish kwanza haikuwa tabu kwakuwa tayari dish nyengine tena zikiwemo Azam tv zimeshafungwa, na ndipo nikapata hii post..






Hii ni kazi ya Fundi ambaye anapewa dhamana kama ambavyo napewa mimi na wateja ila matokeo yake kinachofanyika ni kulipua kama hivi ili tu picha ipatikane ndani biashara imeisha!
Nikaona nifunge hapo hapo ili hata kama naye ni mpitiaji humu aone alichofanya alau nafsi itamsuta na kuona alivyoitendea taaluma ndivyo sivyo na mteja wake pia huku wengine mkijifunza msije kuwa kama mafundi hawa!

Ona kazi ya Mustapha MaDish...


 Tofauti hata kwa macho inaonekana!

 Ugumu upo wapi kufanya hivi..

 Angalia na uyafanyie kazi..

 Tofauti ya kazi zangu na wengine..

 Sababu ya kuitwa Mustapha MaDish..


 Setting zikiendelea..





Baada ya kudrill..

Nikiwa nimeachana na hiyo issue ya Azam tv,nikakumbuka kituko kingine nilikutana nacho Kimara,nikiwa katika huduma yangu ile ile ya PIGA SIMU TUKUFATE ULIPO..
Safari hii sio Azam tv tena...
Ufungaji wa Dish ya DStv...
Kwakweli hii ni kituko,hivi nawe mteja kabisa unakubali kazi ya fundi wako hivi!!??








Ambacho kilichofanya mpaka nianze kumshangaa mteja kwakuwa ndipo mlango wake ulipo maana yake ili aingia nyumbani kwake lazima apitie lilipo hilo dish,jibu lake ameridhika ama!?
Kiukweli kama ningemkuta wala nisingevumilia ningeongea nae mawili matatu kuhusu hilo dish...

Ona kazi ya Mustapha MaDish..






Ustadh nae...

Wale mafundi nonihino wado waliendelea kunishangaza...
Ufungaji wa Dish ya Zuku...
Palee Flat za Ubungo ndipo nilipokutana na ufundi huu..
ukipiga upepo kweli jamani hii Dish haiondoki kweli!!??
Bahati mbaya ama bahati nzuri ukifanyakazi katika hizi flat mara nyingi unapewa mwenyeji wa kuwa nae unapokuwa juu,swali je mwenyeji wa huyu fundi aliifurahia hii kazi!!??

KAZI SAFI | MAFUNDI WAZOEFU | DISH AINA ZOTE | PIGA 0789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita