Call / WhatsApp +255673378129

Sep 15, 2014

DECODER YA CONTINENTAL


Niwe mkweli kwakuwa mimi napenda kwanza muonekano mzuri wa picha hivyo inapozungumziwa HD iwe HD kweli na kama hata isiwe HD lakini muonekano wa picha uwe mzuri, king'amuzi hichi ni moja kati ya ving'amuzi vyenye muonekano wa picha mzuri sana kwa zile channel zote zinazomilikiwa na Continental.
Huu ni mwaka 2018 bei kwa sasa ni Tsh ... kwa Decoder ya Antenna na Tsh ....  kwa Decoder ya Dish ikiwa set imekamilika, hapa nikiwa na maana inakuwa na Dish, Decoder, Cable, LNB
Ufundi ni Tsh 30,000/= kwa king'amuzi cha Dish
Share:

Sep 9, 2014

HII NDIO NYUMBA YA VING'AMUZI

Mwaka 2014 ndio huu unaelekea ukingoni ambapo mwakani mwaka 2015 inatupasa nchi nzima tuwe tumeshahamia Digital huku tukiwa tumeondokana kabisa na Analogue!
Ijapokuwa kuigia Digital kulikuwa na misemo mingi,wapo waliunga mkono ambapo idadi kubwa walilalama huku kila mtu akiwa na sababu yake ila wengi wao wakilalamikia uchumi!
Ingawaje malalamiko yalikuwa meengi ila udigital tumeingia na faida zake zinaanza kuonekana.
Kuna kampuni nyingi za ving'amuzi na kwa ujumla zote zinafanya vizuri haina ubishi kuwa kila kampuni ina wapenzi wake kutokana na huduma na channel husika|
Hii Blog ipo toka hapa Tanzania kuna kampuni tatu tu za ving'amuzi DSTV,GTV na EASY TV ijapokuwa mmiliki mwenyewe ambaye ni Mustapha E.Hanya a.k.a Mustapha MaDish yupo toka enzi ya DSTV tu.
Ukomavu wangu kwenye ukanda huu umenifanya niwe msaada mkubwa kwa watanzania na wasio watanzania kwa kuwahudumia kwa mkono wangu ama kwa ushauri tu.
Nipo sahihi sana nikisema kuwa hii ndio nyumba ya ving'amuzi kwakuwa leta kesi ya king'amuzi chochote ikishindikana kwenye mikono yangu ni hakika umefail jumla.
Binafsi najisikia faraja sana kuona mimi nakuwa msaada kwa wengine,kuona wengine wanaendesha maisha yao kupitia mimi,kuona watu wanatamani kuwa kama mimi..
Sina ambacho naweza sema zaidi ya Ahsante Allah kwa kila hatua nipigayo..
Nafikiria kufanya bora zaidi..zaidi ya hili ambalo naliendeleza kwa lengo lile lile kuendesha maisha huku kuwafunua upeo wengine hasa vijana wenzangu..
kama nilikuwa mwanga kuwa mtanzania wa kwanza kufungua Blogsite inayohusu hii taaluma na ikawa ya kwanza kwa Africa mashariki na kati ni hakika nimechonga barabara wacha wengine wapite kiulaini lakini watakuwa wananishukuru si tu kwa kunifuata hata wakiwa peke yao ndani ya nafsi zao watanishukuru kama si kunizungumzia..
Ili ufikie mafanikio lazima ukumbane na changamoto na ndicho kinachotokea..
Nipo kwa ajili ya kuwahudumia watanzania na wasio watanzania,waishio Tanzania na nje ya Tanzania pia..
Niulize leo chochote kuhusu king'amuzi chochote Tanzania..
DSTV
AZAM TV
ZUKU TV
DIGITEK
TING
STARTIMES
CONTINENTAL
EASY TV
Kwa swali lolote liwe la kiufundi ama huduma kwa ujumla!
Kutaka kuunganishwa pia!
Unaweza wasiliana nami:
Kama upo facebook utafanya busara kama utalike page ya mustaphamadish
+255789476655/714973797
mustaphamadish@gmail.com

 
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita