Call / WhatsApp +255673378129

Dec 6, 2015

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI DSTV


Wateja wengi wa DStv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue vifurushi vya Dstv kwa Kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha DStv Bomba  Tsh 23,500 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha DStv Compact  Tsh 84,500 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-

1 - Washa Decoder yako,kisha weka channel namba 200.
2 - Lipia Tsh 84,500 
3 - Piga nambari 0768988800 ( Atakayepokea mwambie kuwa unahitaji kubadili kifurushi toka DStv Bomba kwenda DStv Compact nae atafanya hivyo na itapokea ndani ya dk 5 tu )

Unaweza kubadili kifurushi kwa kufata utaratibu huu kwa kifurushi chochote kile na unaweza kufanya zoezi hili hata kabla kifurushi chako hakijaisha!

+255789476655
Share:

Dec 5, 2015

EMANUEL TV | TB JOSHUA

 Ni mkristo gani ambaye ni muangaliaji wa tv na haijui Emmanuel tv? ama hamjui TB Joshua?
Pastol wa kanisa la mataifa yote..
Emmanuel tv ni tv ambayo ina wapenzi karibu dunia nzima,ni tv kubwa sana ya dini ambayo makao makuu yake ni Lagos Nigeria,imeanzishwa 8/3/2006 mmiliki akiwa ni Emmanuel Global Network,Lugha inayotumika ni English,Inarusha matangazo Africa,North/Central America na Europe!
Binafsi na team yangu tumeshafunga sana madish ili wadau waangalie hii tv inapatikana bure kama utafunga kwa kupitia Dish ndogo/kubwa na receiver ya kawaida tu unapata zaidi ya channel 65 zote zikiwa free ikiwemo hii Emmanuel tv! Ila hata katika baadhi ya ving'amuzi Emmanuel tv inapatikana ila huko ni lazima malipo ya mwezi yahusike vinginevyo huwezi kuiona!

Kwa maelezo zaidi jinsi ya kuipata channel hii na nyengine za Dini!
+255 789 476 655





Share:

Dec 3, 2015

FUNDI DISH HUJISIKII VIBAYA | KWA UCHAFU HUU!?

 Lawama zimekuwa ni nyingi kuhusu Ving'amuzi kusumbua,ambapo Ving'amuzi vinavyolalamikiwa wala havina usumbufu huo,katika kuchunguza nimegundua ya kuwa mafundi husababisha Ving'amuzi vionekane vinasumbua hata kama havina sifa hiyo ijapokuwa kweli kuna Baadhi ya Ving'amuzi vinasumbua ukiachilia uwezo wa fundi..
Baadhi ya Dish nilizowahi kukutana nazo na nikabahatisha kupiga picha ni hizi hapa chini:-

 Dish ya ZUKU tv
Badala ya fundi kutoboa na Drill yeye alichofanya ni kutafuta mawe na mbao na kufanya alichofanya kama ambavyo macho yenu yanaona hapo,matokeo yake kila baada ya muda mfupi picha itakuwa inakata kata ama hata kupotea na matokeo yake fundi hakauki kwako mwisho wa siku king'amuzi hiki kinasumbua!
 Hizi ni Dish za Azam tv
Nilikutana nazo pale Ubungo National Housing,hii ya mbele ndio mpya kwa muonekano na ya kule mwisho ya siku za nyuma kidogo,kilichofanyika hapa ni kile kile uzembe wa fundi wa kutokutoboa na Drill!

Alichofanya fundi ni kutafuta misumari ya zege na kugonga mpaka nadhani alijibonda midole kwa maana zege hili sio la kitoto..

 Baada ya kukata misumari kadhaa maana ulishindwa kuingia wote akaonelea atafute vitu vya kuweka ili kuweza kukaza kwakuwa msumari hauwezi kuingia wote,juu ya kichwa cha msumari kumewekwa bolt kwa ili pia kuweka mkaze ambao haijasaidia chochote..

 .....!!

 Kwakuwa kazi yote aliyoifanya haijasaidia kitu fundi huyu akaonelea atafute na kamjiti ili kuizuia Dish hii isishuke na kupoteza signal..

 Fundi wetu huyu akamalizia kwenye kuchomeka cable kwenye lnb,ukiachilia uchafu alioufanya hapo pia kuna kitu hajakifunga hapo ambacho kazi yake ni kufunika kabisa hayo maungio ya hiyo cable,je unayajua madhara ya ufundi huu..!!??

 Kazi ya fundi hiyoo...!!!

 Yametafutwa mawe yalipo yakapangwa kwa uchungu ili kuhakikisha signal zinapatikana na hazipotei..
Ah jamani kweli hii hata hujisikii vibaya bwana fundi..!!??

 Ile ya zege ikagongwa hapa kwa mbwembwe balaa..

 Hivi mteja wako unayemfungia ameona kazi hii?

Hii ni maeneo ya Kimara ila hii cha ajabu ni kwamba ilipofungwa mteja anaona kila kitu jinsi ilivyo sasa ambacho nimeshindwa kuelewa ameridhika na uchafu huu ama vepe!
 Hii ni Dish ya DStv

 Macho yako yameona nini hapo...!?

 Ni wazi kuwa ukuta huo haufai kubeba hii dish ila alichofanya bwana fundi akatumia ufundi wake kuonyesha yakuwa hata kama ukuta haufai yeye anauwezo wa kufanya ukafaa..

 Fundi na ufundi wao..!

 Hapa uhakika wa signal hakuna kabisa...

 Hii nadhani inatokea kwa mafundi dish wa Tanzania tu!


Hapa utalaumu King'amuzi unachotumia ama fundi aliyekufungia?
Nnachoweza kukusihi angalia sana kazi anayokufanyia fundi wako zinafanana na hizi?
JE UNAHITAJI FUNDI KWENYE KAZI SAFI TOFAUTI NA UCHAFU HUU KWA AJILI YA KING'AMUZI CHOCHOTE UNACHOKIJUA WEWE?
PIGA +255 789 4766 55



Share:

Dec 1, 2015

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI AZAM TV


Wateja wengi wa Azam tv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue Vifurushi vya Azam tv kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Azam Pure Tsh 15,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Azam Plus Tsh 23,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Lipia kwanza Tsh 23,000 kisha chukua simu yako bonyeza *150*50*5# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu Azam tv
Chagua
  1. Kiswahili <
  2. English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
  1. Angalia salio
  2. Badili kifurushi <
  3. Sajili Huduma Mpya
  4. Endeleza Kifurushi Cha Nyongeza
( Unachagua Badili kifurush,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata nia:-
  • Tafadhali ingiza namba ya Smartcard
( Weka namba za Smartcard yako,kisha una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
  1. Pure 15,000
  2. Plus 23,000 <
  3. Play 28,000
  4. Kihindi Pekee 16,000
( Unachagua namba 2,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-
  1. Badili sasa hivi <
  2. Badili baada ya kifurushi kuisha
( Unachagua namba 1,una bofya OK )

Ujumbe utakaoupata ni:-

Asante. Ombi lako linashughulikiwa. Utapata ujumbe muda si mrefu.AZAM TV

Kisha utapokea ujumbe mfupi kwenye simu yako unaotoa maelezo kama ombi lako limefanikiwa ama laa!!
Hii ni jinsi ya kuhama toka kifurushi cha Azam Pure kwenda kifushi cha Azam Plus.Utaratibu wa kuhama kifurushi ni huu kwa vifurushi vyote na ikitokea umelipia Tsh 23,000 na haujahama kifurushi itafunguka kifurushi kile kile cha Tsh 15,000 na kubaki kwenye a/c yako Tsha 5,000.Unaweza ukabadili kifurushi ndani ya masaa 72 kwa lugha nyepesi siku tatu na ikitokea imezidi hapo huna budi kupiga simu ili wakusaidie zaidi!
Zoezi hili uhakikishe king'amuzi chako umekiwasha kisha ndipo unafanya zoezi hili na inachukua dk 5 mpaka 20 kubadilika kifurushi na ukitaka kujua zoezi lako limefanikiwa baada ya muda Angalio Salio kwa kutumia utaratibu wa hapo juu!
Kwa uchache huu nadhani nimekusaidia kitu!

+255 789 476 655
Share:

Nov 26, 2015

RATIBA YA AZAM TV

Ilikupata ratiba ya king'amuzi chako cha Azam tv:-
Chukua remote yako,bonyeza 1- menu..

2- Digital TV
 

3- Programme Guide 

4- Chagua channel unayotaka kupata ratiba yake ya wiki nzima kama inavyoonekana hapo juu! 
 
5- Ikiwa maelezo hayajaeleweka kwamsaada Zaidi piga +255789476655
Share:

Nov 25, 2015

KUZIMIKA KWA VING'AMUZI BILA TAARIFA KWA WATEJA!

Idadi ya simu ninazopokea kwa takribani wiki tatu mpaka leo hii ni wateja wa baadhi ya ving'amuzi ambavyo vimekata matangazo yao bila taarifa yeyote kwa wateja wao na kitu kibaya zaidi ushirikiano unakuwa sio mzuri kwa mujibu wa wateja wanaonipigia mimi!


Ving'amuzi vilivyokata ni ZUKU tv.
Ijapokuwa ikarejea hewani ila hakukuwa na taarifa yeyote ama kuwataka radhi wateja wao.
TING nao wakapotea hewani mpaka leo hii na mchezo ni ule ule hakukuwa na taarifa wala kuomba radhi kwa kwa nguvu ile wanayotumia kuuza ving'amuzi!

CONTINENTAL pia hawapo hewani!
Ubaya ambao unatokea hapa taarifa na kuwataka radhi wateja hakuna kwa nguvu ile wanayotumia kuuza king'amuzi na kwa bahati mbaya Continental wana nafasi nzuri ya kufikisha ujumbe kwa umma kupitia Startv ama RFA lakini matangazo yanayoendelea ni yale ya kuuza ving'amuzi!
ANGALIZO TOKA KWA MUSTAPHA MADISH:
Tatizo lililopo kwa Continental na Ting ni satellite waliyopo ya Amos 5:-
Jukumu la makampuni waliyopo Satellite hii walitakiwa watoe taarifa kwa wakati kwa wateja wao ili waendelee kuwa na imani nao kwa maana ipo wazi kifundi tunajua Satellite ya Amos 5 haipo tena imepotea hivyo ili Ting na Continental ni lazima wahame Satellite je watahamia Satellite gani hilo wanalijua wahusika.
Yapo matatizo ambayo huwezi kuyazuia kwakuwa najua vema mfumo mzima ulivyo,yapo ya kuepukika na yapo ambayo hayaepukiki,ila kinachopaswa kufanyika ni kutoa taarifa kwa wakati kwa wateja wenu na kwa umma kwa ujumla huku mkiendelea kutatua tatizo kwa wakati,kukaa kimya kwenu ni kupoteza imani kwa wateja wenu,inaonekana mnatoa huduma mbovu na hii inapelekea kufanya maamuzi ya kuamua kununua king'amuzi kingine!
+255789476655
Share:

Nov 19, 2015

UNATAKA KUJUA NINI KUHUSU DIGITAL TV ?



Yapo mengi ambayo siwezi kuyamaliza kwa siku moja na pia siwezi kuyamaliza ikiwa sijajua ambacho wewe ungependa kujua kuhusu ulimwengu huu wa Digital tv na hata ukihitaji kujua yale ya Analogue tv nipo tayari kukujuza kwa kina kabisa!
Ni nini ambacho ungependa kukijua yawezekana kuhusu king'amuzi chochote kati ya vilivyopo Tanzania ama vinavyotumika Tanzania ingawaje ninauzwa nje ya nchi.Hata kama swali halihusiani na ving'amuzi ila tu linahusiana na ulimwengu huu wa Digital tv nnachoweza kusema karibu alau tuwekane sawa.

NIULIZE:
  • Chochote ambacho ungependa kujua ikiwa kutokea kule tulikotoka Analogue tv ama hapa tulipo Digital tv.
  • Jambo lolote la kiufundi ambalo linakutatiza katika ving'amuzi vyote vilivyopo.

Ili na wengine wanufaike na majibu ya maswali yatakayoulizwa naomba muulize kwenye sehemu ya ku comment nami nitajibia hapo ili maswali yasijirudie!
Share:

Nov 16, 2015

DSTV HUDUMA KWA WATEJA NA KUPATA MAFUNDI WA DSTV


Je unatumia DStv? ama unahitaji kujiunga na DSTV? 
Karibu kwa kufata utaratibu huu:-

IKIWA UNATUMIA DSTV:
  • Umelipia na bado hupati channel?
  • Picha inakatakata ama haionyeshi kabisa
  • Unataka kuhama toka nyumba moja kwenda nyengine
  • Unahitaji kuongeza Decoder nyengine ama kubadili
  • Unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu bei mpya za vifurushi
  • Unahitaji kujua chochote kuhusu huduma za DStv
  • Unahitaji Fundi 
  • Msaada wowote wa kiufundi
Dish ya DStv ikiwa kwenye setting!

Fundi akifanya ufundi wake!

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi! 

UNAHITAJI KUJIUNGA NA DSTV
  • Kujua Bidhaa zote za DStv
  • Kujua bei halisi/Offer ya kununua king'amuzi
  • Kujua bei halisi ya vifurushi Bofya Hapa
  • Kujua bei ya Ufundi
  • Kujua namna ya kuweza kuunganishwa
  • Kupata huduma ya kuletewa ulipo na kulipia baada ya kuletewa
  • Ikiwa umenunua na hujafungiwa ili upate fundi popote ulipo Tanzania
  • Yote yanayohusu DStv

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi!


Share:

Nov 1, 2015

VIFURUSHI NA CHANEL ZA STARTIMES



Ni moja kati ya makampuni ambayo yanamiliki ving'amuzi aina mbili tofauti kimasafa,nikiwa na maana ya kuwa kuna aina mbili ya Decoder za startimes:
  • StarTimes ya Antenna
  • StarTime ya Dish
Kwa kukurahisishia startimes wakati wanaanza hapa nchini walianza na mfumo wa kutumia Antenna tu,mfumo huu ukawa na lawama nyingi sana katika swala zima la kukatakata kwa picha wakaja kuboresha kwa kuleta na mfumo wa Dish ingawaje hata ule mfumo wa Antenna nao kwa sasa upo vizuri umeboreshwa!

Hivi ndivyo vifurushi vya StarTime:-

KWA KING'AMUZI CHA DISH

1- KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 11,000 Kwa mwezi
Tsh 4,000 Kwa wiki
Tsh 1,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2- KIFURUSHI CHA SMART
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 21,000 Kwa mwezi
Tsh 8,000 Kwa wiki
Tsh 2,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-STARTIMES SPORT PLUS ( Cha ziada )
Ina channels 4+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4- KIFURUSHI CHA SUPER
Ina channels 100+ bora!
Bei yake ni Tsh 36,000 Kwa mwezi
Tsh 12,000 Kwa wiki
Tsh 3,600 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5- STARTIMES CHINESE PACKAGE
Inajumuisha kifurushi cha Smart
Ina channels 84+ bora!
Bei ni Tsh 43000
Bofya hapa kujua channels zilizopo katika kifurushi hiki!

6-STARTIMES INDIAN PACKAGE 
Sasa inapatikana kama kifurushi cha ziada
Ina channels 8+ bora!
Bei ni Tsh 18000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

KWA KING'AMUZI CHA ANTENNA

1-  KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 9,000 Kwa mwezi
Tsh 3,000 Kwa wiki
Tsh 900 Kwa wiki
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-  KIFURUSHI CHA MAMBO
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000 Kwa mwezi
Tsh 6,000 Kwa wiki
Tsh 1,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-  KIFURUSHI CHA UHURU
Ina channels 80+ bora!
Bei yake ni Tsh 20,000 Kwa mwezi
Tsh 7,000 Kwa wiki
Tsh 2,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!




Kwa Maelezo zaidi
Instagram @mustaphamadish
Call / Whatsapp / Text 
+255 658 046 655
Share:

KING'AMUZI GANI BORA TANZANIA!?


Swali ambalo kila kukicha nakutana nalo kutoka kwenu..
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vilivyopo Tanzania ili niweze kukwambia kilicho bora..
Azam tv
 Continental
Coconut Digital tv
DStv
Digitek
Easy tv
Startimes
Ting
Zuku tv
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vyote vina ubora wake na mapungufu yake,itakapotokea umemiliki king'amuzi kimojawapo kati ya hivyo lazima utatoa sifa na mapungufu pia ila tatizo linakuja pale mapungufu yanapozidi sifa jibu linakuwa hakifai ila kama itatokea sifa zikazidi mapungufu jibu linakuja ndicho king'amuzi bora.
Ili ujue ni king'amuzi gani bora inapaswa kutambua wewe muhitaji vifuatavyo:-
  • Unataka kuangalia nini? ( Unapendelea channel gani )
  • Unataka kuangalia picha katika ubora upi?
  • Uwezo wako kifedha wa kununua king'amuzi na kufanya malipo ya mwezi?
  •  
Ukishajielewa wewe mwenyewe ndipo unapaswa kufanya hili la pili:-
  • Tafuta chaguo lako lilipo ( Unachotaka kuangalia kipo king'amuzi gani )
  • Ubora wa kampuni husika na Product ( Huduma zitolewazo ni katika misingi inayotakiwa )
  • Uliza kwa mtu ama watu wanaojua ( wanaotumia/waliowahi kutumia ) king'amuzi unachohisi kinakufaa ili kujiridhisha kabla ya kununua.N.B:usiulize kwenye kampuni husika kabla hujauliza kwa wanaotumia kwakuwa kama kampuni inayouza hicho king'amuzi hakitakupa jibu sahihi ila watakupa jibu la kibiashara ili ununue.
  • Uliza hapa +255789476655 tunajua ving'amuzi vyote kiundani zaidi,jibu utakalopata hapa lifanyie kazi.
  •  
King'amuzi gani unachopaswa kununua baada ya kuzingatia hayo:-
  • Ambacho kina Products nzuri na imara.
  • Ambacho kinajali wateja  
  • Ambacho matangazo yake hayakatikati kira mara pasipokuwa na taarifa.
  • Ambacho kina channel nzuri na picha safi.
  •  
Kila king'amuzi kinajitahidi kufanya kila wawezalo ili wawe wabora,wingi wa ving'amuzi umesaidia hili hivyo kila leo uboreshaji unafanyika kama unaona king'amuzi unachotumia hawana dalili ya kuboresha huduma zao unangoja nini kuhama!?
Kuna king'amuzi kilikuwa na wateja wengi sana lakini sasa ama kila kukicha idadi ya wateja inapungua,unadhani ni kutokana na nini? huduma mbovu na kutotaka kubadilika,hili makampuni mengine mjifunze laa sivyo kila kukicha watabadilishwa Ma sales Manager
+255 789 476 655 
Share:

Oct 18, 2015

OCTOBER 25 | FANYA KWELI



NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA
Popote nitasimama na kujivunia kuwa mtanzania mzawa,najivunia lugha yetu kiswahili najivunia na mengi mazuri yaliyopo nchini mwangu,nchi huru ambayo najisikia kufanya chochote wakati wowote pasi tu kuvunja sheria...
AMANI  IMESABABISHWA NA UPENDO
Ni jambo tunalojivua mpaka leo hii,sababu kubwa ikiwa ni upendo tulionao baina yetu.Daima tujitahidi kuidumisha amani hii tuliyonayo ambayo ni kama ndoto kwa baadhi ya mataifa mengine.
KIZAZI CHA DIGITAL
Kuna kundi kubwa la vijana ambao naweza kusema ni kizazi cha Digital,nikiwa na maana yakuwa ndio wenye chachu kubwa ya kutaka mabadiliko kuliko kizazi cha Analogue..
UNA KADI YA KUPIGIA KURA?
Zimebaki siku chache mnoo! swali langu ni kwamba una kikatio? ama unampigia kampeni tu mgombea unayempenda ila kura humpigii!!? Je umefikisha umri wa kupiga kura ama unabishana tu kuhusu mgombea unayeona anafaa!?
KWANINI UNAMCHAGUA!?
Unayekusudia kumchagua siku ya kupiga kura october 25,umejiuliza ni kwanini unamchagua!? Unamfahamu? Umekula pesa yake? Unaamini atatekeleza kile alichoahidi? Unampenda tu? Ama kwanini!!?
OCTOBER 25 USIFANYE MAKOSA
Kura yako itasababisha kile unachokitarajia kutokea kitokee,unahitaji tutoke hapa tulipo tuelekee hatua nyengine nzuri zaidi? kura yako ndio itakayoleta mabadiliko hayo!
Tukapige kura tuwachague wale viongozi ambao tunaona watatuletea mabadiliko,watakaotuletea maendeleo na sio vinginevyo.
TUKUBALI MATOKEO
Uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti na miaka yote kiukweli kabisa,mwaka huu ile hamasa imekuwa kubwa mno naweza kusema kile kizazi cha Digital hakitaki mchecho wanachotaka kuona mambo yanaenda sawa na si ubabaishaji.Kama ambavyo tunatokea wengi kwenye kampeni tunapaswa kutokea wengi kwenye kupiga kura pia.Jambo la kuzingatia ni kwamba tukubaliane na matokeo yatakayotokea kwa zile kura tutakazopiga.
Ili tuweze kuendelea kuilinda amani yetu tuliojaaliwa na Allah.
+255 MUNGU IBARIKI TANZANIA
Share:

Oct 15, 2015

ZUKU TV TANZANIA VIFURUSHI NA BEI MPYA


 Tsh 75000/= Unapata king'amuzi kikiwa na muda wa kuona wa mwezi mmoja.
Inakuwa na vifaa vyote kama:Dish,Decoder,LNB,Cable na stendi.
HII INAKUWA BILA UFUNDI 
Kwa sasa kuna vifurushi vinne tu navyo ni kama ifatavyo:-
  1. ZUKU CLASSIC TSH 15,500 Per Month - Channels 69. Bofya hapa
  2. ZUKU PREMIUM TSH 22,500 Per Month - Channels 100. Bofya hapa
  3. ZUKU ASIAN TSH 24,000 Per Month - Channels 27 Bofya hapa
  4. ZUKU ASIAN ( yenyewe ) TSH 32,000 Per Month - Channels 33 Bofya hapa
Kwa maelezo zaidi ama msaada kiufundi.
+255659161111/789476655
Share:

Oct 13, 2015

MIEZI MITATU BURE | TUKIKUHUDUMIA


Ikitokea umekuwa mteja wetu kwa mara ya kwanza tumekufungia king'amuzi chochote kile kati ya hivi:-
  • DSTV
  • STARTIMES
  • ZUKU TV
  • AZAM TV
  • CONTINENTAL
Tatizo lolote la kiufundi likitokea ndani ya miezi mitatu tutahusika kwa kukuhudumia pasi kulipia malipo ya ziada ikiwa halijasababishwa na mteja.
Ikitokea umetutafuta na tukakuhudumia kwa kufanya repair king'amuzi chako ambacho hujanunua kwetu,pia huduma hii itakuhusu baada ya kumaliza tatizo lako,nikiwa na maana ya kuwa baada ya huduma zetu ndani ya miezi mitatu tatizo likitokea tunakuhudumia bure.
Hii inajumuisha king'amuzi chochote kiwe cha bure ama kulipia,dish ndogo ama kubwa.

+255789476655
Share:

Oct 10, 2015

NUNUA KING'AMUZI UKIWA KWAKO


PIGA SIMU +255789476655
  • Jitambulishe na mahali ulipo.
  • Chagua king'amuzi chochote kwa matakwa yako.
  • Tutakushauri kabla hujanunua king'amuzi ulichokusudia na vyengine kama utapenda.
  • Tutakapofika muafaka unaletewa king'amuzi ulipo.
  • Na fundi anakufungia papohapo kama ukihitaji hivyo.
  • Kisha unafanya malipo ukiwa hapo ulipo baada ya kuletewa na kufungiwa.
 FAIDA ZA KUNUNUA NA KUFUNGIWA NASI:
  • Chochote kikitokea tunahusika asilimia 100
  • Fundi hatoondoka mpaka kuhakikisha umepata picha (umeona channel)
  • Ufundi ndani ya miezi mitatu ni bure baada ya kufungiwa.
  • Tupo kijamaa zaidi,wateja wetu ni ndugu zetu hivyo upo huru kuzungumza.

+255789476655
Share:

Sep 29, 2015

CHANNEL ZA LOCAL BURE | VING'AMUZI VYOTE







Utatumia king'amuzi gani!!?? Swali la kwanza ambalo naweza kukuuliza..
Najua kwa mapenzi ya king'amuzi ulichokichagua na kukinunua ukiachilia mapenzi yako ila umehitaji kuona na Local Channel maana yake uone mambo yanayoendelea nyumbani kwako ikiwemo taarifa ya habari.
Hivi unajua kama channel hizo zinatakiwa kuwa bure hata kama hujalipia malipo ya mwezi?
Pengine huzijui channel ninazozizungumzia hapa baadhi ni hizi :-
  • ITV
  • TBC
  • CLOUDS TV
  • CHANNEL 10
  • STAR TV
  • TV 1 
Je king'amuzi unachotumia salio likiisha zinabaki channel hizo!!??

Share:

Sep 6, 2015

KIFURUSHI CHA NYOTA TSH 9,000 | TSH 11,000

Kifurushi hichi kinapatikana kwenye kisimbuzi cha Dish na Anntena, ambapo kwenye Dish ni Tsh 11,000 na kwenye Antenna ni Tsh 9,000
Zijue channel zilizopo kwenye kifurushi cha Nyota:-
Kuna zaidi ya channel 30!

Channels za Dish:-
Filamu na Tamthilia
ST Zone
AMC Movies

Burudani
ST Kung fu
Startimes Real Time
E. Tv

Burudani za Kiafrika
St Dadin Kowa
TBC2
NTV Uga.
NBS
Silverbird
E Stars
ST Swahili

Michezo
ST Sports Focus

Habari
CGTN
TVC News
CNC World
NTA News 24
CGTN F
CCTV 4
Telesur Africa

Makala
 Safari tv
CGTN Doc.

Watoto
Smile of a child
Da Vinci
Mindset Learn

Chaneli za Nyumbani
 TBC
Clouds Tv
EATv
ITV
CHANNEL 10
STAR TV
TV E

Dini
St Gospel
Madani Channel
Tumaini Tv
Dove Tv
Iqraa
Upendo Tv

Muziki
Clouds Tv
Wasafi Tv

Chaneli za kwenye Kisimbuzi cha Antenna:-
Filamu na Tamthilia
ST Zone
ST Sino Drama

Burudani
ST Kung fu
Startimes Real Time
Wasafi tv

Burudani za Kiafrika
Citizen tv
E Stars
ST Swahili

Michezo
ST Sports Focus

Habari
CGTN

Makala
 Safari tv

Watoto
Smile of a child

Habari na Burudani
 TBC
Tv 1
Clouds Tv
EATv
TBC2
ITV
CHANNEL 10
STAR TV
TV E
Kwanza Tv

Dini
Arise and Shine
WRM
ATN
Tumaini Tv
Living Water
Upendo Tv
IBN Tv Africa
Iqraa
TBN

Chaneli za Tanzania
ST Guide
TBC 1
Tv 1
Channel 10
Star tv tz
ITV tz
EATV
Clouds Tv
Tv E
ATN
Safari Tv
Upendo Tv
Sibuka Maisha
Dar es salaam Only
Dira Tv
Arise and Shine
WRM
Tumaini Tv
Living Water
IBN Tv Afrika
Mlimani Tv
Tv Imaan
Kwanza Tv
Mwanza only
Barmedas Tv
Morogoro Only
Top Tv
Abood Tv
Iringa Only
Iringa Tv
Tanga Only
Tanga Tv
Arusha Only
ABC Tv

KUNUNUA | MAFUNDI | USHAURI NA MSAADA ZAIDI KUHUSU STARTIMES
MUDA  08:00 - 20:00
Piga | Whatsapp  +255789476655
Share:

Sep 3, 2015

TV 1 | IMEKUJA VIZURI SANA

Hii ni tv ya kitanzania iliyoanzishwa mwanzoni mwa mwaka jana,ambayo imejikita zaidi kwenye burudani nami nimekuwa nikiifatilia niseme tu ukweli ni tv 1 kweli kwa ambacho wanakifanya!
Inamilikiwa na kampuni ya sweden iitwayo ( MTG ) Modern Times Group.
Usiniambia kuwa hujawahi kuiona katika pita pita yako ya ving'amuzi.
Inapatikana Startimes na Azam tv hii ni ya bure wapendwa!

Share:

Sep 1, 2015

WAPENZI WA SOKA WAZIDI KULIA


Kwa siku kama nne hivi nimepokea simu nyingi sana zinazouliza kama kuna namna nyengine ya kuangalia mpira wa ligi za nje tofauti na dstv,sababu nikiuliza ni nini jibu jepesi sana ni kutokana na licha ya wadau kulalamika malipo ya mwezi yapo juu imeongeza tena toka leo hii tarehe moja na mbaya zaidi katika kifurushi cha Compact Plus hakuna tena kuona mpira kama ilivyo awali hii inamaanisha ili uangalie mpira ni lazima kulipia package ya Premium.
Kuhusu jibu njia gani nyengine ukiacha dstv unaweza ukaangalia mpira mimi naweza kusema hakuna ijapokuwa zipo,kwanini nasema hakuna ijapokuwa zipo,zote zilizopo hazina uhakika.
Kama ligi ya la liga unaweza ukaiona kupitia azam katika channel ya azam sport HD kwa tsh 15000 ambapo inakupa jumla ya channel 4 za michezo.
Wadau wanatamani kuona inatokea kampuni ambayo itakuwa unaonyesha mipira yote kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa.
Bein Sport wapo ila baadhi ya mikoa ndio inakamata,ambapo watanzania na wapenzi wa mpira walitamani ipatikane kama ilivyo awali ilipokuwa Aljazeera.
+255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita