Call / WhatsApp +255673378129

Dec 26, 2016

TUNAAGA 2016 | KWA KUJITUMA ZAIDI


Mafanikio hayana njia ya mkato,ukipata kauli za wengi wa liofanikiwa watakwambia njia walipitia na kamwe hakuna njia ya mkato.. nimejifunza kutokutamani mafanikio ya mtu bila kuwa tayari kupitia hatua za kufikia mafaniko..
Mafanikio yanahitaji:-
  • Kupenda unachofanya
  • Kukijua ama jifunze zaidi ili ukijue
  • Kuheshimu na kukitetea unachofanya
  • Kujitoa
  • Kujituma
  • Juhudi binafsi
  • Kujiongeza ( kuwa mbunifu )
  • Kuwa na heshima na Pesa
  • Kutokuwa mnyimi  ama mbinafsi 
  • Na mengineyo...
Nipo kwenye ukanda huu yapata mwaka wa nane sasa nina uzoefu wa kutosha kuhusu makampuni yote ya ving'amuzi Tanzania na watumiaji wake pia ile kiundani zaidi..
Najua nimesaidia wengi ndani na nje ya Tanzania,nimetengeneza BASE kubwa mno mpaka binafsi kama siamini hivii ila hii yote kutokana na Kupenda nilichamua kufanya n nashukuru Alhamdullah!
Mwaka unaishi na tunategemea kuingia mwaka mpya 2017
mimi na team yangu ile mikono salama #FundiMakini tunakuletea kitu kizuri sana kwenye ulimwengu wa Digital Tv... Kubwa tunashukuru kwa uwepo wenu na kutupa moyo zaidi ya yote tunawaahidi kuwaletea vitu vizuri zaidi ili kila mmoja wenu ahufurahie ulimwengu wa Digita Tv!
+255 789476655
Share:

Dec 2, 2016

TV E TANZANIA | KWENYE KING'AMUZI CHAKO



Siku zote ili ufanye vizuri ni lazima upate mpinzani na ndicho kinachotokea hapa..
Historia inaonyesha Clouds Fm ilifanikiwa kuzipoteza radio ambazo alizikuta katika swala la burudani na kupelekea kuunyanyua kwa kiasi kikubwa music wa Bongo Flavour,mpaka ikafikia hatua hata kwa wasanii wa music huo ukienda kinyume na matakwa ya uongozi wa radio hiyo kinachotokea ni kupotea katika game ya Bongo Flavour hapo hapo bado kuna malalamiko mengi ya kwamba kuna unyonyaji!
E - Fm radio,ndio radio pekee inayoonekana imekuja kuleta upinzania mkubwa kwa radio Clouds Fm katika swala zima la burudani.. E - Fm radio wamefanikiwa kuufanya music wa Singeli kuwa biashara.. ukiacha hilo kwa mtazamo wa haraka haraka tu ni kwamba mmiliki wa E - Fm anakijua sana anachokifanya kwakuwa yupo kwenye ukanda huo muda mrefu hivyo alichoangalia udhaifu wa wengine nae akaongeza ubunifu na ndicho kinachompa na kitakachompa mafaniko zaidi..
E - Fm imepelekea kuzalisha TvE - Tanzania ni hatua nzuri sana na ya kupongeza mno..
TvE - Tanzania inapatikana kwenye ving'amuzi vifatavyo kwa sasa:-
  • Azam Tv - channel namba 115
  • DStv - channel namba 295
  • StarTimes channel namba 115
Binafsi nawatakia kila la heri katika kuboresha ili kutuongezea machaguo wapi tuangalie ama kusikiza
+255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita